Waandishi Kugomea Habari Za Kipolisi; Naomba Nichangie Haya...

maggid

Probably you are right with the resoning, but do you really expect soon report from the g'vmnt? same G'vment tht experienced push(by meetings, strike frm her citizens) EAC ex employees(retired), teachers,doctors, etc? would you have suggested the same way if we'd be talking abt you as in really dead(no offence)??
 
Last edited by a moderator:
Waandishi mnaogoma kuandika habari zinazohusu jeshi la polisi mtameza matapishi yenu. Mngesema hivi" WAANDISHI KUGOMA KUANDIKA HABARI ZA IGP SAID MWEMA" ningewaelewa na ningewaunga mkono.

Kwa mfano kituo cha Chanel 10, radio Country, Ebony FM, nk vikipata matatizo ama ya kuibiwa au kuunguliwa moto taarifa zao watapeleka wapi? Waandishi wakumbuke Godwin alipopigwa na kijana mdogo Diamond Platnum pale uwanja wa Samora Iringa ni polisi ndio waliomsaidia, Mwandishi Maregesi Gilshon alipopata ajali ya gari ni polisi haohao waliomsaidia.

BUSARA ITUMIKE WAANDISHI MSIPEWE MANENO. AJALI IKITOKEA POLISI WATAFIKISHAJE TAARIFA KWA NDUGU WA MAJERUHI. HAO MAITI TAARIFA ZAKE TUTAZIPATAJE?USITUKANE UKUNGA NA UZAZI UNGALIPO.
.. Napingana na dhana ya polisi "kuwasaidia" wananchi, lolote litakalofanywa na polisi ktk ajali au uhalifu linafanyika ili kutekeleza WAJIBU wao. Si kweli kwamba ni msaada!
 
Kumbuka, hayati Daudi Mwangosi aliuaua kwa kusadikiwa kutenda kosa la KUWATAHADHARISHA UONGOZI WA JUU CHADEMA juu Taifa juu ya mpango wa siri kwenda kuuwaua kwenye shughuli za kichama Mufindi masaa 48 toka siku husika.

Sehemu ya hizo taarifa hizo nyeti zilikua zikinyoosha kidole kwa mwanahabari mwenzake na Mwangosi kuwa ndiye aliyerejesha taarifa hizo masaa machache baada ya marehemu kuanzisha thread hapa JF ambayo pia ilitoa tahadhari hizo hizo za MPANGO WA POLISI IRINGA KWENDA MUFINDI KUUA.

Japo taarifa hizo hazijaelezea kwamba mwanahabari huyo mwenzake na Mwangosi ni nani hasa ila naamini muda utatubainishia kabisaa mtu huyo.

Ni sikitiko na ni muhimu tena Mzee Wasira akahojiwa kwa VITISHO alivyovitoa kwa viongozi wa CHADEMA masaa 72 kabla ya mauaji ya kinyama huko huko Mufindi.

Maggid atakuwa ameshiriki kwa namna moja ama nyingine "kutengeneza" kifo cha kinyama cha Shujaa Daud Mwangosi,
MAGGID wewe ni muuwaji, wito wangu nae ahojiwe, ushahidi unaonyesha umeshiriki. na damu ya Mwangosi itakufuata daima.
 
Maggid msimamo wako nauunga mkono kwasababu kususia kuandika habari za polisi ni adhabu kwa raia wasio na hatia.
Mi nadhani busara ni kuandika zaidi polisi hasa pale wanapokosea ili wabadilike.

Kuwasusia kunaweza kuwapa nafasi ya kufanya madudu zaidi kwakuwa hakuna atakaye jua.
Pia umeonyesha ujasiri kwa kutafakari uamuzi wa wanahabari wenzako na kuwa na msimamo tofauti wa kufanya kile unachoamini ni sahihi. Watanzania wengi tmezoea kufuata mkumbo bila kutafakari.

Naomba hao wanaosusia polisi watuambie faida anazopata mtanzania wa kawaida kutokana na mgomo wao. Mi si mtaalam ila sidhani kama kuna kipengele katika maadili ya uandishi wa habari kinacho wafundisha kugoma.
Hivi kuna mtanzania ana kuwa na hamu ya kuangalia/kusoma habari za police, yaani kova kila baada ya mwezi au miezi lazima atokeee kwenye TV na bunduki kubwa akidai wamekamata jambazi!

Msipotoke, polisi kimsingi siyo source ya information za matukio, ila wao mara nyingi hujulishwa juu ya matukio na kuyatolea taarifa. Mkitaka kupata taarifa za uharifu kwanini msiende kwenye source ya tukio lenyewe? mara nyingi polisi wanakuwaga hawana detail zozote mpaka uchunguzi ufanyike kwa kuwahoji watu walewale ambao nyie waandindishi mngeweza kuwahoji kupata details za tukio. Kwa mfano mtu anakutwa amekufa na kutupwa polini, halafu polisi wanapewa taarifa na wapita njia, nyie waandishi mnawafuata polisi wa nini wakati mnaweza kufanya uchunguzi maeneo ya tukio kupata detail zaidi?

Sioni sababu za msingi za kuwasaliti wenzenu katika hili la kukataa kutoa taarifa za polisi kwa ajili ya kushinikiza polisi waheshimu haki za waandishi na raia.
 
Je nani anakumbuka vifo vya waandishi hawa wawili yaani Stanley Katabaro (LOLIONDO GATE) na Ishu ya Adam Mwaibabile (Songea)
 
.. Napingana na dhana ya polisi "kuwasaidia" wananchi, lolote litakalofanywa na polisi ktk ajali au uhalifu linafanyika ili kutekeleza WAJIBU wao. Si kweli kwamba ni msaada!

Ndugu zangu,
Nahofia hata baadhi yetu humu tumetawaliwa zaidi na jazba na hasira ya kilichotokea. Inaeleweka, lakini tuna lazima pia ya ku-face reality. Huwa namtolea mfano mdogo wangu Francis Godwin, miaka kadhaa iliyopita aliwahi kuamrishwa na kamanda wa polisi wa mkoa atoke nje ya chumba cha mkutano kwa vile anamwandika vibaya magazetini. Francis akatamka; " Hiyo pia ni habari!".

Ukweli wengi mmeelezea fikra zenu kwa hisia, lakini kwangu hakuna hata mmoja wenu aliyejenga hoja ya kunishawishi kuamini kuwa kwa waandishi kugomea habari za polisi ni jambo sahihi, nasikitika kusema hilo na msimamo wangu unabaki pale pale, kuwa ni mkakati wa kimakosa. Tulipo sasa waandishi wanatakiwa wawa-engage polisi kuliko kabla. Kuna maswali mengi yenye kuhitaji majibu, na wenye nafasi ya kutupatia majibu hayo ni polisi, ndio maana siioni mantiki ya kuwagomea polisi kwa sasa. Maana mahitaji ya majibu ya maswali hayo si yetu tu waandishi, bali ni ya jamii pana.

Ona leo hapa Iringa, kunako saa tano tu asubuhi meza nyingi za magazeti zilishaishiwa na magazeti. Na magazeti mengi hii leo yameripoti habari za kipolisi. Hata yale magazeti ya udaku sasa hayajayafikia magazeti ya hard news kwenye kasi ya kuuza. Na magazeti ambayo yamedoda mezani ni yale ambayo hayana hata habari moja ya kipolisi kuhusiana na kilichomtokea Daud Mwangosi.

Hii ina maanisha, jamii kwa sasa ina kiu kali ya kuujua ukweli. Na wenye wajibu wa kuwa mstari wa mbele kwenye kuusaka ukweli ni sisi waandishi wa habari. Na nahofia ni kazi ngumu kwetu kuupata ukweli kwa kuamua kuwasusia wale ambao wanao ukweli, lakini wameuficha, Polisi.

