DOKEZO Waandishi wa Habari na Media Tanzania, tunateseka sana! Kosa moja, hukumu mbili, kupitia Sheria mbili, Mamlaka mbili Tofauti!. Ni Haki? Tufanyeje?

DOKEZO Waandishi wa Habari na Media Tanzania, tunateseka sana! Kosa moja, hukumu mbili, kupitia Sheria mbili, Mamlaka mbili Tofauti!. Ni Haki? Tufanyeje?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
57,101
Reaction score
128,716
Wanabodi
Hii ni makala yangu kwenye Gazeti la Nipashe Jumapili ya Leo
Kosa Moja, Kesi Mbili, Adhabu Mbili, Sheria Mbili Tofauti, Chini ya Mamlaka Mbili .jpg

Wanabodi, msituone Waandishi wa Habari na Watangazaji wa Tanzania, kama ni waoga waoga, na vyombo vya habari vya Tanzania kuwa ni media oga, kazi yake ni kusifia tuu na kufanya uchawa!.

No!, waandishi majasiri na wa kweli tupo, na vyombo vya habari vya kiukweli na vya kijasiri vipo, mfano mzuri wa mwandishi jasiri ni mwandishi mimi na mfano mzuri wa vyombo vya habari vya kijasiri ni JF, ila tunapitia wakati mgumu sana, tunateseka sana, ila basi tuu, hatulalamiki, tunakufa kizungu na tai shingoni, tukifanya kosa moja, tunashukiwa kama mwewe na sio tuu kupigwa rungu, lingekuwa moja, ni kosa moja, tunapigwa marungu mawili kwa kuhukumiwa na ma Pilato wawili tofauti, wenye mamlaka mbili tofauti, kwa kutumia sheria mbili tofauti, zilizoko chini ya mawaziri wawili tofauti, hivyo mtu kwa kosa moja, kuhukumiwa adhabu mbili tofauti na mamlaka mbili tofauti kwa kosa lile lile moja, jambo ambalo ni kinyume cha kanuni za natural justice!

Haya mambo yamekuwa yakitokea, tumekuwa tukishughulikiwa kikamilifu, na baada ya pale, huwa tunajinyamazia kuogopa kufungiwa jumla.

Mimi imenitokea mara nyingi,
  1. Nikiwa Mtangazaji wa DTV kupitia kipindi cha Mada Moto, tulitangaza matokeo ya kweli ya uchaguzi wa Zanzibar 1995, kituo kilipigwa fine, kipindi kikafutwa, mimi nikafutwa kazi!
  2. Nikachukuliwa na Masai Studio (RIP Ally Oki) kuendesha kipindi cha Kiti Moto, yale yale yaliyomo yapo, kipindi kikafa kifo cha mende!
  3. Nikaibukia TVT, nikiendesha kipindi cha Ulingo wa Siasa, kilichotokea kwa vile huku ni serikalini unakula kiapo cha usiri, lakini yalinikuta ya kunikuta, nikapigwa summary dismissal kwa kosa la insubordination!, nikafungasha virago!
  4. Nikaanzisha kampuni yangu ya media, PPR Media, nikampiga mtu swali, PPR chali!
  5. Nikageukia magazeti, nikaandika kuhusu uchawa wa mhimili mmoja kumchawia Mkuu wa mhimili mwingine, nikaitwa Dodoma mbele ya kamati fulani, nilipotoka nilinywea na kuwa mdogo kama piriton!
  6. Nialikwa Jambo TV ile kutoa tuu maoni yangu fulani, Rungu la JAB likanishukia huku rungu la TCRA likiishukia Jambo TV! .
Siku ya kuzinduliwa rasmi kwa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari, JAB, niliandika makala 3 kuipongeza JAB, moja humu JF Pongezi Bodi ya Ithibati kwa Waandishi wa Habari kwa Mwanzo Mzuri, Cheti Kisitumike kama Fimbo Kuwachapia Wenye Vipaji, Uwezo na Uzoefu wasio na Cheti moja kwenye gazeti la Nipashe
1773081957200.png

na nyingine kwenye gazeti la Mwananchi https://www.mwananchi.co.tz/mw/kolamu/hongera-bodi-ya-ithibati-mwanzo-mzuri-ila--5136714
Pongezi Ithibati. .jpg

