VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,007
Ni upotofu kudhani kuwa katika Viwanja vya Jangwani leo kutakuwa na mkutano wa wapinzani.Tena wapinzani wa Katiba. Leo tarehe 21/9/2013,watanzania wenye mapenzi mema juu ya mustakabali wa Taifa lao hili watajumika,kuzungumza na kuazimia juu ya Katiba mpya-yaani jinsi mchakato wake uendeshwavyo. Ingawa CHADEMA,CUF na NCCR-Mageuzi wanaweza kuonekana kama ndio wenye mkutano wa Jangwani,ukweli ni kuwa mkutano huo ni zaidi ya vyama vya siasa.
Hoja kuu ya Mkutano wa leo wa Jangwani ni kukosoa kupitishwa 'kihuni na kibabe' kwa Muswada wa Sheria ya Katiba ambao,pamoja na mambo mengine unadadavua jinsi ya kuwapata Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba;jinsi ya kupiga kura kuikubali/kuikataa Rasimu ya Katiba na kadhalika.Tulishuhudia jinsi wapinzani walivyoghafilika Bungeni na kuamua 'kususia' Muswada huo kwa kutoka nje. Bila hata ya kuzingatia akidi ya kuchangia na kupitisha,chama chetu cha MAPINDUZI kikajadili na kupitisha Muswada huo.
Sasa Muswada husika unasubiri saini ya Rais Kikwete ili uwe Sheria. Mkutano wa leo wa watanzania wapenda nchi yao wa Jangwani una nia ya kutuma ujumbe mmoja kwa Rais. Ujumbe wa kwamba asisaini Muswada husika hadi kwanza urejeshwe Bungeni;ujadiliwe kwa kina na kupitishwa kwa akidi zinazotakiwa na Kanuni za Kudumu za Bunge za mwaka 2007. Rais leo atapigiwa kelele za kuomba msaada wa kusikilizwa. Rais ataombwa kwa yowe na hoja. Leo ndio leo. Asipoisikia sauti ya watanzania wa Jangwani leo,tutasubiri kuona kitakachofuata. Lakini,Jangwani hawakutani wapinzani kichama wala katika minajiri nya kuipinga katiba na mchakato wake.
Karibuni wote.Nami,kamamtanzania mzalendo, leo siendi Lumumba.Nakwenda Jangwani kujumuika na watanzania wenzangu kutuma ombi kwa Rais Kikwete. Ombi la kusikilizwa na kulinda ustaha wa kuundwa kwa Katiba yetu. Taifa kwanza,chama baadaye!
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam.