Wa Jangwani si mkutano wa 'wapinzani'!

Wa Jangwani si mkutano wa 'wapinzani'!

Katiba imeshajadiliwa kwenye mabaraza. Maoni yote yameshapelekwa kwa tume.

Huo ndio utaratibu tuliokubaliana kistaarabu. Haya mengine ni siasa tu, zenye lengo la kuifanya Katiba iwe ya vyama vya siasa.

Katiba ni ya wananchi wote, sio ya Lipumba, Mbowe na Mbatia wanaoshinikiza mchakato uwe mali ya vyama vyao.
Kweli kwani katiba si ya Watu wa Dar peke yao.
 
Hata hauelewi unachoandika Katiba imeishajadiliwa siku nyingi.

Tunachokwenda kujadiliana ni muswada wa sheria ya uandikaji wa katiba mpya ilivyo na mapungufu na ilivyopitishwa kibabe pamoja na mapungufu yake pale bungeni....! Baada ya hapo wananchi wenye mapenzi mema na nchi yao wataamua wafanye nini....! Nadhani tumeelewana!!!!
 
Katiba imeshajadiliwa kwenye mabaraza. Maoni yote yameshapelekwa kwa tume.

Huo ndio utaratibu tuliokubaliana kistaarabu. Haya mengine ni siasa tu, zenye lengo la kuifanya Katiba iwe ya vyama vya siasa.

Katiba ni ya wananchi wote, sio ya Lipumba, Mbowe na Mbatia wanaoshinikiza mchakato uwe mali ya vyama vyao.

By nature, Human being is a political animal.....
Kwa hiyo waache wanaoijua siasa waitendee haki!
 
Tunachokwenda kujadiliana ni muswada wa sheria ya uandikaji wa katiba mpya ilivyo na mapungufu na ilivyopitishwa kibabe pamoja na mapungufu yake pale bungeni....! Baada ya hapo wananchi wenye mapenzi mema na nchi yao wataamua wafanye nini....! Nadhani tumeelewana!!!!

Sana tu
😛eace:
 
CCM mwisho wao unakaribia,maana mambo wanayoyafanya wakati mwingine ni ya aibu kwelikweli.
 
Ni upotofu kudhani kuwa katika Viwanja vya Jangwani leo kutakuwa na mkutano wa wapinzani.Tena wapinzani wa Katiba. Leo tarehe 21/9/2013,watanzania wenye mapenzi mema juu ya mustakabali wa Taifa lao hili watajumika,kuzungumza na kuazimia juu ya Katiba mpya-yaani jinsi mchakato wake uendeshwavyo. Ingawa CHADEMA,CUF na NCCR-Mageuzi wanaweza kuonekana kama ndio wenye mkutano wa Jangwani,ukweli ni kuwa mkutano huo ni zaidi ya vyama vya siasa.

Hoja kuu ya Mkutano wa leo wa Jangwani ni kukosoa kupitishwa 'kihuni na kibabe' kwa Muswada wa Sheria ya Katiba ambao,pamoja na mambo mengine unadadavua jinsi ya kuwapata Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba;jinsi ya kupiga kura kuikubali/kuikataa Rasimu ya Katiba na kadhalika.Tulishuhudia jinsi wapinzani walivyoghafilika Bungeni na kuamua 'kususia' Muswada huo kwa kutoka nje. Bila hata ya kuzingatia akidi ya kuchangia na kupitisha,chama chetu cha MAPINDUZI kikajadili na kupitisha Muswada huo.

Sasa Muswada husika unasubiri saini ya Rais Kikwete ili uwe Sheria. Mkutano wa leo wa watanzania wapenda nchi yao wa Jangwani una nia ya kutuma ujumbe mmoja kwa Rais. Ujumbe wa kwamba asisaini Muswada husika hadi kwanza urejeshwe Bungeni;ujadiliwe kwa kina na kupitishwa kwa akidi zinazotakiwa na Kanuni za Kudumu za Bunge za mwaka 2007. Rais leo atapigiwa kelele za kuomba msaada wa kusikilizwa. Rais ataombwa kwa yowe na hoja. Leo ndio leo. Asipoisikia sauti ya watanzania wa Jangwani leo,tutasubiri kuona kitakachofuata. Lakini,Jangwani hawakutani wapinzani kichama wala katika minajiri nya kuipinga katiba na mchakato wake.

Karibuni wote.Nami,kamamtanzania mzalendo, leo siendi Lumumba.Nakwenda Jangwani kujumuika na watanzania wenzangu kutuma ombi kwa Rais Kikwete. Ombi la kusikilizwa na kulinda ustaha wa kuundwa kwa Katiba yetu. Taifa kwanza,chama baadaye!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam.