Kwenye ipongeza, zote hizo pia niliweka angalizo fulani, Leo ni mwaka mmoja wa uwepo wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari, hivyo naandika makala nyingine kuipongeza kutimiza mwaka mmoja, ila sasa sio tuu kuipa angalizo, bali lile angalizo limekuja kutokea kweli na mimi pia likanikumba!, hivyo naiomba JAB na TCRA, kama kuna mtu amekashifiwa, alalamike, JAB na TCRA, wasifanye uchawa kwa serikali na viongozi wa serikali kwa kutoa maonyo batili na maonyo vivuli, kwa waandishi wa habari ambao ni wachambuzi, maoni yao yanalindwa na ibara ya 18 ya katiba, hivyo adhabu zao na maonyo yao ni yako kinyume na Ibara ya 18 ya katiba ya uhuru wa kutoa maoni, na wakati huo huo huo Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, ikipiga rungu kwa chombo cha habari, hivyo mwandishi wa habari na chombo cha habari, kuhukumiwa mara mbili, kwa kupigwa marungu mawili, na kuadhibiwa mara mbili, na vyombo viwili vya udhibiti, kupitia sheria mbili tofauti, zilizo chini ya mamlaka mbili tofauti, Bodi ya Ithbati iliyo chini ya Wizara ya Habari inayotumia sheria ya habari, na mamlaka ya Mawasiliano, TCRA, inayopiga rungu lale kupitia Sheria ya Utangazaji, hivyo kukiuka kanuni ya pili na natural justice, inayosema, no one should be condemned twice for the same offence!, yaani mtu asihukumiwe mara mbili kwa kosa lile lile!.

Hapa naomba kutoa pongezi kwa mamlaka zote mbili, JAB na TCRA, kutoa nafasi ya mtuhumiwa kupatiwa haki ya kusikilizwa kabla ya kuhukumiwa, kwa upande wa JAB ni unapigiwa tuu simu, bila barua yoyote ya wito, yenye tuhuma rasmi, na kutakiwa kufika ndani ya saa 24!, na baada ya kujieleza, unatolewa hukumu, ambayo wewe mtuhumiwa hupewi maandishi yoyote, bali unakuja kusoma tuu huku yako kwenye taarifa ya JAB kwa vyombo vya habari, hii mimi nimeiita hukumu kivuli. Ila kwa TCRA, angalau, wao walileta barua ya wito, yenye tuhuma specifi, ambayo imeletwa saa 5 asubuhi, na kutakiwa kufika mbele ya kamati ya maudhui saa 8 mchana, hivyo ndani ya saa 3, uwe na majibu ya maandishi!. Hivyo ndivyo sheria, taratibu na kanuni zinavyoelekeza?!.

Serikali ilipopitisha sheria hii ya habari ilikuwa na malengo mazuri tuu

· Kuweka utaratibu wa kisheria katika tasnia ya habari,

· Kuunda bodi ya ithibati ya wanahabari,

· Kuunda baraza huru la wanahabari,

· Kushughulikia masuala ya kashfa na

· Kushughulikia makosa yanayohusiana na utangazaji.

Kusimamia Ueledi na Uwajibikaji katika Tasnia ya Habari
Kupitia kifungu cha 26(1)(a) Sheria hii inalipa Baraza Huru la Wanahabari jukumu la kuandaa kanuni za nidhamu ya wanahabari na vyombo vya habari na kuzisimamia kanuni hizo. Kwa kulipa Baraza hili la wanahabari jukumu hili, ni dhahiri kwamba, Sheria hii imelenga mambo mawili makubwa. Moja ni kuwa wanahabari walinde nidhamu yao wao wenyewe (self regulation) na pili kuwalinda wananchi na jamii dhidi ya wanahabari wasiofuata maadili mema katika jamii.

