Wadau,
Leo asubuhi nilikuwa nikiangalia kipindi cha jicho letu ndani ya habari ambacho hurushwa na Star TV kila Jumamosi. Wageni waalikwa kwa upande wa DSM alikuwa Pascal Mayala na mwingine simkumbuki jina.
Kwa upande wa Mwanza, walikuwepo vijana wachambuzi wazuri na wanaonekana wana weledi mkubwa wa mambo ya habari, ulipofika wakati wa fursa ya upande wa DSM, nimewashangaa waandishi hawa Pascal Mayala na mwenzake ambao wameamua kwa makusudi kujitoa ufahamu wakitetea kwamba Mkapa kuwaita watu wapumbavu na malofa si tusi!
Hisia niliyopata ni kwamba CCM wamepanga watu wao katika baadhi ya vyombo vya habari ambao watakuwa wanachambua lakini kwa kuwatetea, pamoja na kwamba inawezekana ni mkakati wa kisiasa lakini binadamu unapolazimika kutamka kitu ambacho kinaenda tofauti na dhamira yako unakuwa mtumwa.
Kwa kweli kwa mara ya kwanza nimemuona Pascal Mayala akijivisha nafsi isiyo ya kwake. Waandishi msijidhalilishe kiasi hiki, uchaguzi utapita lakini madoa na makovu ya kujidhalilisha huchukua muda mrefu kwisha.
Nawasilisha