Waandamanaji wa Mtwara ni hawa hapa

Waandamanaji wa Mtwara ni hawa hapa

tata mura

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2012
Posts
275
Reaction score
49
Ngugu zangu kumekuwepo na danganya toto nyingi, kuhusu kuwatuhumu na kuwalaumu wananchi wa Mtwara huku tunaficha ukweli wa mambo. Kabla ya maandamano ya mwaka jana Mtwara kutokea, baadhi ya Vyama vya Siasa vilisikika kwenye vyombo vya habari vikihamasisha wafuasi wao walioko Mtwara na kwingineko Nchini, kuandamana na kujiaandaa kuunda Chama cha Muungano na walienda mbali zaidi na kufikilia kutafuta aina ya bendera yao na Nembo itakayotumika.

Leo hii tumesahaulishwa na kuanza kuwatupia mzigo mzito wanamtwara bila kujua madhara yake. Naomba nivitaje Vyama vilivyoratibu maandamano ya mwaka jana Mtwara kama ifuatavyo; NCCR - Mageuzi, CHADEMA, SAU, TLP, APPT - Maendeleo, ADC pamoja na DP. Leo hii vyama husika tena vimeanza kugawanyika, mfano juzi tu Mwenyekiti wa Taifa wa NCCR- Mageuzi alibadilikiwa alipotembelea Mtwara na kutoeleweka, huku wao ndo walioanzisha Parade.

Mimi siamini kama wanamtwara ndo waliandaa maandamano yale huku awali vyama vyote tajwa vilisikika vikiandaa maandamano yale. Kwa wasiojua mambo ya ajira Mtwara, kutoka kwa wawekezaji ni hivi kwa nafasi za kawaida; Kama unaajiri wafanyakazi kwa fani ambazo Wanamtwara wanaziweza lazima uajiri Mtwara au kama utaona sivyo unaleta waajiriwa wapya kutoka mikoani idadi sawa unayotarajia kuajiri Mtwara kisha unawachukuwa wengine kutoka Mtwara(Wazawa) na kuwapeleka Mikoani unakotaka wewe.

Kwa maana nyepesi wanabadilishana kwa idadi sawa. Huu mfumo umekuwepo muda mrefu hapa Mtwara, ni kweli kila mtu hupenda kuvutia kwake lakini si kama ilivyochukuliwa na vyama vya kisiasa hadi kuja na watu kutoka Mikoani kwaajili ya kuongeza idadi. Kiongozi wa kwanza kutuhamasisha hapa Mtwara kuhoji mambo ya gesi alikuwa Zitto ngawaje siku hizi amejiweka pembeni kidogo, tuanamsikia kwenye mitandao tu najua ni mambo ya kisiasa.

Kwa yule atakae bisha atueleze ni lini tulihamasishana kuhusu maandamano tofauti na vyama?. Ukibisha sana ntantumia ishale; Ukikaa ishale, ukichimama nchale, ukilala nchale, ukimung'unya nchale, ukikimbia nchale na ukichuchumaa nchale. Ntwara tunaipenda serikali ije tuongee tumalize tofauti zilizopandwa na vyama vya kisiasa, chacha chichi ntaka ntule wapi?
 
Kwahiyo unataka kusemaje sasa? ivi unapinga nini na unakubali nini? acha sarakasi...
 
Kwahiyo unataka kusemaje sasa? ivi unapinga nini na unakubali nini? acha sarakasi...
Ukitulia utamuelewa, Mi nimeshangazwa na jinsi CCCUFM walivyojipenyeza na kudaka hoja ya gesi na sasa wanaimiliki. Hiyo vyama alivyovitaja mdau sasa havisikiki tena. Finally, lengo hatitafanikiwa kama misingi ya madai haitabaki imara.
 
Gesi kwanza, vyama Baadae!!!
 
sijakuelew
a.! Unamaanisha Tuvilaumu vyama vya siasa kwa kuwaamusha wanamtwara kudai haki yao au.?
 
Miguu juu kichwa chini hueleweki kajipange uje tena...
 
sijakuelew
a.! Unamaanisha Tuvilaumu vyama vya siasa kwa kuwaamusha wanamtwara kudai haki yao au.?

Namaanisha muungano wa vyama vya kisiasa umeishia wapi na kuwatupia mzigo Wananchi wasiokuwa na ufahamu wa gesi?. Waendelee kutujuza je kama tutashinda kupambana na serikali, plan 'b' ni ipi na je wakisusa kwa wanaofanya kazi ajira zetu zitakuwaje kwa maisha magumu haya?.
 
Wachambuzi wa mambo mmekuwa wengi,sasa jitokezeni mstari wa mbele na muache kubwabwaja!
 
Ngugu zangu kumekuwepo na danganya toto nyingi, kuhusu kuwatuhumu na kuwalaumu wananchi wa Mtwara huku tunaficha ukweli wa mambo. Kabla ya maandamano ya mwaka jana Mtwara kutokea, baadhi ya Vyama vya Siasa vilisikika kwenye vyombo vya habari vikihamasisha wafuasi wao walioko Mtwara na kwingineko Nchini, kuandamana na kujiaandaa kuunda Chama cha Muungano na walienda mbali zaidi na kufikilia kutafuta aina ya bendera yao na Nembo itakayotumika. Leo hii tumesahaulishwa na kuanza kuwatupia mzigo mzito wanamtwara bila kujua madhara yake. Naomba nivitaje Vyama vilivyoratibu maandamano ya mwaka jana Mtwara kama ifuatavyo; NCCR - Mageuzi, CHADEMA, SAU, TLP, APPT - Maendeleo, ADC pamoja na DP. Leo hii vyama husika tena vimeanza kugawanyika, mfano juzi tu Mwenyekiti wa Taifa wa NCCR- Mageuzi alibadilikiwa alipotembelea Mtwara na kutoeleweka, huku wao ndo walioanzisha Parade. Mimi siamini kama wanamtwara ndo waliandaa maandamano yale huku awali vyama vyote tajwa vilisikika vikiandaa maandamano yale. Kwa wasiojua mambo ya ajira Mtwara, kutoka kwa wawekezaji ni hivi kwa nafasi za kawaida; Kama unaajiri wafanyakazi kwa fani ambazo Wanamtwara wanaziweza lazima uajiri Mtwara au kama utaona sivyo unaleta waajiriwa wapya kutoka mikoani idadi sawa unayotarajia kuajiri Mtwara kisha unawachukuwa wengine kutoka Mtwara(Wazawa) na kuwapeleka Mikoani unakotaka wewe. Kwa maana nyepesi wanabadilishana kwa idadi sawa. Huu mfumo umekuwepo muda mrefu hapa Mtwara, ni kweli kila mtu hupenda kuvutia kwake lakini si kama ilivyochukuliwa na vyama vya kisiasa hadi kuja na watu kutoka Mikoani kwaajili ya kuongeza idadi. Kiongozi wa kwanza kutuhamasisha hapa Mtwara kuhoji mambo ya gesi alikuwa Zitto ngawaje siku hizi amejiweka pembeni kidogo, tuanamsikia kwenye mitandao tu najua ni mambo ya kisiasa. Kwa yule atakae bisha atueleze ni lini tulihamasishana kuhusu maandamano tofauti na vyama?. Ukibisha sana ntantumia ishale; Ukikaa ishale, ukichimama nchale, ukilala nchale, ukimung'unya nchale, ukikimbia nchale na ukichuchumaa nchale. Ntwara tunaipenda serikali ije tuongee tumalize tofauti zilizopandwa na vyama vya kisiasa, chacha chichi ntaka ntule wapi?

