Album 50 Maarufu zilizong'arisha zaidi muziki wa Kizazi kipya. (BONGO FLEVA)

Torch

JF-Expert Member
Aug 11, 2013
1,200
1,116
MUZIKI WETU.
----------------------

ALBAMU 50 MAARUFU ZILIZOUNG'ARISHA ZAIDI MUZIKI WA KIZAZI KIPYA. (BONGO FLEVA)

Bado tunaendelea kuwaletea mwendelezo wa Makala zinazozungumzia kumbukumbu za chimbuko la muziki wa kizazi kipya nchini maarufu kama Bongo Fleva.

Tukumbuke tu kuwa, wengi wetu (nikiwemo mimi mwenyewe) tumekuwa tunajifunza mengi sana kupitia michango ya jumbe mbalimbali (comments) zinazotolewa na baadhi ya wachangiaji wenzetu, kutokana na pengine wao kuyajua mengi zaidi yanayouhusu Muziki huu kuliko sisi, hivyo basi ni vyema pia tukajikita kusoma comments za wadau ili kuyajua mengi zaidi.

Niseme pia, Ni vigumu kwangu kukumbuka kila msanii au kila kinachohusu muziki huu, hivyo kiungwana kabisa nitarajie na nikaribishe pia kurekebishwa na ikiwezekana kuongozwa na wajuzi zaidi kutokana na kile ninachokieleza.

Niombe basi kupitia jukwaa hili tushirikiane pamoja kwa kutoa kila aina ya jambo au neno litakalosaidia wengi kuyajua mengi zaidi kupitia muziki huu unaopendwa zaidi kwa sasa kuliko muziki wowote mwingine.

Ebu nisiwachoshe sana, wacha moja kwa moja nikuwekee orodha ya Albamu 50 maarufu zilizotolewa na wasanii mbalimbali katika nyakati tofauti tofauti za ukuaji wa muziki huu na kupelekea ushawishi mkubwa kwa baadhi ya vijana wengi kujikita katika tasnia ya muziki huu.

Niwakumbushe tena kuwa, mpangilio wa namba za albamu zilizoorodheshwa kwenye mtiririko huu hazimaanishi ubora kati ya Albamu zilizo juu ya namba au udhaifu kwa Albamu zilizo chini ya namba.

ORODHA.

1. Sauti ya Dhahabu - TID.
2. Tropical Tekniqs - KWANZA UNIT.
3. Funga Kazi - HARD BLASTERS.
4. Ni Mimi - 2 PROUD.
5. Simulizi la Ufasaha - GANGWE MOBB.
6. Nini Chanzo - JUMA NATURE.
7. Kwanzania - KWANZA UNIT.
8. Machozi - LADY JAYDEE.
9. Mwanafalsafani -MWANAFALSAFA.
10. Ulimwengu ndio Mama - JAY MOE.

11. Machozi Jasho na Damu - PROF J.
12. Nje ya Bongo - Mr 2.
13. Ugali - JUMA NATURE.
14. Nje Ndani - GANGWE MOBB.
15. Rafiki - MR NICE.
17. Binti - LADY JAYDEE.
18. Mwana Mnyonge - Q CHIEF.
19. Historia ya Kweli - DULLY SYKES.
20. Ukweli Mtupu - WAGOSI WA KAYA.

21. Subra - BANANA ZORRO.
22. Taswira - MANDOJO & DOMOKAYA.
23. Fahari Yako - MR EBBO.
24. Homa ya Dunia - SOLO THANG.
25. Nawe Milele - RAY C.
26. Kamanda - DAZ NUNDAZ.
27. Majobless -BIG DOG POSSE.
28. Darubini Kali - AFANDE SELE.
29. Ni Saa ya Kufa kwangu -DUDU BAYA.
30. Ndio Zetu - TMK WANAUME.

31. Nitakupa Nini Mama - CRAZY GK.
32. Mazimwi -GWM.
33. Safari - FEROOZ.
34. Ripoti Kamili - WAGOSI WA KAYA.
35. Mzee wa Busara - WACHUJA NAFAKA
36. Maashallah - AFSA KAZINJA.
37. Mapinduzi Halisi - PROF J.
38. Girlfriend - TID.
39. Kitambo Kidogo - BDP.
40. Kufa au Kupona - KIKOSI MIZINGA.

41. Muziki na Maisha - SUGU.
42. A.k.a. Mimi - ALBERT MANGWEAR.
43. Bembeleza - MARLAW.
44. Elimu Dunia - DAZ BABA.
45. Vina Kati, Mwanzo na Mwisho- FID Q.
46. Ng'e 1982 - ALBERT MANGWEAR.
47. Siamini - MATONYA.
48. Amri 10 za Mungu - DUDUBAYA.
49. Handsome - DULLY SYKES
50. Ice Ice Baby - SALEH JABIR.

#MuzikiTanzania

Source: KADO COOL fb page

Sent using Jamii Forums mobile app
 
FB_IMG_1579696196676.jpg
FB_IMG_1579696203749.jpg
 
Kiranga,
Umenikumbusha mbali sana.. By the way UGALI ipo namba 13.
Kuna vikundi hapo vipo tangu Nigger J (later Professor Jay kama alivyobatizwa na DJ John "Mbatizaji" Dilunga Matlou) hajaruhusiwa kushika mic Hard Blasterz, alikuwa mbeba jezi tu na mbandika mabango.

Jay alikuwa chembambaaa, ukimuona leo shavu utasema kweli hakuna mtu mwembaba, ni mazingira tu.

Leo nikikutana naye mheshimiwa Mbunge.

Tumetoka mbalii.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom