vyuo vikuu vya Tanzania vyatia aibu

vyuo vikuu vya Tanzania vyatia aibu

Ptz

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2011
Posts
541
Reaction score
385
Heshima yenu wakuu! Leo hapa Dar es Saalam katika chuo kikuu cha Dar es Saalm sehemu ya Mlimani kumezinduliwa rasmi mashindano ya vyuo vikuu vya Afrika Mashariki vikijumuisha Tanazania, Uganda na Kenya, cha kushangaza Tanzania kama wenyeji ni vyuo vikuu sita ndo vimeshiriki vikiwepo DUCE, Mkwawa, Tumaini Iringa, SUZA. Mount Meru na Ardhi wakati Kenya wameleta vyuo 17, na Uganda pia vyuo 17. Nimefanikiwa kungalia mechi ya ufunguzi ya soka iliyofanyika Mabibo Hostel kati ya Chuo cha Zanzibar na Kyambogo Uganda Zanzibar wamepigwa goli nne kwa mbili, na Mechi ya pili ilikuwa kati ya Tumaini ya Iringana Makerere Uganda Tumaini wamepigwa goli mbili kwa sifuri. Mashindano haya yamefunguliwa na Waziri wa michezo Dr Fenera main Campus, pamoja na hayo kumethibitika kuwa na maandalizi mabovu.
 
Wenyeji wanawakilishwa na Vyuo Sita tu? Hivi sisi tunaweza jambo gani? Zain challenge tulikuwa tunapuuza, taaluma pia na michezo? Halafu nimesikia timu ya UDSM ilitaka kugoma kucheza leo baada ya kutopewa pesa mapema. Hata hivyo wameifunga DUCE jioni hii.
 
Back
Top Bottom