Waandishi Kugomea Habari Za Kipolisi; Naomba Nichangie Haya...

maggid

JF-Expert Member
Dec 3, 2006
1,084
1,246
Ndugu zangu,

Ahsanteni kwa mitazamo yenu. Katika hili yawezekana tukawa na mitazamo tofauti, ni hali ya kibinadamu. Kwangu mimi, kwa wanahabari huu si wakati wa kutangaza mgomo wa kuripoti habari za kipolisi, kinyume chake, ni wakati wa kushambulia kwa pamoja kwa kuwakabili polisi na wahusika wengine kwa maswali yenye kuhitaji majibu.

Huu ni wakati wa jeshi la wanahabari kuishambualia polisi kama taasisi muhimu ya dola ili ipate majibu ya maswali ambayo jamii inataka majibu yake. Mbali ya tukio la mauaji ya mwandishi mwenzetu Daud Mwangosi, hatuwezi kuacha kufanya kazi na polisi kupata majibu ya matukio mengine ya kihalifu yanayotokea katika jamii kwa vile tu tuna mgogoro na polisi.

Naamini, tofauti na kugoma, kuna njia nyingine za kuishinikiza Serikali na hata taasisi ya polisi kuchukua hatua katika yanayotokea. Na moja ya njia hiyo ni kila linapotokea tukio, kwa wanahabari kwa uwingi wetu, ' kuvamia' ofisi za wenye kuhusika na kutoa majibu ya maswali ambayo jamii inataka majibu yake.

Msimamo wangu huu unaeleweka hata na baadhi ya viongozi wa juu wa Iringa Press Club ambao nina ushirikiano nao mzuri. Na jema katika hili ni kuwa, ushauri wangu wa namna ya kwenda mbele umepokelewa vema na Makamu Mwenyekiti ( Francis Godwin) na Katibu Mkuu wa IPC ( Frank Leonard) ambao kimsingi nimefanya mazungumzo nao na wanaufanyia kazi ushauri wangu.

Vinginevyo, naelewa hasira na jazba tuliyo nayo wanahabari wengi kutokana na kilichotokea. Hata hivyo, hata katika hali kama hii, tuwe na ujasiri wa kumeza vipande vya barafu. Tutangulize hekima na busara. Ndio, tutulie na kupanga mikakati ya pamoja itakayohakikisha jamii tunayoitumikia hainyimwi haki yake ya kimsingi ya kupata habari ikiwamo habari za kipolisi. Na hata katika hili, jamii ina mengi inayoyahoji kupitia wanahabari. Wenye kuhitajika kuhojiwa ndio hao tunaofikiria kuwagomea. Naam, tuna lazima ya kuwahoji wahusika. Ni kazi yetu.

Ndio, mikakati hiyo ituhakikishie wenye kuhusika na kutoa majibu ya unyama uliomtokea mwanahabari mwenzetu hawapati muda wa kupumua. Hii ni pamoja na sisi tulio mstari wa mbele kuhakikisha kila kukicha wahusika wanatukuta nje ya milango ya ofisi zao tukisubiri majibu ya maswali ambayo jamii inayauliza.

Kwamba matukio kama ya mauaji ya Daud Mwangosi kamwe yasiwe ni ' Upepo tu unaopita'- Kwa wanahabari kugomea kuwakabili polisi kwa maswali ni namna moja au nyingine ya kutengeneza mazingira ya kuruhusu ' Upepo upite'.

Kufanya hivyo ni kulisaliti jukumu letu la msingi- Kuitumikia Jamii ya Watanzania.

Maggid Mjengwa
Iringa
 
hii ni sahihi pia na naamini ndivyo wanafanya na kama ni kuripoti polisi ni kuripoti taarifa ambazo zinawaathri polisi.....keep it up waandishi...........
 
Mwenyekiti mtendaji wa mjengwablog ndugu Maggid Mjengwa amesema ataendelea kuandika habari zinazolihusu jeshi la polisi nchini licha ya wanahabari kuazimia kutoandika habari za jeshi hili ikiwa ni hatua ya kuonyesha kutoridhishwa kwao na tabia ya polisi kuua raia wasio na hatia na hususani tukio la juzi ambao mwanahabari mmoja, David Mwangosi, aliuawa na polisi. Je, uamuzi huu wa Mjengwa unatupa tafsi gani? Unafiki, usaliti, uhuru binafsi au nn?
 
