King Mgogo
Member
- Dec 6, 2025
- 54
- 74
Siku mkija kujitambua ninyi ni nani hamtaendeshwa na kima yeyote ila kwa sasa endeleeni kunyooshwa tu maana hamna msaada wowote kwa watz
Yaani nyie machawa mnatakiwa mfanyiziwe hadi akili ziwakae vizuri. Maana nyie watu wanapotaka mabadiliko mnapewa vijisent vya kununulia vijigari mnajitoa ufahamu na kukwamisha mabadiliko. Yaani hata kukiwa na mamlaka kumi za kuwadhibiti nyie machawa, ni sawa tu.Wanabodi
Hii ni makala yangu kwenye Gazeti la Nipashe Jumapili ya Leo
View attachment 3554648
Wanabodi, msituone Waandishi wa Habari na Watangazaji wa Tanzania, kama ni waoga waoga, na vyombo vya habari vya Tanzania kuwa ni media oga, kazi yake ni kusifia tuu na kufanya uchawa!.
No!, waandishi majasiri na wa kweli tupo, na vyombo vya habari vya kiukweli na vya kijasiri vipo, mfano mzuri wa mwandishi jasiri ni mwandishi mimi na mfano mzuri wa vyombo vya habari vya kijasiri ni JF, ila tunapitia wakati mgumu sana, tunateseka sana, ila basi tuu, hatulalamiki, tunakufa kizungu na tai shingoni, tukifanya kosa moja, tunashukiwa kama mwewe na sio tuu kupigwa rungu, lingekuwa moja, ni kosa moja, tunapigwa marungu mawili kwa kuhukumiwa na ma Pilato wawili tofauti, wenye mamlaka mbili tofauti, kwa kutumia sheria mbili tofauti, zilizoko chini ya mawaziri wawili tofauti, hivyo mtu kwa kosa moja, kuhukumiwa adhabu mbili tofauti na mamlaka mbili tofauti kwa kosa lile lile moja, jambo ambalo ni kinyume cha kanuni za natural justice!
Haya mambo yamekuwa yakitokea, tumekuwa tukishughulikiwa kikamilifu, na baada ya pale, huwa tunajinyamazia kuogopa kufungiwa jumla.
Mimi imenitokea mara nyingi,
Siku ya kuzinduliwa rasmi kwa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari, JAB, niliandika makala kwenye gazeti hili kuipongeza, na pia nikaitolea angalizo. Leo ni mwaka mmoja wa uwepo wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari, hivyo naandika makala nyingine kuipongeza kutimiza mwaka mmoja, ila sasa sio tuu kuipa angalizo, bali pia kuiomba isifanye uchawa kwa serikali na viongozi wa serikali kwa kutoa maonyo batili na maonyo vivuli, kwa waandishi wa habari, ambayo yako kinyume na Ibara ya 18 ya uhuru wa kutoa maoni, na wakati huo huo huo Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, ikipiga rungu kwa chombo cha habari, hivyo mwandishi wa habari na chombo cha habari, kuhukumiwa mara mbili, kwa kupigwa marungu mawili, na kuadhibiwa mara mbili, na vyombo viwili vya udhibiti, kupitia sheria mbili tofauti, zilizo chini ya mamlaka mbili tofauti, Bodi ya Ithbati iliyo chini ya Wizara ya Habari inayotumia sheria ya habari, na mamlaka ya Mawasiliano, TCRA, inayopiga rungu lale kupitia Sheria ya Utangazaji, hivyo kukiuka kanuni ya pili na natural justice, inayosema, no one should be condemned twice for the same offence!, yaani mtu asihukumiwe mara mbili kwa kosa lile lile!.
- Nikiwa Mtangazaji wa DTV kupitia kipindi cha Mada Moto, tulitangaza matokeo ya kweli ya uchaguzi wa Zanzibar 1995, kituo kilipigwa fine, kipindi kikafutwa, mimi nikafutwa kazi!
- Nikachukuliwa na Masai Studio (RIP Ally Oki) kuendesha kipindi cha Kiti Moto, yale yale yaliyomo yapo, kipindi kikafa kifo cha mende!
- Nikaibukia TVT, nikiendesha kipindi cha Ulingo wa Siasa, kilichotokea kwa vile huku ni serikalini unakula kiapo cha usiri, lakini yalinikuta ya kunikuta, nikapigwa summary dismissal kwa kosa la insubordination!, nikafungasha virago!
- Nikaanzisha kampuni yangu ya media, PPR Media, nikampiga mtu swali, PPR chali!
- Nikageukia magazeti, nikaandika kuhusu uchawa wa mhimili mmoja kumchawia Mkuu wa mhimili mwingine, nikaitwa Dodoma mbele ya kamati fulani, nilipotoka nilinywea na kuwa mdogo kama piriton!
- Nialikwa Jambo TV ile kutoa tuu maoni yangu fulani, Rungu la JAB likanishukia huku rungu la TCRA likiishukia Jambo TV! .
Hapa naomba kutoa pongezi kwa mamlaka zote mbili, JAB na TCRA, kutoa nafasi ya mtuhumiwa kupatiwa haki ya kusikilizwa kabla ya kuhukumiwa, kwa upande wa JAB ni unapigiwa tuu simu, bila barua yoyote ya wito, yenye tuhuma rasmi, na kutakiwa kufika ndani ya saa 24!, na baada ya kujieleza, unatolewa hukumu, ambayo wewe mtuhumiwa hupewi maandishi yoyote, bali unakuja kusoma tuu huku yako kwenye taarifa ya JAB kwa vyombo vya habari, hii mimi nimeiita hukumu kivuli. Ila kwa TCRA, angalau, wao walileta barua ya wito, yenye tuhuma specifi, ambayo imeletwa saa 5 asubuhi, na kutakiwa kufika mbele ya kamati ya maudhui saa 8 mchana, hivyo ndani ya saa 3, uwe na majibu ya maandishi!. Hivyo ndivyo sheria, taratibu na kanuni zinavyoelekeza?!.
Serikali ilipopitisha sheria hii ya habari ilikuwa na malengo mazuri tuu
· Kuweka utaratibu wa kisheria katika tasnia ya habari,
· Kuunda bodi ya ithibati ya wanahabari,
· Kuunda baraza huru la wanahabari,
· Kushughulikia masuala ya kashfa na
· Kushughulikia makosa yanayohusiana na utangazaji.
Kusimamia Ueledi na Uwajibikaji katika Tasnia ya Habari
Kupitia kifungu cha 26(1)(a) Sheria hii inalipa Baraza Huru la Wanahabari jukumu la kuandaa kanuni za nidhamu ya wanahabari na vyombo vya habari na kuzisimamia kanuni hizo. Kwa kulipa Baraza hili la wanahabari jukumu hili, ni dhahiri kwamba, Sheria hii imelenga mambo mawili makubwa. Moja ni kuwa wanahabari walinde nidhamu yao wao wenyewe (self regulation) na pili kuwalinda wananchi na jamii dhidi ya wanahabari wasiofuata maadili mema katika jamii.
Pia kanuni hizi ambazo zitatokana na mamlaka ya Baraza chini ya Sheria hii, zitakuwa na msukumo wa kisheria na hivyo wanahabari na vyombo vyote vya habari vitapaswa kuzifuata. Mpaka hapa ninapoandika leo, ikiwa ni miaka 10 tangu kutungwa kwa sheria hii, Baraza Huru la Habari, bado halijaundwa, hayo mambo ya JAB na TCRA kuita waandishi na kuvitia kibano vyombo vya habari kwa tuhuma za kukiuka maadili pale viongozi wanapokosolewa, vyombo hivi vimegeuka machawa wa viongozi, hakuna kiongozi aliyelalamika, bali JAB na TCRA vinawaita waandishi na chombo na kukitia kibano!. Maadam sasa JAB ipo, na waandishi tuliosajiliwa tupo, tuundeni Baraza letu huru la habari, tutungiane kanuni tuwajibishane, sio JAB, sio TCRA kutuingilia!.
Pamoja na JAB kufanya vizuri kwa kusajili wanahabari kadhaa, JAB bado ina mapungufu
Kwa mifungu cha 12(1) Waziri atateua wajumbe 7 kuwa wanabodi ya ithibati ya tasnia ya habari. Japo Bodi hii inauwakilishi wa wadau mbalimbali wengi wakitokea kwenye tasnia ya habari, wanabodi hao wote watateuliwa na Waziri. Ingekuwa vyema kama Sheria ingesema kuwa watu hao watachaguliwa na makundi wanayoyawakilisha. Kwa mfano, mwakilishi wa wahadhiri wa vyuo vya tasnia ya habari wangepaswa kuchaguliwa na wahadhiri wenyewe, vilevile, wawakilishi wa wanahabari pia wanapaswa kuchaguliwa na wanahabari wenyewe.
Mfumo huu wa kuchagua wawakilishi ndio bora zaidi na unaendana na demokrasia na utawala bora huku ukihakikisha kuwa maslahi ya kundi Fulani yanalindwa na hoja zao kufika bila kupindishwa. Mfumo wa wawakilishi kuteuliwa na wakilishwaji wenyewe umetumika kwenye sheria nyingi hapa nchini na hivyo ni vyema sheria hii ikarekebisha ili kuleta uwakilishi thabiti na kamili.
Ikumbukwe kuwa tasnia ya habari ni tasnia nyeti inayohitaji uhuru na ueledi wa hali ya juu hivyo uwakilishi wa moja kwamoja wa makundi yote ya tasnia hii kwenye bodi ya ithibati ni muhimu.
Sheria ya Huduma za Habari ya 2016 kwa mapana yake ni sheria nyeti na inayosimamia tasnia nyeti na inayopaswa kuwa huru japo imejitahidi kuweka mazingira bora zaidi kwa wanahabari ikiwemo
Kutambua uhuru wa habari,
Kuwatambua wanahabari kama wanataaluma kwa kuwaundia Bodi ya Ithibati na orodha ya wanataaluma hao,
Kwanini mpaka sasa Baraza la Huru la Wanahabari halijaundwa?!
Kwanini mpaka sasa mfuko wa mafunzo ya wanahabari haujaanzishwa?!
Kwanini mpaka sasa sharti kwa mmiliki wa chombo cha habari kuwakatia wanahabari bima ya kazi yao bado halijafanyika?!
Kwanini Waziri wa Habari kuteua wajumbe wa JAB badala ya kuacha waandishi tuchague wenyewe wawakilishi wetu
Hitimisho. Kitendo cha vyombo vya habari Tanzania kuwa chini ya wizara mbili, mawaziri wawili, sheria mbili na mamlaka mbili tofauti ni kaburi la uhuru wa habari Tanzania!, ili tuweze kuwa uhuru wa kweli wa habari, lazima tufike mahali, tuwe na wizara moja ya Mawasiliano, Habari na Utangazaji, chini ya sheria moja, waziri mmoja, mamlaka moja.
Mungu Ibariki Tanzania.
Paskali.
Taasisi yoyote ni watu wanaohusika, kuanzia zilizo na zisizo za kiserikali, za kitaifa hata binafsi.Wanabodi