- Thread starter
- #21
Elewa maana ya uchambuzi, sio kila mchambuzi achambue unvyotaka wewe.
Tunachotaka ni uchambuzi wa kutumia common sense hata kama unaambiwa kupendelea, Mambo ya kutwambia kwamba beleshi ni kijiko kikubwa huo ni kutufanya majuha
Elewa maana ya uchambuzi, sio kila mchambuzi achambue unvyotaka wewe.
Vyombo vya habari vimegawanyika vingi vinafanya kazi kishabiki kwa sasa jambo ambalo ni baya sana kwa kipindi hiki
Mkuu Ndagla, asante kunishtua!.Ngoja aje atolee ufafanuzi Pascal Mayalla.
Wadau,
Leo asubuhi nilikuwa nikiangalia kipindi cha jicho letu ndani ya habari, waalikwa Pascal Mayala na mwingine simkumbuki jina. nimewashangaa waandishi hawa Pascal Mayala na mwenzake ambao wameamua kwa makusudi kujitoa ufahamu wakitetea kwamba Mkapa kuwaita watu wapumbavu na malofa si tusi!
Hisia
Hisia ni haki ya kila mtu ambayo unao uhuru nayo kwa asilimia 100% kuhisi chochote juu ya jambo lolote au kumhusu mtu yoyote, hakuna mwenye uwezo wa kuzuia hisia za mtu yoyote!.niliyopata ni kwamba CCM wamepanga watu wao katika baadhi ya vyombo vya habari ambao watakuwa wanachambua lakini kwa kuwatetea, pamoja na kwamba inawezekana ni mkakati wa kisiasa lakini binadamu unapolazimika kutamka kitu ambacho kinaenda tofauti na dhamira yako unakuwa mtumwa.
Kwa kweli kwa mara ya kwanza nimemuona
Kwa vile ndio umeniona kwa mara ya kwanza nikijivisha nafasi isiyo ya kwangu, jee wewe kwa ufahamu wako nafasi stahili au stahiki yangu ni ipi?!.Pascal Mayala akijivisha nafsi isiyo ya kwake. Waandishi msijidhalilishe kiasi hiki, uchaguzi utapita lakini madoa na makovu ya kujidhalilisha huchukua muda mrefu kwisha.
Nawasilisha
Mkuu Ndagla, asante kunishtua!.
[/B][/FONT]
Mkuu Emalau, kwanza asante kwa uzi huu ambao pia unanipa fursa ya kupata mrejesho wa kile nilichokiongea leo asubuhi pale star TV.
Naomba kuanza kwa msisitizo kuwa kumtukana mtu mpumbavu au lofa, ni kumtukana tuu lakini sio kumtukana matusi!. Kuna kutukana na kuna kutukana matusi, sio kila kutukana ni kutukana matusi, ila kila kutukana matusi ni kutukana!.
Neno Mpumbavu sio tusi, wala neno lofa sio tusi!, bali ni matukano!.
Kwa faida ya wale ambao hawakutazama na kusikia nilisema nini,
Hiki ndicho nilichosema.
Namfahamu Mkapa, katika kipindi chake chote cha miaka 10, mimi tayari niliishakua mwandishi, nimemcover sana na nimesafiri nae kwenye baadhi ya ziara zake hadi za nje ya nchi!, nikasema Mkapa ni hot tempared man, yaani mtu anayehamaki wka haraka na anayekasirika kwa urahisi, nikatolea mfano mahojiano yake na Tim sebatian katika kipindi cha Hard Talk, kilichorushwa na BBC TV, Mkapa lihamaki hadi akaulizwa "are you angry Mr. President?", akajibu "Yes, I'm very angry!". (BBC World Hardtalk with Tim Sebastian - YouTube) hivyo nikasema Mkapa alitukana kwa sababu amekasirika, ila matukano hayo sio matusi!, na hawezi kushtakiwa kwa sababu hakutaja jina la mtu yoyote, ila kilichoandikwa na gazeti la Mawio kumjibu Mkapa, ni matukano ya matusi, ni uchochezi na yanashitakika
Nikasema hata Nyerere alipokasirika alikuwa anatukana tena sio mara moja wala mbili ameatukana watu wapumbavu, wajinga, wahenzi, wahuni, mahayaani, mazuzu, kaburu, na hadi kutukana ka kikabila kama "manzi ga nyana!", etc, ila vyombo vya habari havikushupalia matukano hayo!.
Nikasema kwa level ya Mkapa kama rais mtaafu hakupaswa kutukana nikasema its inappropriet, sio sahihi, nikasisitiza wenye jukumu la kumkanya Mkapa ni Tume ya Uchaguzi na Msajili wa vyama!.
Pia nikasema kuna waandishi makasuku, ambao kila watakalolisikia, wataliandika kama lilivyo kama wafanyavyo kasuku yaani 'parroting journalim', na kuna waandishi maripota ambao kile watakachokisikia watakitafakari na kuripoti kile tuu kitakachoisaidia jamii. Pia nikazungumzia wajibu wa vyombo vya habari wakati wa uchuguzi, ni kuwasaidia watanzania wafanye informed decision kuchagua kiongozi bora.
Hisia ni haki ya kila mtu ambayo unao uhuru nayo kwa asilimia 100% kuhisi chochote juu ya jambo lolote au kumhusu mtu yoyote, hakuna mwenye uwezo wa kuzuia hisia za mtu yoyote!.
Lakini unapohisi jambo ambalo sii la kweli, then hisia hizo ni za uongo, kwa vile mimi sio mwana CCM siwezi kukubishia kama CCM wamepanga watu wao kwenye baadhi kujifanya achambuzi ili kuitetea CCM. Mimi sii manachama wa CCM, wala chama chochote cha siasa, hivyo sijapangwa na yoyote wala sijakwenda kutetea lolote bali nilisisitiza watanzania tuwe tayari kuupokea ukweli hata ukiwa ni ukweli mchungu kiasi gani, ndio ukweli wenyewe!
Kwa vile ndio umeniona kwa mara ya kwanza nikijivisha nafasi isiyo ya kwangu, jee wewe kwa ufahamu wako nafasi stahili au stahiki yangu ni ipi?!.
Paskali.
Mkuu kivava, kwanza naheshimu mchango wako ndio maana nimekutupia like, pili ili watanzania tuweze kusonga mbele, ni lazima kwanza tuukubali ukweli, hata ukiwa ni ukweli mchungu kiasi gani!, pili tuukatae uongo, na kujitahidi kadri ya uwezo wetu, kuuepuka uongo. Katika mada hii ukweli halisi bila chenga ni kuwa maneno wapumbavu na malofa sio matusi, bali ni matukano tuu, kuna matukano ya kawaida, yaani kutukana tuu, na matukano ya matusi, yaani kutukana matusi, hivyo naisitiza mimi sijasema uongo kutetea kibarua changu!.Paschal Mayala analazima kusema uongo kulinda kibarua chake cha kutangaza nane nane na saba saba
maneno 'pumbavu na lofa' yameanza lini kua tusi? au kiswahili hukijui?
Ukitaka kufahamu maana ya maneno hayo muite mzazi wako pumbavu !
Juha wee!
Viongozi wa CCM wanawadharau sana Watanzania,hayo matusi yote tuliyoitwa yanatosha sasa TUTAKUTANA OCTOBER 25 kwenye kupiga kura.
Mkuu kivava, kwanza naheshimu mchango wako ndio maana nimekutupia like, pili ili watanzania tuweze kusonga mbele, ni lazima kwanza tuukubali ukweli, hata ukiwa ni ukweli mchungu kiasi gani!, pili tuukatae uongo, na kujitahidi kadri ya uwezo wetu, kuuepuka uongo. Katika mada hii ukweli halisi bila chenga ni kuwa maneno wapumbavu na malofa sio matusi, bali ni matukano tuu, kuna matukano ya kawaida, yaani kutukana tuu, na matukano ya matusi, yaani kutukana matusi, hivyo naisitiza mimi sijasema uongo kutetea kibarua changu!.
Kwa kusaidia zaidi, naomba tutembelee kamusi ya Kiswahili sanifu na kutafsiri maneno yafuatayo,
apumbavu, lofa, matusi, kutukana, na kutukana matusi.
Paskali.