Ngugu zangu kumekuwepo na danganya toto nyingi, kuhusu kuwatuhumu na kuwalaumu wananchi wa Mtwara huku tunaficha ukweli wa mambo. Kabla ya maandamano ya mwaka jana Mtwara kutokea, baadhi ya Vyama vya Siasa vilisikika kwenye vyombo vya habari vikihamasisha wafuasi wao walioko Mtwara na kwingineko Nchini, kuandamana na kujiaandaa kuunda Chama cha Muungano na walienda mbali zaidi na kufikilia kutafuta aina ya bendera yao na Nembo itakayotumika.
Leo hii tumesahaulishwa na kuanza kuwatupia mzigo mzito wanamtwara bila kujua madhara yake. Naomba nivitaje Vyama vilivyoratibu maandamano ya mwaka jana Mtwara kama ifuatavyo; NCCR - Mageuzi, CHADEMA, SAU, TLP, APPT - Maendeleo, ADC pamoja na DP. Leo hii vyama husika tena vimeanza kugawanyika, mfano juzi tu Mwenyekiti wa Taifa wa NCCR- Mageuzi alibadilikiwa alipotembelea Mtwara na kutoeleweka, huku wao ndo walioanzisha Parade.
Mimi siamini kama wanamtwara ndo waliandaa maandamano yale huku awali vyama vyote tajwa vilisikika vikiandaa maandamano yale. Kwa wasiojua mambo ya ajira Mtwara, kutoka kwa wawekezaji ni hivi kwa nafasi za kawaida; Kama unaajiri wafanyakazi kwa fani ambazo Wanamtwara wanaziweza lazima uajiri Mtwara au kama utaona sivyo unaleta waajiriwa wapya kutoka mikoani idadi sawa unayotarajia kuajiri Mtwara kisha unawachukuwa wengine kutoka Mtwara(Wazawa) na kuwapeleka Mikoani unakotaka wewe.
Kwa maana nyepesi wanabadilishana kwa idadi sawa. Huu mfumo umekuwepo muda mrefu hapa Mtwara, ni kweli kila mtu hupenda kuvutia kwake lakini si kama ilivyochukuliwa na vyama vya kisiasa hadi kuja na watu kutoka Mikoani kwaajili ya kuongeza idadi. Kiongozi wa kwanza kutuhamasisha hapa Mtwara kuhoji mambo ya gesi alikuwa Zitto ngawaje siku hizi amejiweka pembeni kidogo, tuanamsikia kwenye mitandao tu najua ni mambo ya kisiasa.
Kwa yule atakae bisha atueleze ni lini tulihamasishana kuhusu maandamano tofauti na vyama?. Ukibisha sana ntantumia ishale; Ukikaa ishale, ukichimama nchale, ukilala nchale, ukimung'unya nchale, ukikimbia nchale na ukichuchumaa nchale. Ntwara tunaipenda serikali ije tuongee tumalize tofauti zilizopandwa na vyama vya kisiasa, chacha chichi ntaka ntule wapi?