Waandishi wa habari watimuliwa msafara wa waziri mkuu Ruvuma

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
images


Na Gideon Mwakanosya,Songea


WAANDISHI wa habari wawili wawakilishi wa vyombo vya habari tofauti mkoani Ruvuma wamefukuzwa kawenye ziara ya waziri mkuu wa Jamhuri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda kwa kushutumiwa kuandika habari ya ajali iliyotokea kwenye ziara hiyo wakati msafara wa waziri mkuu ukitoka wilayani Tunduru kuelekea wilyani Namtumbo.


Habari zilizopatikana jana mjini Songea ambazo zimethibitishwa na katibu wa chama cha waandishi wa habari wa mkoa wa Ruvuma Andrew Chatwanga zimeeleza kuwa tukio la kufukuzwa kwa waanahabari hao wawili limetokea jana majira ya saa 1.45 katika eneo la Ikulu ndogo ya mjini Songea wakati msafara huo unatarajia kuondoka kuelekea wilayani Nyasa.


Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wakiwemo waandishi wa habari wa mkoani Ruvuma ambao walionyesha kushangazwa na tukio hilo la mwandishi wa habari wa ofisi ya waziri mkuu Said Nguba kuwahoji kwa nyakati tofauti wanahabari hao wawili kuhusiana na tukio la ajali iliyotokea juzi kwenye ziara hiyo ya waziri mkuu ambayo ilisababisha magari manne kugongana na kusababisha taharuki kwenye msafara huo huku baadhi yao kujeruhiwa.


Walisema kuwa mara baada ya ajali hiyo kutokea kulitolewa maelekezo na Afisa habari wa mkoa wa Ruvuma Revokatus Ksimba mbele ya waandishi wa habari waliokuwepo kwenye eneo la tukio kuwa taaifa hiyo ya ajali isitangazwe kwenye vyombo vya habari kwa madai kuwa haina madhara makubwa kauli ambayo ilipingwa pale pale na baadhi ya waandishi wa habari .


Ajali hiyo ilihusisha magari manne yenye namba za usajili PT 1437 Mali ya jesji la polisi,STK 7929,DFP 6627 na DFP 8709 iliyokuwa imewabeba baadhi ya waandishi wa mkoa wa Ruvuma pamoja na Afisa habari wa mkoa huo ambaye anadaiwa kuwa alipewa maelekezo na baadhi ya waandishi wa habari waliotoka jijini Dar Es Salaam pamoja na mwandishi wa habari wa ofisi ya waziri mkuu ambao walitoa maelekezo kuwa ajali hiyo ni ndogo na haina haja kuandikwa na kutangazwa kwenye vyombo vya habari jambo ambalo baadhi ya waandishi wa habari wa mkoa wa Ruvuma walilipinga kwa sababu wao ndiyo wahanga.

Katika ajali hiyo jumla ya waandishi habari nane wa mkoani Ruvuma walikuwemo kwenye magari mawili kati ya magari manne yaliyopata ajali hiyo iliyotokea kwenye kijiji cha Namingwea wilayani Namtumbo kwenye msafara huo.


Hata hivyo katibu wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Ruvuma Chatwanga alionyesha kusitikishwa na kitendo cha kuwafukuza waandishi wawili ambao ni Nathan Mtega mwakilishi wa ITV na Radio One Stereo mkoani Ruvuma na Ngaiwona Nkondola mwakilishi RFA na STAR TV Mkoani Ruvuma ambao wanadaiwa kuandika na kutangaza habari za tukio hilo la ajali iliyotokea wakati wao kama wanataaluma wa tasnia ya habari wamehabarisha jamii yaliyojiri kwenye msafara huo.


Hata hivyo jitihada za kumpata mwandishi wa habari wa ofisi ya waziri mkuu Nguba zimeshindikana kwa kuwa bado yuko kwenye msafara huo wa waziri mkuu.

 
Kuingilia uhuru wa vyombo vya habari!!

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Ajali ilikuwa ndogo na kwamba haikuwa na athari! Kama haina athari basi hata ikiandikwa haitakuwa na athari. Kumbe siku hizi habari zinachaguliwa ipi iwe habari na ipi isiwe habari? Wakome kuwa kwenye msafara wa "wapigwe tu"
 
Nyie waandishi wa habari tumeshawaasa sana mnajifanya wajuaji.Taaluma yenu sasa imekuwa kama ubaamedi (very sorry).
Jukwaa la wahariri halina nguvu wala tija kwa ufupi nyie ndio mnaochelewesha ukombozi wa taifa hili ndio maana hata Wakenya wanawachorea katuni kwa jinsi mnavyojidharaulisha.
Najua kwa tukio hili hamtachukua hatua yoyote pamoja na kufukuzwa kama kuku.
Toka mlivyomgeuka Kubenea eti aombe msamaha ikulu mlitoa picha ya ajabu kweli.
Yakiwapata mnalialia kama yatima while mmetengeneza mazingira ya kutoheshimika.
Tena subirini kuelekea 2015 muone mtavyotumika tena kwa hela mbuzi na baada ya uchaguzi mtabaki na umaskini ule ule.
Fanyeni mapinduzi mheshimike.
 