IMG00473.jpg
 
Hivi huu mswada unasema nini kuhusu katiba ni marekebisho gani yanawapa kiwewe wapinzani,unahusu kuunda bunge la katiba au nini kwani Tume ya kuunda katiba ipo,mabaraza ya wilaya tayari yameshatoa maoni asasi mbalimbali pia tayari wameshatoa maoni maani yao makundi mbalimbali nayo tayari tunachosubiri ni bunge la katiba baada tume kutengeneza rasimu ya pili bunge la katiba inapitia na kuurekebisha na kuupitisha tayari kwa Watanznia kuupigia kura ya ndiyo na hapa.Sasa hoja ya marekibisho ni ya kuunda Bunge la katiba namna ya kupata wajumbe wale 166 au nini?
Watanzania tuwe makini na vyama vya siasa na viongozi wao hawa ndio chimbuko la kuvunjika kwa amani katika dunuia hii kwa ajili ya maslahi yao ya kisiasa(conflict of interest) wala sio maslahi ya wananchi.Mh. Rais nafikiri utumie busara kuuelimisha uma wa Tanzania tufahamu hawa wajumbe 166 wanapatikanaje wasitokane na wnasiasa sehemu kubwa wawe wakulima wa kawaida,wafugaji na wafanyakazi wa chini ambao ndio wengi na ndio wanaonyanyasika katika dunia hii ikiwemo Tanzania.
Wanasiasa wasiteke nyara katiba ili waendelee kutawala kwa manufaa yao badala ya kuwajibika. Tunaona Bunge letu lisivyo wajibika viti vikavu miswada inapitishwa na wachache ndio tunaanza kulalama huko ndio wanatumia kodi zetu kunywa kulewa na matusi Bunge. AIBU TUPU.
 
Kikanuni mswada umepita na lazima usainiwe, mengine ni manjonjo tu, wanachoweza kufanya ni kupeleka bunge lijalo mapendekezo ya marekebisho ya sheria husika mikutano hii ni porojo tu.

Tuambie nani na nani waliujadili huo mswada? Maana baada ya wabunge wenye akili timamu kuondoka bungeni, waliobakia hawakujadili mswada tena bali waliwajadili waliotoka nje ya ukumbi wa bunge kana kwamba cuf, nccr, cdm, ndiyo mswada wenyewe...mda mwingine tumieni hata akili za kuazima
 
Hivi huu mswada unasema nini kuhusu katiba ni marekebisho gani yanawapa kiwewe wapinzani,unahusu kuunda bunge la katiba au nini kwani Tume ya kuunda katiba ipo,mabaraza ya wilaya tayari yameshatoa maoni asasi mbalimbali pia tayari wameshatoa maoni maani yao makundi mbalimbali nayo tayari tunachosubiri ni bunge la katiba baada tume kutengeneza rasimu ya pili bunge la katiba inapitia na kuurekebisha na kuupitisha tayari kwa Watanznia kuupigia kura ya ndiyo na hapa.Sasa hoja ya marekibisho ni ya kuunda Bunge la katiba namna ya kupata wajumbe wale 166 au nini?
Watanzania tuwe makini na vyama vya siasa na viongozi wao hawa ndio chimbuko la kuvunjika kwa amani katika dunuia hii kwa ajili ya maslahi yao ya kisiasa(conflict of interest) wala sio maslahi ya wananchi.Mh. Rais nafikiri utumie busara kuuelimisha uma wa Tanzania tufahamu hawa wajumbe 166 wanapatikanaje wasitokane na wnasiasa sehemu kubwa wawe wakulima wa kawaida,wafugaji na wafanyakazi wa chini ambao ndio wengi na ndio wanaonyanyasika katika dunia hii ikiwemo Tanzania.
Wanasiasa wasiteke nyara katiba ili waendelee kutawala kwa manufaa yao badala ya kuwajibika. Tunaona Bunge letu lisivyo wajibika viti vikavu miswada inapitishwa na wachache ndio tunaanza kulalama huko ndio wanatumia kodi zetu kunywa kulewa na matusi Bunge. AIBU TUPU.

Mda wa kuandika unao, ila mda wakufatilia mambo ya siasa na bunge huna, ndo maana unawashangaa wapinzani, acha nikuelemishe kidogo tu.

Umesema katiba hii unataka iwe ya wakulima?
Pili unataka kuelemishwa kuhusu hao wajumbe 166, iko hivi, kamati ya bunge ya sheria na katiba ilishauri wajumbe hao wachaguliwe na taasisi zao moja kwa moja, mfano, umoja wa vijana wa ccm wateue mjumbe wao mmoja aende kuwa kwenye bunge la katiba bila kupita kwa rais, maccm nao wanataka umoja wa vijana wa ccm wachague wajumbe 9 kisha majina hayo yapelekwe kwa rais ili ayadhibitishe, wakati huo huo kumbuka rais ni mwenyekiti wa ccm..swali: likipelekwa jina mtu acye mpenda atalichagua?

Pili katika majina hayo rais kapewa mamlaka ya kutoteua jina lolote kati ya hayo tisa, mpk hapo utakuwa ushaelewa why wapinzani wanapiga kelele mkuu
 
mbowe na wenzake akili zao zinafaa kutumika kwenye diaco tu basi wamekimbia bunge halafu wanakwenda kupinga mswada jukwaani .
Spika atakuwa nani na hizo hansad mwandishi ni nani hata katibu wa bunge mmemtoa wapi.

attachment.php
 
Huyu jamaa wala hajui misingi ya demokrasia.

Demokrasia imeheshimiwa. Katika mfumo wa dekokrasia watu wachache hawawezi kulazimisha matakwa yao dhidi ya watu wengi.
Democracy is not just about winning elections, it’s also about how are you working with an opposition; how do you treat dissenting voices; how do you treat minority groups. - President Barack Obama (01.07.2013 - Ikulu Dar)
 
Back
Top Bottom