Chilipamwao
JF-Expert Member
- Nov 15, 2010
- 523
- 128
Majjid ni traitor! shame on you!
"I believe in equality for everyone, except reporters and photographers." – Mahatma GandhiNtaramuka,
Ungewasaidia basi wachangiaji wa mada uliyoianzisha kwa kuwaeleza sababu ama hoja za Mjengwablog za kuendelea kuandika habari za Kipolisi. Vinginevyo, ni aina hii ya maswali uliouliza bila kueleza kilichosemwa na Mjengwablog ndio hupelekea upotoshaji wa jambo zima na watu kuishia kumjadili mtoa hoja badala ya hoja iliyowasilishwa mezani. Natumaini hukufanya hivi kwa kukusudia.
Maggid
Waandishi mnaogoma kuandika habari zinazohusu jeshi la polisi mtameza matapishi yenu. Mngesema hivi" WAANDISHI KUGOMA KUANDIKA HABARI ZA IGP SAID MWEMA" ningewaelewa na ningewaunga mkono.
Kwa mfano kituo cha Chanel 10, radio Country, Ebony FM, nk vikipata matatizo ama ya kuibiwa au kuunguliwa moto taarifa zao watapeleka wapi? Waandishi wakumbuke Godwin alipopigwa na kijana mdogo Diamond Platnum pale uwanja wa Samora Iringa ni polisi ndio waliomsaidia, Mwandishi Maregesi Gilshon alipopata ajali ya gari ni polisi haohao waliomsaidia.
BUSARA ITUMIKE WAANDISHI MSIPEWE MANENO. AJALI IKITOKEA POLISI WATAFIKISHAJE TAARIFA KWA NDUGU WA MAJERUHI. HAO MAITI TAARIFA ZAKE TUTAZIPATAJE?USITUKANE UKUNGA NA UZAZI UNGALIPO.
Huwa sipendi hata kidogo kusoma habari zako. Umekuwa mtu wa kuandika vitu ambavyo mantiki inakataa.
Ni kweli binadamu tunatofautiana nami pia kwenye hili nakuunga mkono pamoja na kwamba muda mwingi na hasa kupitia makala zako Rai Mwema nimekuwa na mtazamo hasi. Naomba kwenye hili uweke msisitizo kuwa taarifa zitakazo fanyiwa kazi na wanahabari ziwe taarifa za kihalifu za kipolisi dhidi ya raia tu hadi hapo watakapo jirekebisha na jamii kuona wamerekebishika na wala sikwenda kupokea taarifa feki za kipolisi zinazotengenezwa maofisini. (tumeua li-jambazi na mengineyo..........)Mbali ya tukio la mauaji ya mwandishi mwenzetu Daud Mwangosi, hatuwezi kuacha kufanya kazi na polisi kupata majibu ya matukio mengine ya kihalifu yanayotokea katika jamii kwa vile tu tuna mgogoro na polisi.