Kwangu mimi huo ndio ukweli wa hali halisi na ninaoushuhudia kwenye field. Tuache sasa kuogelea kwenye beseni la mapovu. Tuna jeshi moja tu la Polisi. Ingelikuwa rahisi kususia habari za kampuni za bia au simu. Hasara ingewafika wahusika kwa haraka. Lakini sidhani kama polisi wa nchi hii wanapata hasara kubwa wasipowaona waandishi wakiwafuata kuwahoji na kutaka majibu ya maswali yanayoulizwa na jamii.

Let us face the reality.

Maggid
 
ajid, naamini uko sahihi kuwasusia hawa haisaidii lolote yenyewe inaendelea kupata mishahara na allowance zao nono nono, muhimu ni kupambana nao head on kwa kuandika bila kuchoka maovu yao yote wanayofanya naamini tunawajua vizuri hawa kwani ni ndugu, jamaa na marafiki zetu. Nadhani kwa kuwaweka wazi tutawaumiza zaidi ya kuwanunia
 
Nashangaa mnaomshambulia Mjengwa kiasi cha kumiuta mnafiki, msariti na majina mengine. Hivi kama waandishi wakigoma kuandika habari zote za Polisi ni kumkomoa nani?

Habari nyingi za Polisi ni negative zaidi kuliko positive. Polisi wetu wanasifika kwa mauaji ya raia wasio na hatia. Wanaua hadi watuhumiwa wakiwa katika vituo vya Polisi. Wanaongoza kwa kulalamikiwa kwa rushwa na madudu mengine kibao. Kuto yaanika wazi kwenye vyombo vya habari si unafuu zaidi kwao?

Mimi naona Polisi waandikwe zaidi si kwa mazuri yoyote baali kwa mabaya tu. Hapo ndipo kalamu itakapokuwa imewakomoa. Binafsi nafuatilia jinsi wanavyochakachua utoaji wa leseni za udereva kama njugu bila kufuata utaratibu huku wakiongozwa na rushwa katika maeneo mengi nchini. Mtandao huo ambao unachangia kwa kiasi kikubwa kuongezeka kwa ajali za barabarani unafahamika hadi kwa Maafisa waandamizi wa Jeshi hilo Makao Makuu.

Tunalia watu kupoteza maisha kutokana na ajali, kumbe wao wanachangia kwa 80%. Nitaweka wazi kila kitu ili umma ujue. Najua kutokana na uoza wa serikali yetu inayoongozwa kwa kulindana na ushemeji; hatua zinaweza zisichukuliwe.

Potelea mbali umma ukishajua utamlilia Mungu na naamini atasikia vilio hivyo. Ipo siku watanzania tutapumzika kutokana na unyama huu, tuombe uzima.
 
Ndugu Mjengwa, moja ya habari ulizoweka kwenye blog yako baada ya wenzio kutangaza kususia habari ya polisi ni ile inayohusu wiki ya nenda kwa usalama.

Hii habari, haina umuhimu sana kwa jamii kwa sababu stika zenyewe tunapewa bila hata ya gari kukaguliwa-hata ukienda na gari central. Kwahiyo, ni zoezi lisilo na mantiki kutokana na namna linavyoendeshwa, naamini hata wewe unalijua hilo maana una gari. Cha muhimu kwako, labda ilikuwa kuvutia matangazo kutoka TBL ambao ndio wadhamini wa wiki ya nenda kwa usalama, maana naona wenye blog mko kwenye mashindano ya kupata wadhamini. Mim nakubaliana na dhana yako kwa habari zenye maslahi kweli kwa wananchi kama uhalifu n.k. Naamin hata hao waliosusia polisi, likitokea jambo kubwa linalohusu uhalifu, wataandika na kushirikiana na polisi.

Kwa upande mwingine, nashawishika kuamini kwamba unataka ku-take advantage ya hali hii kwa maana kwamba kwanza polisi wa iringa watakukumbuka daima maana umewaunga mkono kipindi kigumu kwao. Pili, kwa sasa makampuni mengi yakitaka habari inayohusu ushirika wao na polisi iifikie jamii watakutumia wewe na hapo waweza kufaidi bahasha au mkataba wa matangazo. Sijasahau kwamba unadai huwa hupokei bahasha, lakin hata matangazo ni some kind of bahasha maana mpaka uandike habari za makapuni kwa wingi ndo unaweza ukapata matangazo.

Ndugu Mjengwa, hoja yako ina mushkeli kwasababu yametokea matukio makubwa kama la Mwangosi (Arusha, Ulimboka na Zona Moro), mbona kuandika kwenu hakujazuia yasiendelee kutokea? Kweli wewe Mjengwa unaweza ukamhoji Kamhanda hata kama hataki kuhojiwa, si atakukata kibao?

Hawa ma-RPC wanapenda sana PR ndio maana wako karibu na waandishi wa habari, usitegemee watakupa ushirikiano kama kuna mambo machafu ya kuwahusu. PR ndo iliyomtoa Kova Mbeya na kumpandisha cheo hadi dar. Ni PR tu.
 
Ndugu zangu,
Nahofia hata baadhi yetu humu tumetawaliwa zaidi na jazba na hasira ya kilichotokea. Inaeleweka, lakini tuna lazima pia ya ku-face reality. Huwa namtolea mfano mdogo wangu Francis Godwin, miaka kadhaa iliyopita aliwahi kuamrishwa na kamanda wa polisi wa mkoa atoke nje ya chumba cha mkutano kwa vile anamwandika vibaya magazetini. Francis akatamka; " Hiyo pia ni habari!".

Ukweli wengi mmeelezea fikra zenu kwa hisia, lakini kwangu hakuna hata mmoja wenu aliyejenga hoja ya kunishawishi kuamini kuwa kwa waandishi kugomea habari za polisi ni jambo sahihi, nasikitika kusema hilo na msimamo wangu unabaki pale pale, kuwa ni mkakati wa kimakosa. Tulipo sasa waandishi wanatakiwa wawa-engage polisi kuliko kabla. Kuna maswali mengi yenye kuhitaji majibu, na wenye nafasi ya kutupatia majibu hayo ni polisi, ndio maana siioni mantiki ya kuwagomea polisi kwa sasa. Maana mahitaji ya majibu ya maswali hayo si yetu tu waandishi, bali ni ya jamii pana.

Ona leo hapa Iringa, kunako saa tano tu asubuhi meza nyingi za magazeti zilishaishiwa na magazeti. Na magazeti mengi hii leo yameripoti habari za kipolisi. Hata yale magazeti ya udaku sasa hayajayafikia magazeti ya hard news kwenye kasi ya kuuza. Na magazeti ambayo yamedoda mezani ni yale ambayo hayana hata habari moja ya kipolisi kuhusiana na kilichomtokea Daud Mwangosi.

Hii ina maanisha, jamii kwa sasa ina kiu kali ya kuujua ukweli. Na wenye wajibu wa kuwa mstari wa mbele kwenye kuusaka ukweli ni sisi waandishi wa habari. Na nahofia ni kazi ngumu kwetu kuupata ukweli kwa kuamua kuwasusia wale ambao wanao ukweli, lakini wameuficha, Polisi.

Kwangu mimi huo ndio ukweli wa hali halisi na ninaoushuhudia kwenye field. Tuache ssa kuogelea kwenye beseni la mapovu. Tuna jeshi moja tu la Polisi. Ingelikuwa rahisi kususia habari za kampuni za bia au simu. Hasara ingewafika wahusika kwa haraka. Lakini sidhani kama polisi wa nchi hii wanapata hasara kubwa wasipowaona waandishi wakiwafuata kuwahoji na kutaka majibu ya maswali yanayoulizwa na jamii.

Let us face the reality.

Maggid

Niliijibu post yako ya mwanzo kwa kufikiri kuwa umekuja hapa JF ili kujadili na kama watu wanahoja basi ueleweshwe, kwa majibu uliyoyatoa kwenye hii post baada ya post nyingi zenye maswali mengi ambayo umeacha kuyajibu kwa makusudi, nashawishika kuwa umetumwa kuja hapa JF kuendeleza upotoshaji wako.