Pia kanuni hizi ambazo zitatokana na mamlaka ya Baraza chini ya Sheria hii, zitakuwa na msukumo wa kisheria na hivyo wanahabari na vyombo vyote vya habari vitapaswa kuzifuata. Mpaka hapa ninapoandika leo, ikiwa ni miaka 10 tangu kutungwa kwa sheria hii, Baraza Huru la Habari, bado halijaundwa, hayo mambo ya JAB na TCRA kuita waandishi na kuvitia kibano vyombo vya habari kwa tuhuma za kukiuka maadili pale viongozi wanapokosolewa, vyombo hivi vimegeuka machawa wa viongozi, hakuna kiongozi aliyelalamika, bali JAB na TCRA vinawaita waandishi na chombo na kukitia kibano!. Maadam sasa JAB ipo, na waandishi tuliosajiliwa tupo, tuundeni Baraza letu huru la habari, tutungiane kanuni tuwajibishane, sio JAB, sio TCRA kutuingilia!.

Pamoja na JAB kufanya vizuri kwa kusajili wanahabari kadhaa, JAB bado ina mapungufu

Kwa mifungu cha 12(1) Waziri atateua wajumbe 7 kuwa wanabodi ya ithibati ya tasnia ya habari. Japo Bodi hii inauwakilishi wa wadau mbalimbali wengi wakitokea kwenye tasnia ya habari, wanabodi hao wote watateuliwa na Waziri. Ingekuwa vyema kama Sheria ingesema kuwa watu hao watachaguliwa na makundi wanayoyawakilisha. Kwa mfano, mwakilishi wa wahadhiri wa vyuo vya tasnia ya habari wangepaswa kuchaguliwa na wahadhiri wenyewe, vilevile, wawakilishi wa wanahabari pia wanapaswa kuchaguliwa na wanahabari wenyewe.

Mfumo huu wa kuchagua wawakilishi ndio bora zaidi na unaendana na demokrasia na utawala bora huku ukihakikisha kuwa maslahi ya kundi Fulani yanalindwa na hoja zao kufika bila kupindishwa. Mfumo wa wawakilishi kuteuliwa na wakilishwaji wenyewe umetumika kwenye sheria nyingi hapa nchini na hivyo ni vyema sheria hii ikarekebisha ili kuleta uwakilishi thabiti na kamili.

Ikumbukwe kuwa tasnia ya habari ni tasnia nyeti inayohitaji uhuru na ueledi wa hali ya juu hivyo uwakilishi wa moja kwamoja wa makundi yote ya tasnia hii kwenye bodi ya ithibati ni muhimu.

Sheria ya Huduma za Habari ya 2016 kwa mapana yake ni sheria nyeti na inayosimamia tasnia nyeti na inayopaswa kuwa huru japo imejitahidi kuweka mazingira bora zaidi kwa wanahabari ikiwemo

Kutambua uhuru wa habari,

Kuwatambua wanahabari kama wanataaluma kwa kuwaundia Bodi ya Ithibati na orodha ya wanataaluma hao,

Kwanini mpaka sasa Baraza la Huru la Wanahabari halijaundwa?!

Kwanini mpaka sasa mfuko wa mafunzo ya wanahabari haujaanzishwa?!

Kwanini mpaka sasa sharti kwa mmiliki wa chombo cha habari kuwakatia wanahabari bima ya kazi yao bado halijafanyika?!

Kwanini Waziri wa Habari kuteua wajumbe wa JAB badala ya kuacha waandishi tuchague wenyewe wawakilishi wetu

Hitimisho. Kitendo cha vyombo vya habari Tanzania kuwa chini ya wizara mbili, mawaziri wawili, sheria mbili na mamlaka mbili tofauti ni kaburi la uhuru wa habari Tanzania!, ili tuweze kuwa uhuru wa kweli wa habari, lazima tufike mahali, tuwe na wizara moja ya Mawasiliano, Habari na Utangazaji, chini ya sheria moja, waziri mmoja, mamlaka moja.

Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali.
 
Tanzania ishakuwa Korea kaskazini. Hii siyo Nchi huru tena. Ni kama Bulgaria ya Seusescu.

Sheria nyingi za kukandamiza habari.

Lazima tuongee wanachopenda watawala na machawa wao mana wana Bunduki na magari ya kutekea watu.
 
Pasco, kisu kifike kwenye mfupa.

Moja: Waandishi wengi bongo hii ni Makasuku, machawa, waimba mapambio, wapambe nuksi, waoga "cowards", wenye elimu ya hapa na pale na wachumia tumbo.

Mbili; kwa uchawa na ukasuku wao, jamii inakosa kupashwa habari za kweli na za kufichua uovu wa jamii.

Tatu; hatuna investigative journalists bongo, wanaoweza kweli kufanya tafiti, kufichua uovu na jamii ikanufaika kwa behavioural change au kujisahihisha.

Nje ya mada: Pasco badirika acha kujipendekeza kwa watu wanaokuona kipengele kwao. Chagua heshima.
 
Wanabodi
Hii ni makala yangu kwenye Gazeti la Nipashe Jumapili ya Leo
View attachment 3554648
Wanabodi, msituone Waandishi wa Habari na Watangazaji wa Tanzania, kama ni waoga waoga, na vyombo vya habari vya Tanzania kuwa ni media oga, msituone hivi mkatubeza, kiukweli tunapitia wakati mgumu sana, tunateseka sana, ila basi tuu, hatulalamiki, tunakufa kizungu na tai shingoni, tukifanya kosa moja, tunashukiwa kama mwewe na sio kupigwa rungu, lingekuwa moja, ni kosa moja, tunapigwa marungu mawili kwa kuhukumiwa na ma Pilato wawili tofauti, wenye mamlaka mbili tofauti, kwa kutumia sheria mbili tofauti, zilizoko chini ya mawaziri wawili tofauti, hivyo mtu kuhumiwa adhabu mbili tofauti na mamlaka mbili tofauti kwa kosa lile lile moja, jambo ambalo ni kinyume cha kanuni za natural justice!

Haya mambo yamekuwa yakitokea, tumekuwa tukishughulikiwa kikamilifu, na baada ya pale, huwa tunajinyamazia kuogopa kufungiwa jumla.

Siku ya kuzinduliwa rasmi kwa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari, JAB, niliandika makala kwenye gazeti hili kuipongeza, na pia nikaitolea angalizo. Leo ni mwaka mmoja wa uwepo wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari, hivyo naandika makala nyingine kuipongeza kutimiza mwaka mmoja, ila sasa sio tuu kuipa angalizo, bali pia kuiomba isifanye uchawa kwa serikali na viongozi wa serikali kwa kutoa maonyo batili na maonyo vivuli, kwa waandishi wa habari, ambayo yako kinyume na Ibara ya 18 ya uhuru wa kutoa maoni, na wakati huo huo huo Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, ikipiga rungu kwa chombo cha habari, hivyo mwandishi wa habari na chombo cha habari, kuhukumiwa mara mbili, kwa kupigwa marungu mawili, na kuadhibiwa mara mbili, na vyombo viwili vya udhibiti, kupitia sheria mbili tofauti, zilizo chini ya mamlaka mbili tofauti, Bodi ya Ithbati iliyo chini ya Wizara ya Habari inayotumia sheria ya habari, na mamlaka ya Mawasiliano, TCRA, inayopiga rungu lale kupitia Sheria ya Utangazaji, hivyo kukiuka kanuni ya pili na natural justice, inayosema, no one should be condemned twice for the same offence!, yaani mtu asihukumiwe mara mbili kwa kosa lile lile!.

