Jacobus
JF-Expert Member
- Mar 29, 2011
- 4,708
- 1,734
Vyombo vya habari vina nguvu zaidi ya kusambaza USHAWISHI kwa wasikilizaji/wasomaji wake na kuaminiwa. Wananchi wengi hapa nchini wanapenda mno soka na hasa soka la vilabu vyetu lakini waandishi/wachambuzi wa habari za michezo wamejikita mno na habari za bara la Ulaya hasahasa England, habari zinazohusu soka letu zinasemwa kijujuu tu lakini za England zitasemwa kwa hisia kali, habari za soka za CAF ndo hakuna kabisa kana kwamba Africa hakuna mashindano ya vilabu na mataifa! Jambo la ajabu ukisikiliza vyombo vya habari vya England huwezi sikia habari za soka zinazohusu vilabu vyetu. Mara kwa mara tumetoa wito kwa waandishi wetu wa habari za michezo kutoa kipaumbele kwa habari za NYUMBANI, AFRICA na mwisho nje ya bara letu, ni kipi kinachowafanya washindwa kufanya hivo?????????????????