Maisha ni kuchagua, wewe umechagua kuishi kwa kutumia kalamu, hakuna wa kukupangia, nafikiri mimi binafsi nimekuelewa. Nasubiri matokeo ya kazi yako, hongera.

kwangu mimi, hii thread is considered closed.
 
Mjengwa,
Niseme tu kwamba sijawahi kusoma Makala zako wala kutembelea blogu yako, ziaid ya hii ya leo. Nimefedheheka na kusikitika sana.

Miaka kadhaa nyuma, akiwa kazini, aliyekuwa Mpiga picha Mkuu wa Makazeti ya The Citizen - Mpoki Bukuku, alipigwa na kuumizwa vibaya akiwa katika kutimiza majukumu yake kwenye kambi ya Magereza Ukonga. Kilichofuata hapo, ni media houses kwa umoja wao, kukataa kutoa habari zilizohusu Mambo ya Ndani (then akiwemo Mapuri). Protest hii ya media iliwapa fundisho serikali ambao walijikuta wanamuondoa Mapuri katika nyadhifa mbali mbali kichama na kiserikali. Leo hii hata hasikiki huko nje alipoenda.

Hivyo nimeshangazwa sana na msimamo wako. Je, wewe si Mwanachama wa IPC ? Haukuwepo kikaoni wakati azimio hilo linapita? Imekuwaj baadaye unaibukia mitandaoni na kusema ulilolisema? Kwa unataka kuwashawisi Godwin na mwenzake wafanye maamuzi nje ya vikao halali?

Mwisho wa ubaya siku zote huwa ni aibu; wewe endelea kuandika habari za polisi lakini wenzako hawaandiki. Kwisha.
 
ndiyo maana sasa utafutwe uandishi utakaolazimisha polisi kuelewa na kutokea publicly kama maharamia.ule kama wa mwanahalisi na usalama wa taifa juu ya ulimboka.fikiria kama leo kuna gazeti lingetoa majina na namba za polisi waliouwa,jamii ingefaidika kiasi gani.namuunga mkono maggid
 
“Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Iringa, walikwishatangaza katika tamko lao, kwamba wamesitisha ushirikiano wa kihabari na Jeshi la Polisi mkoani hapa, mpaka pale tume huru zilizoundwa kuchunguza kifo cha mwanahabari aliyeuawa zitakapotoa majibu yao,”

kumbe mpaka uchunguzi ukamilike sasa mbona huyu mjengwa hana subira,huu ni usaliti bila shaka
 
Mjengwa ni msaliti wa jamii na waandishi wa habari.Kama wao polisi na serikali wanajua umuhimu wa vyombo vya habari hawakutakiwa kuuwa mwandishi wa habari asiye na hatia tena akiwa kazini yaani katika kazi ya kuwapasha habari watanzania, Pia serikali ingeona umuhimu wa habari haikutakiwa kulifungia gazeti la mwanahalisi. Nawapongeza sana waaandishi wanaosusia kutangaza habari za polisi. Huyu Mje pengine analake jambo.
 
Kikombe

ULIVYO NA ROHO MBAYA NAONA HATA KUFUNGIWA
KWA MWANAHALISI ULIFANYA KARAMU.
 
watu kama mjengwa enzi zile tunasoma sekondari tulikuwa tunawaita pai au 22/7 au spy,yani wasalitiwasaliti tu,hujipendekeza kwa walimu,wao wa kwanza kufanya homework lakini majibu yakija ana namba ya kiatu,.chunguzeni historia yake tokea shule ya msingi utaniambia...
 
Na ukumbuke maggid and i mean it, kuwa makini sana na gari yako unayosafiri nayo hasa pale utakapopata pancha. sasa hivi ni muda wa kufundishana uzalendo kwa vitendo then hii tabia ya kununuliwa kama karanga ndio itakwisha.
This is a warning.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom