Waandishi wapewa saa mbili kuihama Bukombe

Mtanzania

JF-Expert Member
May 4, 2006
4,816
678
Wanasiasa wataendelea kunyanyasa waandishi wa habari mpaka lini?
Waandishi wapewa saa mbili kuihama Bukombe


Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bukombe mkoani Shinyanga, imewakataza waandishi wa habari wanne akiwamo mwandishi wa gazeti hili, Raymond Mihayo kufanya shughuli za kiuandishi na kuwapa saa mbili wawe wameondoka katika maeneo ya wilaya hiyo.

Kwa mujibu wa barua iliyotolewa Machi 25 kwenda kwa Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga, waandishi wengine na vyombo vyao kwenye mabano waliofukuzwa wilayani humo ni Anicet Nyahole (ITV/Radio One), Mohab Domonic (Nipashe) na Peter Makunga wa Tanzania Daima.

Barua hiyo iliyotolewa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya hiyo ya Bukombe, ilitoa sababu za kuwatimua waandishi hao ambazo ni kuandika habari zenye nia ya kuihujumu wilaya kwa kuupotosha umma, na kutozingatia maadili ya uandishi wa habari.

Barua hiyo ilitolea mfano habari hizo kuwa ni iliyohusu ‘Mauaji ya vikongwe ni dili kwa polisi, wilaya kukabiliwa na njaa ifikapo Mei na iliyohusu Misitu ya Hifadhi iliyopo wilayani imejaa wahamiaji haramu’. Gazeti hili lilipozungumza na Mkuu wa Wilaya ya Bukombe, Magesa Mulongo, kwa njia ya simu alikiri kuandikwa kwa barua hiyo. Hata hivyo Mulongo alisema lengo la kuandika barua hiyo ni kukipa taarifa Chama hicho cha Waandishi ili kiweze kuchukua hatua dhidi ya wenzao.

Alisema wameshajibiwa kuwa chama hicho kitakaa Aprili 15 mwaka huu kuwajadili waandishi hao na baada ya hapo, kitatoa majibu kwa ofisi ya Mkuu huyo wa Wilaya. Malongo alidai waandishi hao wamekuwa wakichukua rushwa kutoka kwa wananchi ili waweze kuandika habari zao pamoja na kuandika habari za uzushi na alipowaita kuthibitisha baadhi ya habari zao, walikiri kuzusha habari hizo na kuongeza kudai, “mwingine ni mlevi na amewahi kulewa na kumtukana Mbunge hadharani”.

Mbali ya kukiri kuandikwa kwa barua hiyo yenye kumbukumbu namba CM.30/B/3/vol. XII/33, alikanusha taarifa zilizomo ndani yake kuwa ofisi yake imetaka waondoke wote na kufafanua kuwa wanaotakiwa kuondoka ni watatu na Peter Makunga, ambaye wilayani Bukombe ni nyumbani kwao ameruhusiwa kubaki. Wengine kwao ni wilaya za Shinyanga na Kahama. “Mimi sina uwezo wa kuwazuia kufanya kazi, waje lakini wafuate maadili ila kwa sasa tunasubiri uamuzi wa chama chao dhidi yao na tumekuwa tukifanya mazungumzo na Mwenyekiti wao mkoani hapa,” alisema.

Kwa mujibu wa Sheria ya Tawala za Mikoa ya mwaka 1997, Mkuu wa Wilaya ndiye mwenye jukumu la kuhakikisha kunakuwa na usalama wilayani mwake na amepewa madaraka ya kuamuru kukamatwa kwa mtu atakayeona anahatarisha amani na usalama ambapo mtu huyo atatakiwa kufikishwa mahakamani ndani ya saa 48. Pia sheria hiyo inaeleza kazi za Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya kuwa ni kuhakikisha kunakuwa na ulinzi na usalama katika wilaya husika.
 
Hiyo Sheria ya Tawala za Mikoa ya mwaka 1997 haina maana. Inawafanya hawa wakuu wa wilaya wawe kama maamiri jeshi wa wilaya vile - wanaingilia kazi za polisi. Kwa nini utunzaji amani na usalama wasiachiwe polisi?
 
tanzania is increasingly tending towards being a complete police state.

Hivi hawa wakuu wanajua kazi za mahakama?
 
Mkuu wa wilaya anakiuka Katiba ya nchi,kuna kipengele kinachosema mtanzania ana haki ya kuishi au kwenda popote bila kubugudhiwa.Hii ni ishu nzito yua kikatiba,waandishi wasikae kimya ili kuwakomesha kabisa hawa wakoloni
 
Wasitusumbue hawa vibaraka wa MAFISADI kwani wanataka kukataa kuwa hakuna vitu kama hivyo vilivyoandikwa? Walichotakiwa ni kuthibitisha kama hakuna mambo kama hayo na wala siyo kutimua waandishi.
 
Back
Top Bottom