mwaka 2008/9 UDSM ilikuwa ya 13 kwa ubora barani Afrika ikipitwa na vyuo vikuu 12 tu na vyote vikiwa toka bondeni kwa madiba. chuo kingine kilichofuatia nyuma kilikuwa University of Cairo. mwaka huo UDSM ilikuwa ya 800+ (nadhani 823 kama sikosei) duniani
Nashangaa miaka 6 baadaye Udsm haipo kwenye 30 bora za afrika. hii ni aibu kwa kweli. university of Makerere ilikuwa ya 18 na university of Nairobi ilikuwa mbali kabisa mwaka huo
miongoni mwa vigezo walivyotumia ni kuangalia publication kutoka kwenye chuo husika.
swali langu ni je wahadhiri wa udsm mnafanya research kweli na ku-publish? au mmebaki na title zenu za u-professor na u-docta?
kama hamfanyi tafiti na mmebaki tu kuprojekti powerpoint kuwalisha wanafunzi tafiti walizofanya wenzenu basi maendeleo kwa taifa hili yatakuwa ndoto
msisingizie fundi kwa sababu uchumi wa uganda na kenya hauchekani na wetu. kama hao wameweza ku-compete kupata fundi kwa nini nyie mshindwe wakati mna viwango vya elimu vinavyofanana kimataifa?