Vyuo vikuu bora Africa, UDSM tupa kule

Makerere University, bado chuo bora kabisa Africa Mashariki wamepita wanasiasa wetu wengi. Nyerere, Fundikira, Mbowe, Mwapachu.
 
Kwakeli imenisikitisha kidogo Udsm da waache siasa na wa concetrate kwenye ACademics na kikwete na serikali zinazokuja waache kuwatoa wahadhili Ma prof kuwa mawaziri kikwete ndio kapunguza ule moto pale maana kawatoa wengi sana kwenye serikali yake wamebaki ma junior prof's na Dr's
 

duuuh hapana kwakweli hizi lawama nyingine tunamjazia ambazo hata hazimhusu lakini hata ivo sina cha kuongezea naona mawazo yetu yapo mbali mbali mbingu na ardhi.. we amini tu unachokiamini bwana
 
Ndugu, 4icu haipimi ubora wa vyuo kitaaluma na hapa ndipo utakapobaini ubogasi wa ma-profesa wetu manake nakumbuka siku Profesa Mkandala alipotoka mbele ya media kufurahia nafasi ya UDSM kwa kupitia takwimu za 4icu! Binafsi, am Online Researcher na hao 4icu si miongoni mwa source zinazotoa data za vyuo bora duniani kitaaluma lakini The Times Higher Education aliowataja OKW BOBAN SUNZU ndio wanaoaminika hata kwa Ulaya na Amerika! Kwetu sie wengine hizi ni habari njema kuona The Times Higher Education hivi sasa wanatoa data hadi kwa vyuo vya Afrika manake tulikuwa tunapata taabu sana eneo hilo kwavile walikuwa hawashughuliki na vyuo vya Afrika kwahiyo ilikuwa inapokuja issue ya secondary data unayohusiana na vyuo bora Africa, watu hatukuwa na credible source zinazoaminika na wenye dunia yao!!!
 
Last edited by a moderator:
watu wako busy na kushabikia wanasiasa badala ya kufanya tafiti na kupublish.
wanafikiria matumbo yao zaidi.
ila serikali nayo ndio inaua vyuo vyetu. hawapeleki bajeti ya tafiti huko vyuoni.
 
Makerere University, bado chuo bora kabisa Africa Mashariki wamepita wanasiasa wetu wengi. Nyerere, Fundikira, Mbowe, Mwapachu.

ritz Acha utoto mbowe huyu macho kumchuz division zero
 
Tutaacha kuwa nje huku mkandara na jopo lake wakibuni digrii za kikuda na kuzitoa nyingine kwa wanasiasa kama zawadi eg PhD in laws ya baba riz,c ukuda huu,nasubir dit nao wampe PhD ya kuvuruga anga maana cjui kama kuna airport jamaaa hawamjui
 
Wakuu hii kitu Imetolewa BBC TV, hivyo mtoa mada hana hatia. Mimi pia imenistua sana.
Mkuu Nyenyere, nini kimekushtua? Hapa nimeshawahi kukuhoji kwamba hivi tunaposema zamani elimu yetu ilikuwa bora tulikuwa tunajilinganisha na nani?! Tanzania tumezoea kujivika sifa ambazo hazijakuwa researched anywhere! Watanzania tulikuwa tunaambiana kwamba nchi yetu inaongoza kwa upelelezi Afrika! No any legit research had ever said so lakini bado tunaaminishana kwamba tupo top in intelligence! Watanzania kwa miaka mingi tulikuwa tunaaminishana kwamba nchi yetu inafahamika sana duniani!! Waliokuwa wanatoka nje ya Afrika wanafahamu mtu unapotaka kumwelekeza where Tanzania is ni lazima utumie reference ya Kenya... it sucks but that's how it was ingawaje tulikuwa tunaaminishana nchi yetu inafahamika duniani! Mifano ipo mingi lakini hata tukija kwenye hii mada, swali langu linarudi pale pale; nini kimekushitua? Wengi wetu tulikuwa tunaaminishana kwamba UDSM ni chuo bora kupitia 4icu.org! Like I said earlier post, am Online Researcher na hawa 4icu sio miongoni mwa source zinazotambulika kwenye kutoa university ranking na hata ukisoma research methodology wanayotumia, utaona wazi kwamba data zao hazilengi ranking by academic standing! Hao Times Higher Education ndio wanaoaminika duniani... ukiona Harvard, Stanford, Oxford na wenzao wanatoka kifua mbele na kujivunia "utafiti unasema we're.....!" basi huwa wanatumia takwimu za Times Higher Education na sio 4icu.org! Unafortunately, hawa Times Higher Education walikuwa hawatoi takwimu kwa vyuo vikuu vya Afrika... nadhani ndo wanaanza hivi sasa na wakishatukurupusha namna hii kwamba we'r nothing huenda hatimae watu wataamka na kuacha zile mbwembwe kwamba vyuo vyetu ni bora ingawaje output yetu haifanani na hizi mbwembwe zetu!!!
 
Last edited by a moderator:
Makerere University, bado chuo bora kabisa Africa Mashariki wamepita wanasiasa wetu wengi. Nyerere, Fundikira, Mbowe, Mwapachu.
Kamanda unataka kusema nini hasa,kuna jungu unajaribu kupika
 
Watanzania tuache ushabiki wa ccm na ukawa kwenye masuala yenye tija kwa taifa. Wewe unaponda kiwango cha elimu nchini mwako wakati wewe mwenyewe umesoma humo na unafanya mambo ya maana kwa kutumia elimu yako. Wenzetu Kenya na Uganda unasifia kiwango cha elimu na kujivunia. Mbona wapo waliosoma Makerere na Nairobi tupo nao na ni wa kawaida tu. Au mnafikiri mkiponda kwa kuwapa wazungu taarifa za kuandikia ripoti ndo mtapewa nafasi ya kusoma Harvard? Wakati mwingine ongea hali halisi acheni ushabiki wa kisiasa. Pendeni nchi yenu kama majirani wanavyotamani wangezaliwa Tanzania.
 
Udsm jina tu cku izi kama ilivyo kwa makongo secondary
 

Umekurupuka Mzee,uombe radhi waudsm
 
Jamaa alitaka kutuviringisha!!!Duu!!Nadhani hiyo taarifa alitoka nayo kwenye daladala...
Mkuu hii habari ata mimi nimeiona kwenye page ya BBC.Lazima tukubali kuwa elimu ya bongo arobaini yake ilipita siku nyingi baada ya mazishi.Tutafute namna ya kuvirudisha kwenye rank za kimataifa.
 
Mwaka 2011 nilikuwa UDBS.

Kusema ukweli MBA programme yao sio "adding Value MBA". Nilisoma trimester 3 nakaamua kuacha na kwenda kusoma online Msc ya University of Liverpool.

Kwa kifupi huwezi tofautisha MBA na BCom degree.

Utakavyoingia almost ndivyo hivyo hivyo utakavyotoka.
 
Tatizo la vyuo vyetu viko kwenye uwezo wa ku maintain Quality Standards.

Kwa mfano hapo UDBS. Mtu anamaliza undergraduate degree June mwezi wa kumi mwaka huo huo wanampa admission ya Masters while mtu huo hayupo kwenye academic staff programme

Mwisho wa siku huyo mtu atakuwa anasoma hiyo MBA kwa kukariri na akimaliza anaishia kwenda Voda/Tigo kuwa call agent.

Purpose ya MBA ni ku enhance potential ya mtu ambaye tayari yupo kazini na ana experience
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…