Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 15,327
- 24,208
Vyombo vyetu vya Ulinzi na Usalama kwa miaka mingi vimesifika kwa weledi na umahiri wa kiutendaji.
Na ndio maana Operations zake mara zote huwa zinaendeshwa na Intellijesia ya uhakika.
Wazungu wanaita sound intelligence.
Hivi vyombo vyetu ni zao la wananchi wenyewe hivyo kuaminika kwao na jamii ni jambo la lazima, na si ombi.
Vyombo hivi vina wafanyakazi wenye akili timamu na wenye ujuzi na weledi.
Matukio ya miaka ya hivi karibuni imeanza kutia shaka weledi uliojengwa kwa miaka mingi .
Stage managing events ni suala linalotakiwa ujuzi na weledi usiota shaka.
Vyombo vyetu inabidi vikatae katakata kujiingiza kwenye operations zisizo na tija wala manufaa yanayoonekana kwa Taifa.
Suala la kutekwa kwa Mo Dewji limeibua sura mbaya, sura isiyoeleweka na inayoitia aibu nchi kupitia vyombo vyetu vya ulinzi na usalama.
Matukio yasiyo na maelezo yanayotosheleza yanazidi kuongezeka, kutekwa kwa Roma, jaribio la mauaji ya Lissu na mengine.
Vyombo vyetu tunawaamini sana, tusijiweke mkao wa kuvuna dharau ya wananchi.