Mwenyekiti mtendaji wa mjengwablog ndugu Maggid Mjengwa amesema ataendelea kuandika habari zinazolihusu jeshi la polisi nchini licha ya wanahabari kuazimia kutoandika habari za jeshi hili ikiwa ni hatua ya kuonyesha kutoridhishwa kwao na tabia ya polisi kuua raia wasio na hatia na hususani tukio la juzi ambao mwanahabari mmoja, David Mwangosi, aliuawa na polisi. Je, uamuzi huu wa Mjengwa unatupa tafsi gani? Unafiki, usaliti, uhuru binafsi au nn?

Ntaramuka,
Ungewasaidia basi wachangiaji wa mada uliyoianzisha kwa kuwaeleza sababu ama hoja za Mjengwablog za kuendelea kuandika habari za Kipolisi. Vinginevyo, ni aina hii ya maswali uliouliza bila kueleza kilichosemwa na Mjengwablog ndio hupelekea upotoshaji wa jambo zima na watu kuishia kumjadili mtoa hoja badala ya hoja iliyowasilishwa mezani. Natumaini hukufanya hivi kwa kukusudia.

Maggid
 
Hujui kama Mjengwa ni rafiki na kipenzi cha ZZK yule ambaye role model wake ni Zenawi Meles???
Sasa hapo usitegemee kitu, kumbuka jinsi mjengwa alipotaka kuchakachua kura za Lema ktk kinyang'anyiro cha kumpata mwanasiasa bora kijana wa mwaka kilichoendeshwa ktk mitandao.
 
kama ni kusaliti waandishi mlishausaliti uma siku nyingi,sio ninyi mlioenda ikulu tu pindi mwanahalisi lilipofungiwa tena mkiwa na maswali mliyotengenezewa tayari.ila sikulengi wewe usinielewe vibaya lakini.mwisho nawaombea waandishi wote wanafiki vifo vibaya ili siku moja wagundue kwamba unafiki ni mbaya waache waandishi wagome ila tu watuandikie aibu zote za polisi.unasema muwafate ili mkapokee bahasha.
 
Njaa zako hizo!

Hapa wanachotaka wenzako ni kugoma kutoa taarifa zo zote ambazo polisi wanataka au wangependa wananchi wazipate na si habari ambazo polisi wametenda na wanataka kupotosha ukweli!
 
Ntaramuka,
Ungewasaidia basi wachangiaji wa mada uliyoianzisha kwa kuwaeleza sababu ama hoja za Mjengwablog za kuendelea kuandika habari za Kipolisi. Vinginevyo, ni aina hii ya maswali uliouliza bila kueleza kilichosemwa na Mjengwablog ndio hupelekea upotoshaji wa jambo zima na watu kuishia kumjadili mtoa hoja badala ya hoja iliyowasilishwa mezani. Natumaini hukufanya hivi kwa kukusudia.

Maggid

Asante sana! Hoja kubwa anayosimamia ndugu Mjengwa ni kuwa 'HABARI ZA KIPOLISI ZINAIHUSU JAMII'!
 
Mshukuru Mungu tu alikusaidia ukaolewa na Mwanamke wa Kizungu otherwise ungeowa Mzaramo mwenzako sasa hivi ungekuwa ni mchawi tayari. sijawahi kuona mtu mnafki kumzidi Maggid Mjengwa.
Ili kuthibitisha kauli yangu ngoja nizame maktaba nitarudi hapa na vivid evidence.
 
Huwa sipendi hata kidogo kusoma habari zako. Umekuwa mtu wa kuandika vitu ambavyo mantiki inakataa.
 
Maggid msimamo wako nauunga mkono kwasababu kususia kuandika habari za polisi ni adhabu kwa raia wasio na hatia.
Mi nadhani busara ni kuandika zaidi polisi hasa pale wanapokosea ili wabadilike.

Kuwasusia kunaweza kuwapa nafasi ya kufanya madudu zaidi kwakuwa hakuna atakaye jua.
Pia umeonyesha ujasiri kwa kutafakari uamuzi wa wanahabari wenzako na kuwa na msimamo tofauti wa kufanya kile unachoamini ni sahihi. Watanzania wengi tmezoea kufuata mkumbo bila kutafakari.

Naomba hao wanaosusia polisi watuambie faida anazopata mtanzania wa kawaida kutokana na mgomo wao. Mi si mtaalam ila sidhani kama kuna kipengele katika maadili ya uandishi wa habari kinacho wafundisha kugoma.
 
maggid, habari nyingi polisi wanazaotaka kutoa this time ni propaganda uzushi na uongo, this time they have been caught with their pants down, waandishi wasiwape nafasi kuongea upuuzi wao, wangekuwa wanajali by now kamuhanda would be in police custody where he belongs.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom