wa kike wa kiume yote mapenzi ya MUNGU | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

wa kike wa kiume yote mapenzi ya MUNGU

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Pdidy, Dec 17, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Dec 17, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 31,439
  Likes Received: 4,831
  Trophy Points: 280
  Mwanamke siku zote hujihusisha zaidi na undani wa kitu kuliko mwanaume.
  Hebu fikiria pale mtoto akizaliwa, mwanaume kitu ambacho atauliza siku zote “je mtoto ni wa kiume au wa kike?”
  Hicho ndicho kinachomhusu wakati huo na ndicho kinachomhusu kuhusu mtoto ambaye amezaliwa na mara nyingi akishajua hilo basi imetoka.

  Lakini mwanamke atamshika (hold) mtoto wake na kumuangalia (chunguza) kila kila kitu ataanza na vidole vya mkono na miguuni, sura kamili ya mtoto na atajua mtoto anafanana na nani baba (au baba anayemjua yeye mwanamke), nywele za mtoto, midomo, pua, mguu, kila kitu kuhusu mtoto.
  Mwanamke huwa sensitive hata kujua hisia mbalimbali za mtoto hadi aina ya mlio anaotoa akilia na zaidi anajiweka tayari kuwa mama na mlezi wa mtoto.

  Fikiria suala la harusi, mwanaume anachojua ni kuwa na harusi then mke ndani ya nyumba, lakini mwanamke huwaza na kutaka kujua kila kitu kuhusiana harusi kama vile rangi za nguo za harusi, aina za pete na duka gani wanaweza kupata, aina za nguo, maua, wapi watafanyia sherehe za harusi, aina ya wageni, nani atafungisha ndoa na kwa nini, atataka kujua nani atatoa huduma ya chakula na chakula gani kiwepo nk.
  Yupo tayari kuzunguka mji Mzima kujua ni duka gani atapata kile anataka kwa ajili ya harusi yake.
  Naamini ukimwachia mwanaume kila kitu kuhusu harusi anaweza ku-ruin au screw siku yako muhimu duniani maana mwanaume anachosubiri ni kukuvalisha pete na mwanamke kuwa ndani ya nyumba.
  Wapo wanaume ambao pia wapo makini sana na details za kila kitu ila wanawake wao ni wengi zaidi.

  Ukinunua gari mwanamke atataka kujua ni rangi gani. Ingawa mwanaume anaweza kuona rangi ya gari ni rangi tu muhimu ni aina ya gari linalodumu.

  Pia wanawake hukumbuka sana mambo yote yanayohusiana na kalenda, kama vile birthday, anniversary na appointments.
  kama ni mwanaume ni vizuri kukumbuka siku maalumu za maisha yako na ya mpenzi wako kwani ukijisahau anaweza kuhisi humjali.

  Hata mkishaoana mwanamke huwa bado anakumbuka undani wa mwanaume jinsi alivyokuwa anafanya wakati wa wachumba au wakati unafanya juhudi za kumpata, anakumbuka siku amekutana na wewe mwanaume, anaweza kukwambia hata shati ulilokuwa umevaa, kiatu na hata mahali na mpangilio wa vitu ulivyokuwa sehemu mlipokutana mara ya kwanza.

  Anakumbuka sana jinsi ulivyokuwa unamkumbatia na kumpa sifa zote kwamba yeye ni mwanamke bora duaniani na hakuna kama yeye.
  Anakumbuka sana ulivyokuwa unamsifia mbele za rafiki zako na kila aina ya maneno matamu ulikuwa unamwambia ndiyo maana sasa anashangaa mbona upo hivyo.

  Kumbuka mwanamke na mwanaume ni tofauti na hizi tofauti ndizo zinatufanya tuwe na mahusiano mazuri ya ya kudumu na yanayoridhisha kiroho, kimwili na kiakili na pale tunapojisahau ndipo tunarudisha nyumba maendeleo ya kukua kwa mahusiano yetu na matokeo yake kila mmoja anaanza kushangaa vipi upendo mbona unapoa.

  Pia kumbuka vitu vidogo sana ambavyo zamani ulikuwa unafanya ni muhimu sana nab ado unahitaji kufanya tena na tena bila kuacha.
  Upendo daima!
   
 2. p

  prosperity93 Member

  #2
  Dec 18, 2009
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 58
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  mama mia asante kwa ujumbe wako mzuri kwa forum yetu...

  naomba wataalam zaidi wa kujadili eneo hili hasa RIGHT BRAIN AND LEFT BRAIN na effects zake kwa wanawake na wanaume. kwani hili litapunguza migongano kati ya jinsia hizi
  mfano mama yangu akinipigia simu na tukaonge kwa nusu saa, mke wangu atapenda kujua kila kitu tulichoongea yaani kama vile kurudia kila kitu nilichoonge wakati mimi mwanaume nitasema kwa mkato tu "mama anakusalimu sana na anaendelea vizuri"
  mfano wa pili....Rais wa nchi akifariki mwanaume atapenda kujua nani anachukua madaraka, je jeshi limejipanga vipi, uchaguzi ni lini n,k ila kwa mwanamke atawaza...jamani watoto wake, jamani mke wake namwonea huruma sana kafiwa na mumewe". Hii ni sehemu tu ya jinsi jinsia mbili akili zao za kushotom na kulia zinavyofanya kazi.
  naombeni wajuzi watupe details zaidi.
   
Loading...