Wa Machame wametoa wapi maendeleo haya?

gwambali

JF-Expert Member
May 10, 2011
230
76
Machame ni sehemu ya vijiji vilivyo endelea kuliko vijiji vyote Tz. Tuna umeme miaka mingi sana wakati sehemu nyingine ambako ni makao makuu ha wilaya hawajui umeme.! Kati ya matajiri 17 Tz wawili wametoka Machame

Wana maji safi na salama karibia kila nyumba na wale wasiyo na uwezo wakuvuta maji kwenye nyumba zao wametengewa mabomba ya maji ya umma, kila kilomita 50 kuna bomba la umma

Nyumba zao wamejenga kwa mpangilio mzuri utadhani mbezi Beach n`k . Pia hawa watu wamehamasika kielimu sana.Ukiangalia waziri aliye wapatia vyote hivi ni mchaga wa machame.na ndiye aliyekuwa waziri wa kwanza wa elimu
 
acha wivu wa kike fanya kazi na nyie mtatoka, ukiacha uliyoyasema angalia wengi ni wajasiriamali wa nguvu wanawapeleka puta hadi wahindi na waarabu! kariakoo na business kubwa zote wanaziongoza wao!
 
acha wivu wa kike fanya kazi na nyie mtatoka, ukiacha uliyoyasema angalia wengi ni wajasiriamali wa nguvu wanawapeleka puta hadi wahindi na waarabu! kariakoo na business kubwa zote wanaziongoza wao!

Ujasiria mali wao ndio umewapatia umeme toka miaka ya 70 ingali hadi leo kuna mikoa hapa tz ambayo hana umeme?
 
Ni kweli kabisa bila ya wivu wachaga wengi wana maendeleo leo hii huwezi kuona nyumba ya nyasi kwa upande wa wachaga ila wapare bado wanazo. We hushangai kila idara nyeti wachaga wapo kwa kweli ni watafutaji sana na ni wasomi sana, na wajanja sana. Yani ktk makabila ya Tanzania wanaongoza kwa mengi sana. Kwa kweli nafanya nao kazi si wakuchezea wako serios.
 
Machame ni sehemu ya vijiji vilivyo endelea kuliko vijiji vyote Tz. Tuna umeme miaka mingi sana wakati sehemu nyingine ambako ni makao makuu ha wilaya hawajui umeme.! Kati ya matajiri 17 Tz wawili wametoka Machame

Wana maji safi na salama karibia kila nyumba na wale wasiyo na uwezo wakuvuta maji kwenye nyumba zao wametengewa mabomba ya maji ya umma, kila kilomita 50 kuna bomba la umma

Nyumba zao wamejenga kwa mpangilio mzuri utadhani mbezi Beach n`k . Pia hawa watu wamehamasika kielimu sana.Ukiangalia waziri aliye wapatia vyote hivi ni mchaga wa machame.na ndiye aliyekuwa waziri wa kwanza wa elimu

mkuu mimi siyo mchaga wala mmachame ila siku moja niliamua kufuatilia kwenye mtandao historia ya tanganyika kabla ya uhuru na maisha ya watu yalivyokuwa, nilishangaa pale niliposoma kuwa maeneo ya uchagani miaka kabla ya uhuru wa Afrika ndo yalikuwa na maendeleo ya juu kuliko maeneo yote ya watu weusi chini ya jangwa la sahara. Walitoa maelezo kuwa hiyo ilitokana na ushirikiano uliokuwepo kati ya wakulima wa kahawa waafrika na wazungu, uwanzishwaji wa benki ya wakulima wa kahawa na chama chao cha ushirika vilichangia kuleta hayo maendeleo. Pili niligundua kuwa kumbe pesa za NBC baadhi yake ni zile zilizotaifishwa kutoka kwenye bank ya wachaga ilivyovunjwa ili kukidhi siasa za ujamaa na kujitegemea
Inashangaza sana kuwa historia haifundishwi kwa usahihi wake mashuleni na watanganyika hatujui kabisa historia ya nchi yetu, imagine eneo la nchi yako kuwa na maendeleo kushinda waafrika wengine wote katika miaka hiyo lakini mashuleni hatuambiwi??????
 
Ukiwa na tabia ya kurudi nyumbani kwako utagundua tatizo lililopo na kulitatua, hili limewasaidia wenzetu wachaga kwakale katabia kao kakuenda kuhiji kila desemba sababu wanagundua au wanajikwamua kwakuona hayo matatizo mojakwamoja. Na hili linatakiwa liigwe hata na wale wenzetu wa abroad mjitahidi kuwa mnarudi Bongo mlete mabadiliko mnayojifunza huko, msiwe kama from NYC the BIG SHOW maana amerudi dakika za mwisho na kutaka kupata vyeo vya nchi ili aibe ajenge wakati yuko nje miaka arobaini anachojivunia ni shamba tabata ambalo halina evidence yoyote kama alinunua kwa hela yake maana mzee wake alikuwa kwenye system miaka ya mafisadi
 
Chezea hawa watu na pesa ,wewe nasikia wakizaliwa tu,wanachambishiwa pesa hahahah!
 
kila baada ya kilomita 50??? Mbona mbali sana
,kila nyumba kumi kuna bomba la maji kwa ajili ya umma na wanalipia kila ndoo sh 20 tu na kuna kiongozi kwa kila bomba na wanadumisha usafi.
Pia wamachame wanafanya kazi kwa kujitolea hawasubiri sirikali,kila kijiji kina shule mbili za msingi na sekondari 1.na zimejengwa kwa nguvu za wananchi.kwenye kampeni hawapewe kanga wala ubwabwa ,muulize fuya kimbita
 
Machame ni sehemu ya vijiji vilivyo endelea kuliko vijiji vyote Tz. Tuna umeme miaka mingi sana wakati sehemu nyingine ambako ni makao makuu ha wilaya hawajui umeme.! Kati ya matajiri 17 Tz wawili wametoka Machame

Wana maji safi na salama karibia kila nyumba na wale wasiyo na uwezo wakuvuta maji kwenye nyumba zao wametengewa mabomba ya maji ya umma, kila kilomita 50 kuna bomba la umma

Nyumba zao wamejenga kwa mpangilio mzuri utadhani mbezi Beach n`k . Pia hawa watu wamehamasika kielimu sana.Ukiangalia waziri aliye wapatia vyote hivi ni mchaga wa machame.na ndiye aliyekuwa waziri wa kwanza wa elimu

Mkuu umekosea kwamba Wamachame sio wachagga,ila waweza badilisha ukaandika hivi wamachame wana maendeleo kuliko wachagga ,mjadala ndio ungekuwa mzuri zaidi
 
Back
Top Bottom