Wa Kulaumiwa Ni Nani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wa Kulaumiwa Ni Nani?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by X-PASTER, Mar 7, 2009.

 1. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #1
  Mar 7, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Amri za Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) tumeziacha nyuma ya migongo yetu na kuyafanya matashi yetu kuwa ndio muongozo wa maisha yetu.

  Uzinifu tumeufanya kuwa ni ada yetu na pombe ndio muongozo wa maisha ya leo. Imefika hadi ya kuona haramu kuwa halali na halali kuwa ni haramu. Tumejikubalisha kuwa akiba haina faida bila ya riba. Mauziano yasiyokuwa na uongo, utapeli sasa yamepitwa na wakati.

  Imekuwa ni desturi kuona kila kona za majengo na sehemu za mikusanyiko ya watu pamoja na barabarani kuwepo picha za utupu zenye kuamsha hisia za uzinifu. Sio matangazo ya biashara halali wala haramu zenye uadilifu wa kutilia mkazo ubinaadamu na haki za imani zisiopendelea picha hizo.

  Matangazo ya pombe yameshika kasi huku simu, sigara, vyakula na kadhalika vikiwa havipo nyuma kurusha mabomu ya uzinifu.

  Matokeo yake hayo, ni kubakia jamii kwenye matatizo na udhaifu wa mwaadamu wa uchu wa kutosheleza hisia zake kwa kujamiiana tu. Utakuta kwa mfano tangazo la simu lenye msichana aliyevaa jeans yenye kubana akiwa na mvulana aliyesokota nywele zake kwa mtindo wa rasta. Huku ujumbe wa tangazo hilo likisomeka:

  Nini tunawafunza vijana wetu kwa matangazo kama hayo? Na yareiti tangazo hilo lingelikuwa ni moja, lakini kona za barabara nzima zimetapakaa matangazo mfano wa hayo. Lahaula! Kama vijana hawakutoroka shule, tutegemee kutumbukia kwenye uzinifu wa kuiga hizo picha.

  Alhamdulillaah, tumepewa macho lakini hakika atakayeyakemea mambo hayo kwa sauti kali ndio ataambiwa kuwa ni kipofu, mpinga maendeleo, mjinga, hafai katika jamii, mshamba na kadhalika. Wale Waislamu wenye imani zisizoeleweka, ndio wataanza kumuita kwa istihzai na kejeli; Ustadh, Shaykh na kadhalika.

  Tuikumbuke kauli ya Mola (Subhaanahu wa Ta’ala) Aliposema kuwa tuna viungo lakini hatuvitumii:

  Na Tumeiumbia Jahannamu majini wengi na watu. Wana nyoyo, lakini hawafahamu kwazo. Na wana macho, lakini hawaoni kwayo. Na wana masikio, lakini hawasikii kwayo. Hao ni kama nyama howa, bali wao ni wapotofu zaidi. Hao ndio walioghafilika
  Al-A'araaf: 179

  Yote yametokana na wigo wa kuwaiga wasio kuwa Iman Juu ya Mwenyezi Mungu na kuanza kidogo kidogo kufuata tabia na vitendo vyao. Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

  ((Mtafuata nyendo za wale waliokuja kabla yenu hatua kwa hatua mpaka itafika hadi wakiingia katika shimo la kenge, na nyinyi mtaingia pia)) Wakasema (Maswahaba): Ewe Mtume! Je, unamaanisha Mayahudi na Manaswara? Akasema: (Hivyo nani basi mwengine?)
  Al-Bukhariy na Muslim
   
 2. BinMgen

  BinMgen JF-Expert Member

  #2
  Mar 8, 2009
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 1,816
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Kabla hatuja mtafuta nani wa kulaumiwa hatunabudi kutambua kwamba leo Ulimwengu mzima upo chini ya ukapitalistmfumo wa kidemokrasia, unaotenganisha dini na maisha, neno ushanganye dini na siasa ambalo ni maarufu sama katika jamii za kidemokrasia maanayake hasa usichanganye dini na maisha kwa maana. dini kando maisha kando hii ndio akida ya mfumo wa maisha unaotawala leo dunia ambao wamagharibi ndio mabwana wa mfumo huu, katika kitu kibaya zaidi kilichomo katika mfumo huu ni ile fikra ya uhuru ambayo serikali zote zaki Demokrasia duniani zinalinda uhuru wa kila mtu, kutokana na uhuru huu ndio kuna Walevi wako huru, mabaradhuli wako huru, Malaya wapo huru nk, na kila mwe balaa lake yupo huru kufanya iwapo atafuata taratibu zilizowekwa na serikali, serikali katika mfumo huu wa kikapitalist inacho jali ni kodi tu, na serikali itakupatia ulinzi juu ya jambo hilo. Katika nchi zilikomaa kidemokrasia haya yote tunayoyaona ni mambo maovu kwao wao si tatizo hata kidogo, kwani huo ndio uhuru uliomo ktk mfumo huu. Leo wana mtukana Mtume (s.a.w), serikali zao zinawalinda, kuwa huo ni uhuru wa kutoa maoni, Mapadri wanajitangaza kuwa ni mashoga waumini wao wanasema huo ni uhuru wa mtu binafsi. mfumo huu unamadhara mkubwa kwa waumini si Waislamu tu, hata Wakristo walio na ufahamu sahihi juu ya imani yao, mfumo huu umekuja kuzifungia dini zote katika majumba yao ya ibada, mfumo huu hauna tofauti yoyote na ukominist kwa upande wa dini wakominist akida yao hakuna Mungu, wakapitalist wao usichanganye dini na maisha. Lazima ieleweke maisha bila dini ni sawa na mbuga za wanyama, na haya ndio maisha tulionayo leo, tuendele kujadili ilituonenani wa kulaumiwa
   
  Last edited: Mar 8, 2009
Loading...