Tatizo lenu nyie waandishi wa habari hamna umoja kabisa,nilitegemea kukuta habari inayosema waandishi wa habari wasusia msafara wa PM baada ya wenzao kufukuzwa kwa kuandika habari za ukweli!Shame on you!Lingekuwa ni gari la CHADEMA limeingilia msafara lakini hakuna aliyeumia pia mngeambiwa msiandike ni habari ndogo??
Tatizo la WTz sijui akili zao zimeenda likizo?Umuhimu wa kuandika habari hiyo ni kuzisaidia mamlaka husika kufanya uchunguzi ili ajali kama hiyo isiweze kujitokeza.Mfano unaweza kukuta chanzo cha ajali ni fatigue,dreva alikuwa anasinzia kidogo gari likamshinda nguvu.Sasa mnaangalia ni kitu gani kinasababisha fatigue kwa madereva,je hawapumziki vya kutosha then if so mnaweka madereva wawili kwa kila gari!Endeleeni kujifanya hamna kilichotokea tutasikia msiba wa kitaifa muda sio mrefu.
 
Tatizo la waandishi wa habari wa bongo ni njaa, mtu kama Pinda siwezi kupoteza muda naye..! Hana la maana la kuweza kumpa coverage, sana sana ni yaleyale ya kulia mbele za watu..!
 
PM hakuamrisha wapigwe tu? Au ilishindikana kwakuwa wapigaji (polisi) nao walikuwa wanaugulia maumivu baada ya gari lao pia kuhusika? Hata hivyo poleni.
 
Mbona hawaandiki habari za maendeleo au zenye kumsaidia mkulima,wawafukuze tu hawa wambea


Walikuwa kwenye msafara wa waziri mkuu kwahiyo lolote lililojitokeza katika msafara huo ni haki ya wananchi kujua na ndio maana walifanya hivyo. Habari za kumsaidia mkulima si mbaya zikaandikwa na habarileo, jambaleo, dailynews na tbccm.
 
Mtazamo mdogo wa serikali legelege ya Jk + pinda ndiyo faida yake hii!

Na angepigwa ingependeza!
Damu ya Watanzania wasio na hatia unafikiri itaenda bure?
 
Viongozi wa tz wanajisahau sana,
Hivi kwa akili za pinda alijua watu hawatajua hata kama waandishi wasingekuwepo,
kweli kusoma siyo kuelimika.

Unajua kuna watu bado wanalazimisha 1948 iwe ni leo na wanasahau kabisa ulimwengu wa leo ni kijiji, leo maisha ni dotcom, kweni watu wa Ruvuma hawana simu? Raia wa pale gari zilipopata ajali hawana simu? watu wa Ruvuma hawajui kuandika Message? Hawajui kutuma email? Hivi kweli huko kwenye ajali hakuna vijana waliomaliza shule na wana simu ambazo wanauwezo kutuma message? wanashindwa vipi kulielewa hilo au akili zao zimeganda?
 
Kwa akili zao bado hawajui kuwa dunia ipo kiganjani,
ndiyo maana nchi wanaiendesha kama enzi za miaka ya 40
wakijua watanzania hawawaoni, ole yao, tena ole yao ya herufi kubwa.

Unajua kuna watu bado wanalazimisha 1948 iwe ni leo na wanasahau kabisa ulimwengu wa leo ni kijiji, leo maisha ni dotcom, kweni watu wa Ruvuma hawana simu? Raia wa pale gari zilipopata ajali hawana simu? watu wa Ruvuma hawajui kuandika Message? Hawajui kutuma email? Hivi kweli huko kwenye ajali hakuna vijana waliomaliza shule na wana simu ambazo wanauwezo kutuma message? wanashindwa vipi kulielewa hilo au akili zao zimeganda?
 
Nahisi PM aliingia JF na kuziona zile kauli zilizopostiwa na wadau wakisema bora angekufa. Zilimuuma sana kaamua kumalizia hasira kwa waandishi wa habari. Maamuzi haya ni kuingilia uhuru wa wanahabari na vyombo vya habari. Huu ni ufinyu wa mtazamo uliopindukia, kwani hata alipowatimua amebenefit nini? Anafikiri akipata ajari tena watu hawataripoti? Hajui powerful JF media ipo kila mtaa? Kweli majanga!
 
Tasnia ya Habari Tanzania bado tuna safari ndefu sana , wanahabari wasipobadilika na kujijengea uwezo ,umoja na kusimamia maadili "HATUTAFIKA"
 
hata wakiwafukuza , habari za tukio hilo zishatufikia "vitengo" na tumeshaweka kwenye "hansard" zetu za milele. Zidumu fikra za mwalimu na chama .
 
Back
Top Bottom