Waalimu wote wachapwe viboko !

Waalimu wote wachapwe viboko !

Regnatus Cletus

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2018
Posts
1,114
Reaction score
959
Waalimu ni waamini wazuri sana wa adhabu ya viboko! Wanapenda sana matumizi ya fimbo wakiamini ni nyenzo ya kufundisha.

Imani hii ya viboko imewafanya waone kwamba bila fimbo maisha yao yatakosa raha. Kimsingi wanapenda sana kuchapa, tena kuchapa mpaka mwanafunzi atoke uhai basi roho zao zinasuuzika sana.

Waraka wa elimu pamoja na sheria ya elimu na kanuni ya elimu, inaelekeza kwamba, adhabu ya viboko visivyozidi vinne inapaswa kutolewa na mwalimu mkuu husika wa shule kwa kuzingatia umri, jinsia na afya ya mwanafunzi.

Baada ya adhabu, mwalimu mkuu atahakikisha anarekodi jina la mwanafunzi husika, sababu ya kutoa adhabu, na jina husika la mwalimu.

Utaratibu huu umelenga kuepusha ukatili mashuleni, mauaji ya wanafunzi, na adhabu zilizozidi kipimo, mathalani mauaji ya Sperius Eradius huko bukoba. Kwa kuzingatia hilo, utaratibu wa utoaji wa adhabu ya viboko umetengenezewa mfumo stahiki.Lakini walimu wote wanalia. Wanataka kuchapa, tena kuchapa bila utaratibu.

Nashauri walimu wote watakaokiuka utaratibu huu wa utoaji adhabu, baada ya kuchukuliwa hatua za kinidhamu kama kufukuzwa kazi na kusimamishwa, wapewe adhabu kali ya viboko.
 
Mkuu umetembelea walimu wote nchini Tanzania ukawakuta wanalia kuchapa viboko?
 
Waalimu ni waamini wazuri sana wa adhabu ya viboko! Wanapenda sana matumizi ya fimbo wakiamini ni nyenzo ya kufundisha.

Imani hii ya viboko imewafanya waone kwamba bila fimbo maisha yao yatakosa raha. Kimsingi wanapenda sana kuchapa, tena kuchapa mpaka mwanafunzi atoke uhai basi roho zao zinasuuzika.

Waraka wa elimu pamoja na sheria ya elimu na kanuni ya elimu, inaelekeza kwamba, adhabu ya viboko visivyozidi vinne inapaswa kutolewa na mwalimu mkuu husika wa shule kwa kuzingatia umri, jinsia na afya ya mwanafunzi.

Baada ya adhabu, mwalimu mkuu atahakikisha anarekodi jina la mwanafunzi husika, sababu ya kutoa adhabu, na jina husika la mwalimu husika.

Utaratibu huu umelenga kuepusha ukatili mashuleni, mauaji ya wanafunzi, na adhabu zilizozidi kipimo. Kwa kuzingatia hilo, utaratibu wa utoaji wa adhabu ya viboko umetengenezewa mfumo stahiki.

Lakini walimu wote wanalia. Wanataka kuchapa.

Nashauri walimu wote watakaokiuka utaratibu huu wa utoaji adhabu, baada ya kuchukuliwa hatua za kinidhamu kama kufukuzwa kazi na kusimamishwa, wapewe adhabu kali ya viboko. Ndio, wachapwe haswa maana hilo ndilo wanaloliamini na kulipenda sana.

Punda bila mjeledi haendi. Walimu wanaokiuka maaagizo wawajibishwe kikamilifu bila kusahau kuwasulubu kwa mboko toshelezi.

Mtoto laini laini, tumekusikia
 
Hapa fimbo tuu. Dawa ya mwanafunzi ni viboko. Watu hawajui kiasi gani wanafunzi hasa walio kwenye balehe walivyo watukutu na dharau. Hawaendi bila fimbo.
 
Hapa fimbo tuu. Dawa ya mwanafunzi ni viboko. Watu hawajui kiasi gani wanafunzi hasa walio kwenye balehe walivyo watukutu na dharau. Hawaendi bila fimbo.
Ni kweli. Lakini adhabu isiyozidi viboko vinne itatolewa na mwalimu mkuu husika wa shule.
 
Nimesema waalimu wanaokiuka maagizo.
Nazani ungetoa ushauri nini wafanye walimu katika malezi hasa kizazi Cha sasa cha watoto tulio nao,na si kuwapigilia walimu msumari wa moto kwenye kidonda hasa wanaovunja sheria,nini njia mbadala ya kuwalea watoto wetu hasa kwenye kizazi tulichonacho?
 
Ni kweli. Lakini adhabu isiyozidi viboko vinne itatolewa na mwalimu mkuu husika wa shule.
Hilo ni jambo ambalo haliwezekani.
Kwanza litawapa wanafunzi kiburi zaidi. Enzi zetu tulichapwa fimbo hadi unashindwa kukaa na hatukufa.
 
Nazani ungetoa ushauri nini wafanye walimu katika malezi hasa kizazi Cha sasa cha watoto tulio nao,na si kuwapigilia walimu msumari wa moto kwenye kidonda hasa wanaovunja sheria,nini njia mbadala ya kuwalea watoto wetu hasa kwenye kizazi tulichonacho?
Adhabu isiyozidi viboko vinne itatolewa na mwalimu mkuu husika wa shule kwa kuzingatia umri, jinsia na afya ya mwanafunzi. Baada ya adhabu, mwalimu husika atarekodi jina lake, jina la mwanafunzi, na sababu ya viboko.
 
Walimu Wanahasira kali kisa mishahara Yao midogo, hasira zinaishia kwa wanafunzi
 
Waalimu wana tabu sana yaani wamekuchapa ujue angalau kusoma na kuandika leo umekuja JF na uzi wa kuwadhihaki duh,bila fimbo mtoto wa uswazi kama wewe sijui sasa ivi ungekua unamkaba nani mitaani uko.
 
Back
Top Bottom