Kwa vigezo hivyo, ni haki yao watuone Mazuzu.
"Makalio ya sufuria hayaogopi moto"
Kuna mengi sana kuhusu upeo wa kujua mambo wa waafrika na tafiti hizi za wazungu. Kama angefanya mwafrika au mtu wa rangi nyingine jibu lingeweza kuwa tofauti au pengine hilo hilo kutegemeana na mazingira na wakati. Labda utategemea nini iwapo hata tafiti zetu zotei zinahitaji kusaidiwa na fedha na mawazo ya wazungu?
Lakini yote hayo ni matokeo ya kutawaliwa kwetu na hayo weupe ambapo pia ndio walioweka vigezo vya kupima uwelewwa wetu kupitia elimu ya mifumo ya kwao. yawezekana hata huyo mzunu aliyefanya utafiti IQ yake ni robo kibaba kama si kijiko cha sukari lakini kwa kuwa ni Mzungu ataheshimiwa na huo utafiti kachala!.
utafiti huu na inayofanana imefanywa na wazungu ili kuthibitisha upumbavu wetu lakini wao wanakwepa wajibu wa kuwa wamechangia na wanaendelea kuchangia kwa waafrika kuonekana ni wapumbavu zaidi.
Historia inatufundisha kuwa ugunduzi wa mambo mengi ulianzia afrika na wadugunzi wengi ni waafrika lakini kwa kuwa tumekuwa tukiytawaliw, kimwwili na kiakili na hao wazungu, kamwe huwezi kusikia tumefikia katika ngazi ya juu ya uwelewa (intellegence) kwa kuwa taratibu zote za kuwezesha kujua uwelewa wetu ni lazima zithibitishwe na wao wazungu.
Tumetawaliwa kimawazo na mfumo wa elimu ya magharibi kiasi kwamba sasa hatuwezi kubainisha yale tunayoyaweza bila kuwauliza wao kama rejea (reference).
Hatuwezi kujua kuwa yetu yanathamani pasipo kumuuliza au kuona mzungu akifanya na ndio maana hata vile vikubwa sana na tunavyohisi ni bora tunaviita "vyakizubgu (inzi wa kizungu, kuku wa kizungu, rangi ya kizungu, tabia za kizungu nk).
Kweli tutakuwa mapunguani kila siku kwa tabia zetu za kupokea kila toleo la mabiliko ya hao wazungu..hata mzungu akiwa mpuuzi vipi tunampapatikia, ataingia mpaka Ikulu bila vibali kisa mzungu.
Nani anapenda kukaa huko ulaya na marekani kama Afrika isingefujwa rasilimali zake kwa ajili ya kuwekeza katika nchi hizo za wazungu?.
Tofauti na Wayaudi ambao shida zao za utumwani kule Misri ziliwafunza maarifa na sasa wanaheshimika duniani kwa kuwa na IQ kubwa, sisi wabantu shida zetu tunatumia kujinadi kwa mataifa mengine na rasimilali zetu tunazigawa bure ili tutukuzwe kwa wema n ukarimu wetu na wao tukiwaheshimu na kuwaogopa kwa kuwa watatufanya tushindwe kuishi.
Wametubana kila kona, sasa tumekuwa wabeba mizigo ya wazungu na imekuwa sifa kwetu iwapo tutaonekana kama wao kwa tabia na miendendo yetu.
Pale inapofikia dhamira zetu zinatutuma tule, tulale, tunywe, tuvae, tutembee, tuongee,tusali, tuiembe, tulie, tulale, na hata tufe na kuzikwa kama wazungu ndipo hapo wenzetu wanatuona IQ zetu ni ndogo sana na zitaendelea kushuka na ndogo zaidi na zaidi mpaka kiama cha Ulimwengu!