Vyombo vya ulinzi na usalama hawana sababu ya kuchelewa kutekeleza yaliyomo katika ripoti waliopewa na Rais Magufuli

shige2

JF-Expert Member
Oct 11, 2016
8,106
3,967
Wana JF.
Ripoti mbili zinazohusu migodi ya ALMASI na TANZANITE iliyoandikwa na pande zote bungeni (Bipartisan) na kukabidhiwa rais Magufuli Ikulu leo ni ripoti INAYOSIKITISHA na KUUDHI sana.

Hasa kuona WATUMISHI waliopewa DHAMANA ya KULINDA raslimali yetu wao waligeuka KUJITAJIRISHA na hivyo kuwa COMPROMISED na WAWEKEZAJI ili MALI ipite wao wapate PESA tu.

Kila mtu AKIANGALIA PEMBENI miaka hii yote huku tukizidi KUKIIBIWA na watu WANAOJULIKANA ambayo ripoti IMEWATAJA!

KITENDO cha rais KUVIKABIDHI ripoti hii vyombo vya ULINZI na USALAMA ni kitendo cha kupongezwa.

Hapo WANANCHI watajua ni CHOMBO gani KIMECHUKUWA hatua ZIPI kwa HUSIKA na UTEKELEZAJI.Na kulionyesha TAIFA na RAIS nani na nani ni WATEKELEZAJI.

Hivyo basi vyobo hivi HAVINA SABABU ya KUZEMBEA maana USHAHIDI uko TELE. Kama wananchi chombo kama PCCB( TAKUKURU) Kinahitajika to move with SPEED in delivering DESIRED RESULTS/ Yaani kwenda kwa KASI katika KUTOA matokeo YANAYOHITAJIKA.

Wananchi TUNASUBIRI kwa hamuUTEKELEZAJI wa ripoti hii.

Hongera kwa Rais John P. Magufuli, Hongereni KAMATI ya BUNGE

Mungu ibariki Tanzania.
 
..Leo hajatumbua ila kaacha mamlaka zinazohusika zichukue hatua
Ametumbua kiutu uzima, mzee. Kusema wale wote waliotajwa na kamati na leo hii wapo serikalini ni bora wajipime na kuondoka ili police wawe huru kuwachunguza ndo utumbuaji wenyewe huo.

Lakini hata kwa report ya Orosso alitoa maagizo ya kwamba wale jamaa wachunguzwe. Sidhani kama Ngereja, Msabaha, Joka kuu lenye kengeza et al waliguswa.
 
Mkuu umesema kweli. Ametumia hekima kubwa sana.
 
Ametumbua kiutu uzima, mzee. Kusema wale wote waliotajwa na kamati na leo hii wapo serikalini ni bora wajipime na kuondoka ili police wawe huru kuwachunguza ndo utumbuaji wenyewe huo.

Lakini hata kwa report ya Orosso alitoa maagizo ya kwamba wale jamaa wachunguzwe. Sidhani kama Ngereja, Msabaha, Joka kuu lenye kengeza et al waliguswa.
Bila kusahau kuwa alipokuwa akizungumza. Alizungumza kwa MAFUMBO.
Na bila kusahau kuwa mzigo mkubwa AMEWABEBESHA vyombo HUSIKA AONE how FAR these fellows could ACT/Ni namna gani na UHARAKA upi watafanyia kazi ripoti hiyo.
Wale watakaokuwa WAVIVU KUISOMA ripoti na kuifanyia kazi. MLANGO wa kutoka nje UKO.
 
Leo hekima na busara imetumika majipu yatajitumbua yenyewe si mnaona simba mwenyewe....tummbu
 
Post kama hizi hatuna muda nazo. Tundu lisu ndyo habar ya mjini.

‍♂️naenda zimbobo.
 
Leo hekima na busara imetumika majipu yatajitumbua yenyewe si mnaona simba mwenyewe....tummbu
Nakuunga mkono. WENYEWE kuanzia sasa kufikia Juma lijalo nahisi kuna watu WATAJITUMBUA wenyewe. Hasa vyombo husika vitakaposhika KASI.
 
nchi hii itaendelea kila chombo na muhimili ukisimamia ukifanya kazi kwa kufanikisha haya yalliyoanzishwa na mkuu.
excuse za ushahidi sijui hautoshi hazina nafasi, watatukatisha tamaa wananchi.
 
Post kama hizi hatuna muda nazo. Tundu lisu ndyo habar ya mjini.

‍♂️naenda zimbobo.
Nakuelewa mkuu. Hata mimi NALAANI yeyote ALIYEHUSIKA katika UNYAMA huo ili kuliweka taifa letu katika hali ambayo si ya Watanzania.

Hata kama yuko upinzani. Ni makosa na nahisi ni WAHALIFU ambao mkono wa sheria UTAWAPATA. Mimi mwenyewe natakia quick recovery.
Pamoja na hayo mambo ya UCHUMI wetu KUHUJUMIWA si jambo dogo pia mkuu.
 
nchi hii itaendelea kila chombo na muhimili ukisimamia ukifanya kazi kwa kufanikisha haya yalliyoanzishwa na mkuu.
excuse za ushahidi sijui hautoshi hazina nafasi, watatukatisha tamaa wananchi.
Mkuu, Nakuunga mkono 100%. Ili kila chombo kisimamie mahali pake na MATOKEO yaonekane.
Katika mtazamo wangu Mh. Dr John P. Magufuli alikuwa AKIGAWA MITIHANI kwa WATAHINIWA.

Ili watakaofaulu ndo ATAFANYA kazi nao. WATAKAOFELI waende nyumbani. Kando ya wengine waliotajwa KUJITUMBUA wao wenyewe.
Mzee hataki mchezo. Hasa ukizingatia misemo ya KIMAFUMBO aliyoitumia.
 
Back
Top Bottom