MCHEMSHO WA KUKU WA KIZUNGU HAUNA THAMANI TENA: Yaani wewe akili zako ndo zimefika mwisho wa kufikiri?,Haijalishi iwe wamechochewa au wamejichochea suala ni WAMESHITUKIA ufisadi wa ''chamasumu''CCM Wa-ambieni tangu 1998 Mlichota gesi pale songo songo na mka ahidi mgao wa umeme kuwa historia lakini ''mpaka sasa mgao upo'',sasa mtuambie watu wa songo songo wamefaidika na nini kwa mpango ule?,mbali na kuvunwa na kuchotwa kwa MADINI nchi nzima.Ni dhahiri kuwa historia hii mmepanga ku-irudisha kwa wana MTWARA nao wameshtuka.vyama vimetumika kama ving'amuzi tu matangazo(mada ni POWER PLANT ijengwe MTWARA na si gesi kuhamishiwa DAR).jadili hoja si king'amuzi kimeleta uchochezi.
 
Ngugu zangu kumekuwepo na danganya toto nyingi, kuhusu kuwatuhumu na kuwalaumu wananchi wa Mtwara huku tunaficha ukweli wa mambo. Kabla ya maandamano ya mwaka jana Mtwara kutokea, baadhi ya Vyama vya Siasa vilisikika kwenye vyombo vya habari vikihamasisha wafuasi wao walioko Mtwara na kwingineko Nchini, kuandamana na kujiaandaa kuunda Chama cha Muungano na walienda mbali zaidi na kufikilia kutafuta aina ya bendera yao na Nembo itakayotumika.

Leo hii tumesahaulishwa na kuanza kuwatupia mzigo mzito wanamtwara bila kujua madhara yake. Naomba nivitaje Vyama vilivyoratibu maandamano ya mwaka jana Mtwara kama ifuatavyo; NCCR - Mageuzi, CHADEMA, SAU, TLP, APPT - Maendeleo, ADC pamoja na DP. Leo hii vyama husika tena vimeanza kugawanyika, mfano juzi tu Mwenyekiti wa Taifa wa NCCR- Mageuzi alibadilikiwa alipotembelea Mtwara na kutoeleweka, huku wao ndo walioanzisha Parade.

Mimi siamini kama wanamtwara ndo waliandaa maandamano yale huku awali vyama vyote tajwa vilisikika vikiandaa maandamano yale. Kwa wasiojua mambo ya ajira Mtwara, kutoka kwa wawekezaji ni hivi kwa nafasi za kawaida; Kama unaajiri wafanyakazi kwa fani ambazo Wanamtwara wanaziweza lazima uajiri Mtwara au kama utaona sivyo unaleta waajiriwa wapya kutoka mikoani idadi sawa unayotarajia kuajiri Mtwara kisha unawachukuwa wengine kutoka Mtwara(Wazawa) na kuwapeleka Mikoani unakotaka wewe.

Kwa maana nyepesi wanabadilishana kwa idadi sawa. Huu mfumo umekuwepo muda mrefu hapa Mtwara, ni kweli kila mtu hupenda kuvutia kwake lakini si kama ilivyochukuliwa na vyama vya kisiasa hadi kuja na watu kutoka Mikoani kwaajili ya kuongeza idadi. Kiongozi wa kwanza kutuhamasisha hapa Mtwara kuhoji mambo ya gesi alikuwa Zitto ngawaje siku hizi amejiweka pembeni kidogo, tuanamsikia kwenye mitandao tu najua ni mambo ya kisiasa.

Kwa yule atakae bisha atueleze ni lini tulihamasishana kuhusu maandamano tofauti na vyama?. Ukibisha sana ntantumia ishale; Ukikaa ishale, ukichimama nchale, ukilala nchale, ukimung'unya nchale, ukikimbia nchale na ukichuchumaa nchale. Ntwara tunaipenda serikali ije tuongee tumalize tofauti zilizopandwa na vyama vya kisiasa, chacha chichi ntaka ntule wapi?
Kwa hivyo vyama ulivyovitaja havina wanachama huko Mtwara? Havina uwezo wa kuwahamasisha hao wanachama wake wa Mtwara kuandamana?
 
