Vyuma vilikaza enzi hizo!

Vyuma vilikaza enzi hizo!

Maisha yapo kawaida tuu...

Enzi unazozungumzia nadhani ni baada au kipindi cha vita ya kagera, kama sijakosea... ndiyo nchi ilifunga mkanda na vyuma kukazika kisawa sawa...

Wanaolalamika vyuma kukaza bado hawajaona maana halisi ya vyuma kukaza, waache sasa wafanye haya maandamano wanayotaka kufanya alafu waone vyuma vitakavyokaza...

cc: mahondaw
Kongole @ Smart911. MTU anataka kugida bia 5. Starehe!
 
Hata mie ni muhenga lakini naomba uache kudanganya hawa wadogo zetu, enzi hizo si kwamba vyumba vilikaza, tatizo lilikuwa ni ukiritimba wa serikali kufanya biashara (mfano: Maduka ya kijiji, mabasi ya KAMATA, Kampuni za Biashara za Mikoa RTC, RETCO) badala ya kuwaachia wananchi wa kawaida (wafanyabiashara) kufanya baishara; ingawa lengo la Nyerere wakati huo ilikuwa kudhibiti bidhaa za nje na kukuza soko la bidhaa za ndani hivyo lilipelekea upungufu mkubwa wa bidhaa na kupelekea watu kupanga foleni na kuuziwa kiwango fulani tu zaidi yake unakuwa mhujumu uchumi.

Wananchi wa enzi hizo akiwamo baba yangu hawakuwa na shida na pesa (vyuma havikuwa vimekaza) kwani alikuwa mkulima wa pamba na mfugaji mkubwa hivyo kwetu shida ilikuwa upatikanaji wa bidhaa za mahitaji mbalimbali kuwa adimu. Hali ya sasa ni kwamba kuna kila kitu ila watu tunaishia kufanya 'window shopping' kwa kuwa hali ni ngumu sana pesa hakuna.

Hivyo tofautisha enzi tunavaa kamanyola/kaunguza tukiwa hatuna option ingine wakati sasa hivi utavaa chochote ukitakacho muhimu una pesa ya kununulia.
 
Unajua nimekuja kuhitimisha kuwa sisi Watanzania tuko ‘soft’ sana, hususan nyakati hizi.

Unakuta mtu ana likitambi lake likubwa tu halafu eti analalamika vyuma vimekaza.

Watu wanakula bata kila kona huku wanalalamika vyuma vimekaza.

Wakati mwingine huwa nikiwaangalia naishia kucheka na kuwaambia ‘mnacheza nyie’.

Wahenga wenzangu watakubaliana nami kuwa kuna kipindi nchi hii vyuma vilikaza kweli kweli.

Enzi za miaka ya 80, hususan mwanzoni hadi katikati.

Enzi za maduka ya ugawaji. Watu mnajipanga mstari kusubiri kununua bidhaa kama sukari, unga, mafuta, mchele, miche ya sabuni, na vitu vinginevyo.

Bidhaa hizo za kila siku zilikuwa adimu. Sabuni za kuogea kama vile Imperial Lather na Palmolive zilikuwa hazipatikani kirahisi nchini. Kuzipata ilibidi mtu aende nje ya nchi kama Kenya au Ulaya huko. Watu tulikuwa tunaogea sabuni za Mbuni. Sabuni hiyo hiyo unaoshea vyombo, hiyo hiyo unaogea na hiyo hiyo unafulia nguo.

Hata dawa za mswaki zilikuwa adimu. Kunywa hata soda lilikuwa ni jambo la anasa. Watu mnaweza kupitisha hata miezi sita hamjanywa soda. Hata kula mkate wa siha ilikuwa nadra.

Kula pilau nako hivyo hivyo. Kula kuku pia.

Kunywa bia ndo kabisa! Kukaza huko kwa vyuma kulifanya pombe za kienyeji zipande chati, hususan wanzuki na kangala.

