Vyuo Vikuu Tanzania vyaanguka

WENYELE

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
1,291
2,000
Vyuo vikuu vitatu vya Tanzania
ambavyo vilishiriki katika
mashindano ya mjadala wa Afrika
kuhusu Sheria za kimataifa za haki
za kibinaadamu yalioandaliwa na
kamati ya kimataifa ya shirika la
msalaba mwekundu ICRC
vimeshindwa kufika katika raundi
ya mwisho.
Badala yake vyuo hivyo viliondolewa
katika raundi za mapema ambapo
mataifa manane ya Afrika yalishiriki.
ICRC imekuwa ikiandaa hafla kama
hizo kwa kipindi cha miaka 14 sasa
mjini Arusha.
Kulingana na gazeti la the Citizen
nchini Tanzania, vyuo
vilivyoiwakilisha Tanzania ni chuo
cha kanisa katoliki cha Ruaha kutoka
Iringa,Chuo cha Iringa na Chuo
kikuu cha Zanzibar.
Katika raundi ya mwisho ya
mashindano hayo yaliofanyika
mwishoni mwa wiki katika
mahakama maalum ya kimataifa
inayochunguza mauaji ya kimbari
nchini Rwanda ICTR mjini
Arusha,chuo cha Strathmore
University kutoka Kenya kiliibuka
mshindi na kufuatiwa na chuo cha
Christian University kutoka Uganda
huku chuo cha Kunduyi pasi kutoka
Zimbabwe kikiibuka mshindi wa
spika bora.
Raundi ya mwisho ya mjadala huo
ilisimamiwa na jaji wa mahakama
hiyo Vagn Joensen,jaji wa mahakama
kuu ya Tanzania Stella Mugasha,jaji
wa mahakama ya haki katika Afrika
mashariki Fanstin Ntezilyayo,John
Joseph Wamwara na Mutsa mangezi
kutoka ICRC.
Judge Joensen, ambaye alitoa zawadi
kwa washindi aliyapongeza
mashindano hayo kama kifaa cha
kuwahamasisha wanafunzi wa vyuo
vikuu wanaofanya sheria na kwamba
itasaidia kuimarisha maono yao
katika siku za usoni.
Source:BBC
 
AdvocateFi

JF-Expert Member
Jan 15, 2012
11,511
2,000
Tatizo vyuo vilivyowakilisha nchi yetu ni vyuo mbuzi, wangepeleka state university kama UDSM na Mzumbe tusingepata aibu hii.
 
Mkaruka

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
13,316
2,000
Tanzania ni vyuo vya maksi kubwa amma bonge la GPA!Ukihitimu unaenda kupewa kazi then ujipendekeze kwa boss wako(aidha muhindi,fisadi,mkenya au mzungu)akupangie kakitengo uanze kunyanyasa watz wenzio huku ukiibaiba ndio maisha yasonge.THAT'S OUR TRUE EDUCATION. Wenzetu wanazindua gari(UGANDA)Sisi tunafurahia GPA.
 
mkubwa 21

JF-Expert Member
Nov 12, 2014
442
195
tatizo vyuo vilivyowakilisha nchi yetu ni vyuo mbuzi, wangepeleka state university kama udsm na mzumbe tusingepata aibu hii.
udism zamani sio siku iz dogo... Madogo cku iz mmekiaribu icho chuo tuliosoma hapo zaman ndo kilikua na heshima afu achen kuzarau vyuo vyote tanzania ni bora, usije ukaona umeenda na kidiv 2 udism ukajiona bora wakati kuna ambaye ameenda ruaha na div 1... Mwisho wa siku kazin mko pamoja.
 
ndechilio shoo

JF-Expert Member
Feb 16, 2013
999
1,225
kuna jamaa wana one ya 5 4 7 6 hawa nilisoma nao seminary ila wote wapo kwenye vyuo vikuu ambayo havina majina ki vile,tumain,st joseph nk tatizo madogo mmezaliwa polini ndo maana udsm mnaona dili wakati sisi watoto wa mjini ambao tumesoma tution mwenge mapambano hapo udsm, u class a.k.a ardhi ndo ilikuwa prepo mida ya usiku nimeamini ukizaliwa kijijini au ukiwa wa kwanza kufika chuo lazima uwe una kaulimbukeni furani
 
zinc

JF-Expert Member
May 24, 2013
1,354
2,000
Tatizo vyuo vilivyowakilisha nchi yetu ni vyuo mbuzi, wangepeleka state university kama UDSM na Mzumbe tusingepata aibu hii.
Hahahaaa ...!!! Una mawazo positive lakini!!! Ila sijui kama unajua hivyo vyuo mbuzi viliwakilisha tz baada ya mchujo kufanyika hapa bongo. Sasa labda tuseme tatizo siyo vyuo bali ni wanafunzi wenyewe
 
NullPointer

JF-Expert Member
Feb 7, 2011
3,467
2,000
sorry to say hivo vyuo ulivovitaja nlikua sijui hata ka vipo Tanzania.. Ila wamejifunza, next time wanajua what they are up against
 
Perry

JF-Expert Member
Feb 24, 2011
9,995
2,000
Hahahaaa ...!!! Una mawazo positive lakini!!! Ila sijui kama unajua hivyo vyuo mbuzi viliwakilisha tz baada ya mchujo kufanyika hapa bongo. Sasa labda tuseme tatizo siyo vyuo bali ni wanafunzi wenyewe
huo mchujo ulifanyika lini,wapi,vyuo vingapi vilishiriki na ni mamlaka gani ya serikali iliyoendesha huo mchujo?
 
Perry

JF-Expert Member
Feb 24, 2011
9,995
2,000
sorry to say hivo vyuo ulivovitaja nlikua sijui hata ka vipo Tanzania.. Ila wamejifunza, next time wanajua what they are up against
me binafsi cjui mpaka leo hvyo vyuo kama viko hapa tanzania,me nijuavyo tanzania vyuo ni udsm,sua,udom,mzumbe,muhimbili na ardhi..sasa sijui hvyo vingne vimetoka wapi!
 
KILLANEKELI

JF-Expert Member
Nov 26, 2013
295
0
Jamani acheni kuishi kwa kukariri, kuna watu wanadhan labda RUCO, TUMAIN na Zanzibar viliteuliwa tu vituwakilishe, aya mashindano yalianza na ngazi ya kitaifa, hao UDSM na Mzumbe mnaowasifu waligalagazwa vibaya kwenye hatua ya kitaifa
 
KILLANEKELI

JF-Expert Member
Nov 26, 2013
295
0
Nyie mnadhan ndo miaka ile ya ujinga tuliamin UDSM ndo kila kitu, nenda ivi vyuo vidogo mnavyovidharau kuna watu wako vizuri huwezi amin, kwa waliofatilia aya mashindano wameona jinsi madogo toka RUCO na Zanzibar walivyojitaid, kwa msomi hawezi dharau
 
wamejitahidi then wakafika wapi sasa zaidi ya kwenda kutia aibu huko?
 
lusungo

JF-Expert Member
Jan 4, 2014
21,204
2,000
Jamani acheni kuishi kwa kukariri, kuna watu wanadhan labda RUCO, TUMAIN na Zanzibar viliteuliwa tu vituwakilishe, aya mashindano yalianza na ngazi ya kitaifa, hao UDSM na Mzumbe mnaowasifu waligalagazwa vibaya kwenye hatua ya kitaifa

Achana nao maana wanabisha bila ufahamu....
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom