Daata
JF-Expert Member
- Dec 24, 2012
- 4,762
- 2,069
Wakuu haki na amani iwe kwenu.
Kwa kipindi kirefu sasa kumekuwa na lawama kwa waandishi wa habari wa Tanzania baada watu kuona kuwa wanaripoti habari zenye mwelekeo moja wa kuitetea serikali na kunyamazia habari zote zinazokosoa au zenye tafsiri hasi kwa serikali.
Habari za kiuchunguzi dhidi ya matendo ya watendaji wa serikali zinakwepwa kwa kila namna lakini zenye kuipamba serikali zitaandikwa kwa wino mnene.
Sababu ni moja kuwa wahariri wa vyombo vyetu vya habari wameshasoma mwelekeo wa serikali, hivyo ili kuwa salama na kuendelea kuwepo inabidi kufuata kile serikali kinataka.
Wanaelewa kuwa wakijaribu kuandika habari zinakosoa serikali watakutana na TCRA kukisimamisha chombo hicho kwa miezi kadhaa au hata kukifutia usajili bila kukisikiliza .
Nimeona maoni ya watanzania kuwa wanatamani mwandishi wa CNN Larry Madowo aje Tanzania halafu wabadiliashane na wa Tanzania kadhaa.
Ukweli ni kwamba haitafanya kazi kwa sababu akija Tanzania atakutana na serikali ambayo habari kama hizo hazitakiwi na mwishowe ataufyata na kuwa kama waandishi wetu waliounga juhudi.
Nawasilisha.