Hapa naomba kutoa pongezi kwa mamlaka zote mbili, JAB na TCRA, kutoa nafasi ya mtuhumiwa kupatiwa haki ya kusikilizwa kabla ya kuhukumiwa, kwa upande wa JAB ni unapigiwa tuu simu, bila barua yoyote ya wito, yenye tuhuma rasmi, na kutakiwa kufika ndani ya saa 24!, na baada ya kujieleza, unatolewa hukumu, ambayo wewe mtuhumiwa hupewi maandishi yoyote, bali unakuja kusoma tuu huku yako kwenye taarifa ya JAB kwa vyombo vya habari, hii mimi nimeiita hukumu kivuli. Ila kwa TCRA, angalau, wao walileta barua ya wito, yenye tuhuma specifi, ambayo imeletwa saa 5 asubuhi, na kutakiwa kufika mbele ya kamati ya maudhui saa 8 mchana, hivyo ndani ya saa 3, uwe na majibu ya maandishi!. Hivyo ndivyo sheria, taratibu na kanuni zinavyoelekeza?!.

Serikali ilipopitisha sheria hii ya habari ilikuwa na malengo mazuri tuu

· Kuweka utaratibu wa kisheria katika tasnia ya habari,

· Kuunda bodi ya ithibati ya wanahabari,

· Kuunda baraza huru la wanahabari,

· Kushughulikia masuala ya kashfa na

· Kushughulikia makosa yanayohusiana na utangazaji.

Kusimamia Ueledi na Uwajibikaji katika Tasnia ya Habari
Kupitia kifungu cha 26(1)(a) Sheria hii inalipa Baraza Huru la Wanahabari jukumu la kuandaa kanuni za nidhamu ya wanahabari na vyombo vya habari na kuzisimamia kanuni hizo. Kwa kulipa Baraza hili la wanahabari jukumu hili, ni dhahiri kwamba, Sheria hii imelenga mambo mawili makubwa. Moja ni kuwa wanahabari walinde nidhamu yao wao wenyewe (self regulation) na pili kuwalinda wananchi na jamii dhidi ya wanahabari wasiofuata maadili mema katika jamii.

Pia kanuni hizi ambazo zitatokana na mamlaka ya Baraza chini ya Sheria hii, zitakuwa na msukumo wa kisheria na hivyo wanahabari na vyombo vyote vya habari vitapaswa kuzifuata. Mpaka hapa ninapoandika leo, ikiwa ni miaka 10 tangu kutungwa kwa sheria hii, Baraza Huru la Habari, bado halijaundwa, hayo mambo ya JAB na TCRA kuita waandishi na kuvitia kibano vyombo vya habari kwa tuhuma za kukiuka maadili pale viongozi wanapokosolewa, vyombo hivi vimegeuka machawa wa viongozi, hakuna kiongozi aliyelalamika, bali JAB na TCRA vinawaita waandishi na chombo na kukitia kibano!. Maadam sasa JAB ipo, na waandishi tuliosajiliwa tupo, tuundeni Baraza letu huru la habari, tutungiane kanuni tuwajibishane, sio JAB, sio TCRA kutuingilia!.

Pamoja na JAB kufanya vizuri kwa kusajili wanahabari kadhaa, JAB bado ina mapungufu

Kwa mifungu cha 12(1) Waziri atateua wajumbe 7 kuwa wanabodi ya ithibati ya tasnia ya habari. Japo Bodi hii inauwakilishi wa wadau mbalimbali wengi wakitokea kwenye tasnia ya habari, wanabodi hao wote watateuliwa na Waziri. Ingekuwa vyema kama Sheria ingesema kuwa watu hao watachaguliwa na makundi wanayoyawakilisha. Kwa mfano, mwakilishi wa wahadhiri wa vyuo vya tasnia ya habari wangepaswa kuchaguliwa na wahadhiri wenyewe, vilevile, wawakilishi wa wanahabari pia wanapaswa kuchaguliwa na wanahabari wenyewe.