Namaanisha muungano wa vyama vya kisiasa umeishia wapi na kuwatupia mzigo Wananchi wasiokuwa na ufahamu wa gesi?. Waendelee kutujuza je kama tutashinda kupambana na serikali, plan 'b' ni ipi na je wakisusa kwa wanaofanya kazi ajira zetu zitakuwaje kwa maisha magumu haya?.

Haya Maisha magumu yameletwa na CCM mbali na DHAIFU kutamba na ahadi yake ya maisha bora kwa kila mTANZANIA/MFANYAKAZI mpaka saa hakuna ubora wowote wala ahueni,Wana mtwara wamesema GESI KWANZA VYAMA BAADAE, wewe hapa unaleta mada ya vyama,eeeeh kama ungechaguliwa kuwa msuluhishi wewe nadhani wange ku-MBATIA maana hujui na hujaelewa wana MTWARA wanachotaka nini.
HITIMISHO: hau-itaji kuwa na elimu hata ya msingi kujua kuwa wewe ndo huelewi gesi ni nini?,wana MTWARA wanataka nini?,na umuhimu wa wanacho kidai wana KUSINI kuwa ni faida kwa kusini pamoja na TAIFA kwa ujumla.hivyo kijana acha kutumikishwa na mafusadi watakupeleka pabaya.
 
Wala usianze kudanganya watu kwa ujumla wana Mtwara wote, hata tuliopo nje ya Mtwara tunawaunga mkono kwa sana tu, wanasiasa wanatumia tu kama platform ya wao kujijenga pia, .. Kupinga gesi ghafi kwenda Dsm hakuna siasa hapo . Kama umesoma vizuri tamko la Mkapa nae anapinga huu mpango wa serikali kwa maana haukushirikisha watu, ...hamasa ipo hadi vijijini ni mwanasiasa gani kaenda kuhamasisha huko?, ni umasikini wa wanannchi ndio unaleta hamasa
 
Na pia mkataba mbovu wa ujenzi wa hilo bomba la gesi ulisainiwa na hivyo vyama vilivyotajwa.
 
Hakuna mashindano ya kumtafuta Mhamasishaji Mkuu wa maandamano, muhimu watu tumehamasika na tumeungana kutetea Gesi kwa kauli moja, Gesi kwanza Vyama baadae!

safi sana KILAZA hajajua kama MTWARA GESI KWANZA VYAMA /DINI BAADAE.yeye kaibuka na vyama akakojoe alale kwa leo labda kesho ajipange upya.
 
Nyie anzeni tutasogeza vifaa hapo sijui kama mtakaa!! Waiteni uamsho na Alshabab kama ALGERIA !!! mapema hii unachanganyikiwa
 
......wewe nawe sijui umetoka wapi? Hivi ulisikia kauli za akina Malecela, mwenyekiti wa CCM Mtwara na yule mbunge wa Mtwara(kwa tiketi ya CCM)? Unataka kutuaminisha kuwa hao nao wamo kwenye hivyo vyama ulivyoviaja?. Acha upotoshaji wewe!!. GESI KWANZA, VYAMA BAADAE!!!!!!
 
Ndugu yangu kwanza we uko wapi? ivi ukosawa kweri? ivi hautambui kama rais mkapa ndie aliye kasaini mktaba wa uchimbaji wa gesi huku Mtwara/ na mpaka anatoka alituhakikishia kama kila kitu kitafanyika Mtwara mazo yatokanayo na gesi yatasafirishwa kwenda kwengine!!! na kikwete mwenyewe kwenye kampeni zake 2010 ulimsikia? unaongea nini ndugu yangu? au nawe ni mmoja wa mafisadi nini?
 
Back
Top Bottom