Sasa leo nikiona hivi vitoto vya miaka ya 90 vikijiliza liza eti vyuma vimekaza huku majumbani kwao kuna DSTV, maduka yamejaa kila aina ya bidhaa, vikienda baa vinakunywa Smirnoff, Savanna nini sijui, Hennessy V nini sijui, vinavaa nguo za madizaina [hata kama ni feki], yaani starehe mwanzo mwisho!

Nikiona hivyo huwa najiuliza sana...kama sasa hivi vyuma vimekaza...enzi zile vilikuwa vimefanya nini sasa!

Nani humu kaenda dukani akakosa Colgate, kwa mfano?

Nani hajanywa soda mwaka mzima? Nani hajanywa Fursana au Mo Orange kisa kashindwa kununua kwa sababu vyuma vimekaza?

Nani kaenda dukani kununua Rinju akakosa?

Tumekuwa watu walaini mno sisi. Watu wa kudekadeka tu.

Vyuma vilikaza miaka hiyo. Hakuna vyuma vilivyokaza miaka hii.

Acheni usleki mayai.

chief nakuhesabia! hili ni bandiko la kumi ndani ya siku nne seems like unatafuta attention au stress za credit card zinakupeleka mbio?
 
chief nakuhesabia! hili ni bandiko la kumi ndani ya siku nne seems like unatafuta attention au stress za credit card zinakupeleka mbio?

Natafuta ukuu wa wilaya.
 
Sasa hapa umeandika nini? Hakika wewe ni mjinga. Tangia lini maendeleo yakalinganishwa na vitu vya zamani, uchumi wa millenium unaupima na wa karne ya 20? Unalinganisha hali ya maisha ya miaka 1980's na 2010's? Hahahahahaha aki wewe ni mwehu... Maendeleo na ustawi wa jamii wa leo vilikua havizuiliki, kupanda juu ni nature ya wanadamu ni dynamic hao.... Kwaio ulikua unataka kusema nini sasa watu wasilalamikie hali mbaya ya uchumi kwakua hata zamani ilikua ni mbaya zaidi? Hahahahahahaha alaf unajiaibisha ujue, kila saa una post ujinga kuitetea serikali nawe ukitaka ukumbukwe au wakujue.
 
Kweli kabisa watu walikua wanatafuta majani yakitoa povu tu wanafulia,hivi sasa wengi baba zao ndio walioangusha mashirika wanawakejeli wabongo kujidai wazalendo!

Sasa kama hayo mashirika yalikuepo na bado watu mkawa mnafulia majani ya mipapai hata ya kifa kuna hasara gani? Mbona yalishindwa kuwasaidia lolote wakati ule?
 
Nayo ni hoja hiyo? aisee wamarekan walioishi maisha ya mwaka 1777 ni sawa na wa sasa?
Hahahahaha na jamaa akasisitiza kwa mara ya kwanza kacomment sababu jamaa kaongea points sanaa hahahahaha, kama ndio hivi huyu hapaswi kucomment chochote tena maishani.
 
Unajua nimekuja kuhitimisha kuwa sisi Watanzania tuko ‘soft’ sana, hususan nyakati hizi.

Unakuta mtu ana likitambi lake likubwa tu halafu eti analalamika vyuma vimekaza.

Watu wanakula bata kila kona huku wanalalamika vyuma vimekaza.

Wakati mwingine huwa nikiwaangalia naishia kucheka na kuwaambia ‘mnacheza nyie’.

Wahenga wenzangu watakubaliana nami kuwa kuna kipindi nchi hii vyuma vilikaza kweli kweli.

Enzi za miaka ya 80, hususan mwanzoni hadi katikati.

Enzi za maduka ya ugawaji. Watu mnajipanga mstari kusubiri kununua bidhaa kama sukari, unga, mafuta, mchele, miche ya sabuni, na vitu vinginevyo.

Bidhaa hizo za kila siku zilikuwa adimu. Sabuni za kuogea kama vile Imperial Lather na Palmolive zilikuwa hazipatikani kirahisi nchini. Kuzipata ilibidi mtu aende nje ya nchi kama Kenya au Ulaya huko. Watu tulikuwa tunaogea sabuni za Mbuni. Sabuni hiyo hiyo unaoshea vyombo, hiyo hiyo unaogea na hiyo hiyo unafulia nguo.

Hata dawa za mswaki zilikuwa adimu. Kunywa hata soda lilikuwa ni jambo la anasa. Watu mnaweza kupitisha hata miezi sita hamjanywa soda. Hata kula mkate wa siha ilikuwa nadra.

Kula pilau nako hivyo hivyo. Kula kuku pia.

Kunywa bia ndo kabisa! Kukaza huko kwa vyuma kulifanya pombe za kienyeji zipande chati, hususan wanzuki na kangala.

Sasa leo nikiona hivi vitoto vya miaka ya 90 vikijiliza liza eti vyuma vimekaza huku majumbani kwao kuna DSTV, maduka yamejaa kila aina ya bidhaa, vikienda baa vinakunywa Smirnoff, Savanna nini sijui, Hennessy V nini sijui, vinavaa nguo za madizaina [hata kama ni feki], yaani starehe mwanzo mwisho!

Nikiona hivyo huwa najiuliza sana...kama sasa hivi vyuma vimekaza...enzi zile vilikuwa vimefanya nini sasa!

Nani humu kaenda dukani akakosa Colgate, kwa mfano?

Nani hajanywa soda mwaka mzima? Nani hajanywa Fursana au Mo Orange kisa kashindwa kununua kwa sababu vyuma vimekaza?

Nani kaenda dukani kununua Rinju akakosa?

Tumekuwa watu walaini mno sisi. Watu wa kudekadeka tu.

Vyuma vilikaza miaka hiyo. Hakuna vyuma vilivyokaza miaka hii.

Acheni usleki mayai.
Huu uzi braza The List ameuona lakini?
 
Maisha yapo kawaida tuu...

Enzi unazozungumzia nadhani ni baada au kipindi cha vita ya kagera, kama sijakosea... ndiyo nchi ilifunga mkanda na vyuma kukazika kisawa sawa...

Wanaolalamika vyuma kukaza bado hawajaona maana halisi ya vyuma kukaza, waache sasa wafanye haya maandamano wanayotaka kufanya alafu waone vyuma vitakavyokaza...

cc: mahondaw
guilty are afraid
 
mkuu naona mabandiko yako, unajitahidi kutumia nguvu kubwa sana kudhihirisha serikali ya ccm chini ya raisi JPM mambo yako poa tu ajira zipo, maisha hayana gharama, uhuru wa maoni upo, demokrasia ipo, yaani kila kitu kipo, sera za ccm zinatimizwa zote tena kwa wakati n.k.

inahitaji kujitoa akili ili mtu usome na kuelewa unachokipigania hivi karibuni kupitia sredi zako uchwara zenye ukakasi mwingi... kama wewe unapata milo mitatu kwa siku na ukakula hizo unazoziita bata sio wote wako hivo...
mkuu hii mijitu n bogus kbs
 
Kipindi hicho viuma vilikuwa na full greese shida ilikuwa bidhaa maduka hayakuwepo kila bidhaa kwenye maduka ya ujamaa soda unapanga mstari kupata sasa bidhaa zipo madukani shida ni pesa ya kufanyia manunuzi
 
Sahihi kabisa mkuu! Eti jitu linakuja kulinganisha enzi hizo na sasa!
 
Huwezi kulazimisha mtu alinganishe maisha yaliyopita ambayo hata hakuwa amezaliwa na miaka ambayo alikuwa amezaliwa utakuwa unamwonea tu.....na pia lazima ufahamu nyakati zinaenda na mabadiliko yake pia kwa hivyo comparison inapaswa kufanywa kwa kuzingatia hilo pia...
Usiliazimishe watu watembee kwa miguu katika kipindi ambachp techonolijia ya usafiri ni kubwa kulinganisha na huko ulikotoka.

Usilazimishe watu wayaone maisha yao ni afadhali kwa experience ta maisha yako...
 
Back
Top Bottom