Mfumo huu wa kuchagua wawakilishi ndio bora zaidi na unaendana na demokrasia na utawala bora huku ukihakikisha kuwa maslahi ya kundi Fulani yanalindwa na hoja zao kufika bila kupindishwa. Mfumo wa wawakilishi kuteuliwa na wakilishwaji wenyewe umetumika kwenye sheria nyingi hapa nchini na hivyo ni vyema sheria hii ikarekebisha ili kuleta uwakilishi thabiti na kamili.

Ikumbukwe kuwa tasnia ya habari ni tasnia nyeti inayohitaji uhuru na ueledi wa hali ya juu hivyo uwakilishi wa moja kwamoja wa makundi yote ya tasnia hii kwenye bodi ya ithibati ni muhimu.

Sheria ya Huduma za Habari ya 2016 kwa mapana yake ni sheria nyeti na inayosimamia tasnia nyeti na inayopaswa kuwa huru japo imejitahidi kuweka mazingira bora zaidi kwa wanahabari ikiwemo

Kutambua uhuru wa habari,

Kuwatambua wanahabari kama wanataaluma kwa kuwaundia Bodi ya Ithibati na orodha ya wanataaluma hao,

Kwanini mpaka sasa Baraza la Huru la Wanahabari halijaundwa?!

Kwanini mpaka sasa mfuko wa mafunzo ya wanahabari haujaanzishwa?!

Kwanini mpaka sasa sharti kwa mmiliki wa chombo cha habari kuwakatia wanahabari bima ya kazi yao bado halijafanyika?!

Kwanini Waziri wa Habari kuteua wajumbe wa JAB badala ya kuacha waandishi tuchague wenyewe wawakilishi wetu

Hitimisho. Kitendo cha vyombo vya habari Tanzania kuwa chini ya wizara mbili, mawaziri wawili, sheria mbili na mamlaka mbili tofauti ni kaburi la uhuru wa habari Tanzania!, ili tuweze kuwa uhuru wa kweli wa habari, lazima tufike mahali, tuwe na wizara moja ya Mawasiliano, Habari na Utangazaji, chini ya sheria moja, waziri mmoja, mamlaka moja.

Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali.
P yaani ungeandika haya kabla ya kupewa kibano ungekuwa ume-win sana!
Sasa hivi unaonekana una doooooomo tu
 
Mwalimu Pascal Mayalla, shikamoo,

Professionalism katika kila kada ndio pekee njia ya uhakika na ya kistaarabu kuepuka vigingi au changamoto za kisheria na hayo unayoyaita marungu.

Siku hizi katika tasnia ya habari,
kukiuka sheria kwa makusudi na kwa kujua kabiasa kua ni kosa, hasa katika taaluma ya uandishi wa habari imekau kama desturi ya kucraete tension na kugain public sympathy ambayo kimsingi haisaidii chochote katika kubadili sheria, kuboresha au kukuza taaluma yenyewe bali inachochea ugumu zaidi wa kazi yenyewe na kujenga uhasama baina ya wanahabari na mamlaka za usimamizi wa sheria na masuala ya habari.

Ni muhimu sana kufanya kazi kwa weledi kama wanataaluma bila kusingizia sijui uchawa au unyumbu vitu ambavyo ni useless na havina athari yoyote katika jamii na tasnia yenyewe.
 
Pasco, kisu kifike kwenye mfupa.

Moja: Waandishi wengi bongo hii ni Makasuku, machawa, waimba mapambio, wapambe nuksi, waoga "cowards", wenye elimu ya hapa na pale na wachumia tumbo.

Mbili; kwa uchawa na ukasuku wao, jamii inakosa kupashwa habari za kweli na za kufichua uovu wa jamii.

Tatu; hatuna investigative journalists bongo, wanaoweza kweli kufanya tafiti, kufichua uovu na jamii ikanufaika kwa behavioural change au kujisahihisha.

Nje ya mada: Pasco badirika acha kujipendekeza kwa watu wanaokuona kipengele kwao. Chagua heshima.
Hayo yoote uliyoyaelekeza kwa waandishi wa habari yana akisi jamii nzima ya Kitanzania,
So nahisi chakubadilika ni jamii kwa ujumla mana waandishi wapo waliokuwa wamenyooka wakajikuta katika matatizo bila kupata msaada wowote kutoka katika jamii inayowazunguka,
Pole sana Pascal Mayalla,
 
Mwalimu Pascal Mayalla, shikamoo,
professionalism katika kila kada ndio pekee njia ya uhakika na ya kistaarabu kuepuka vigingi au changamoto za kisheria na hayo unayoyaita marungu.

Siku hizi katika tasnia ya habari,
kukiuka sheria kwa makusudi hasa katika taaluma ya uandishi wa habari imekau kama desturi ya kucraete tension na kugain public sympathy ambayo kimsingi haisaidii chochote katika kubadili sheria, kuboresha au kukuza taaluma yenyewe bali inachochea ugumu zaidi wa kazi yenyewe na kujenga uhasama baina ya wanahabari na mamlaka za usimamizi wa sheria na masuala ya habari.

ni muhimu sana kufanya kazi kwa weledi kama wanataaluma bila kusingizia sijui uchawa au unyumbu vitu ambavyo ni useless na havina athari yoyote katika jamii na tasnia yenyewe.
Kwahiyo weledi ni kusifia tu, bila hata kushauri, kukosoa au kutoa maoni?
Mbona wapo wanaosifia hata vitu vya uongo wa wazi lakini hakuna hatua zinazochukuliwa dhidi yao?
 
Pole sana kiongozi watanzania wazalendo wapo wengi tu shida iliyopo ni chama tawala hawataki reforms na sisi watawaliwa tuko kimya, jeshi liko kimya lisu yuko nyuma ya nondo.

Kwa maoni yangu kwa kile kilichotokea tr 29 mwaka jana hawa jamaa hawawezi kufanya reforms tusubiri labda kizazi cha wajukuu wetu wanaweza kushinikiza kupata Tanzania tuitakayo.

Pole sana wazelendo wa nchi hii kwa madhira mnayopitia
 
Hongera kwa ujasiri mkuu,

Hii nchi mambo ya Uhuru wa habari ni mpaka pale mifumo ya CCM itakapoondolewa, hawawezi kukubali kukosolewa sababu wanajua ni waovu.

Fikiria kitu kidogo kama kufunga comment kwenye mitandao ya serikali kuanzia raisi, Polisi nk unajiuliza wanaogopa nini kama ni serikali ya watu?
 
Hongera kwa kuwa na msimamo thabiti kwenye kazi yako bila uoga japo juzi ulikubali kosa huku ukinua hauna kosa! "Nililazimishwa kunywa maji"! Kisha na kuja mbele yetu kwa kujiamini eti nililazimishwa! Shame upon you Mr. Lawyer.

Nyie waandishi wa Tanzania niliwachukia na kuwaona kama mbwakoko (samahani) baada ya Kushindwa kulaani kuuawa Mwangosi huko Iringa, badala yake mkaonesha utiifu wenu kwa wauzaji pale Jangwani!

Kwa udhaifu wenu mlikiua chama chenu cha waandishi wa habari kilichoanzishwa wakati wa Mkapa(kama sijakosea) alipo kuwa katibu mkuu wizara ya Habari, mmegawanyika huku mkikodolea macho bahasha za khaki mnapokwenda kutimiza wajibu wenu.
 
Hivi Pascal Mayalla yule balile mlimchagua nyie kama kiongozi wenu kama mlichagua nyie basi kwenye kada yenu kuna machawa wengi.

Kada ya sheria wanajitahidi sana viongozi wao wanaowachagua waliowengi ni wapigania nchi tuitakayo
 
Back
Top Bottom