Vyeti feki vyazua kizaazaa

Vyeti feki vyazua kizaazaa

Wakalime tu hakuna namna
IMG_20170503_195723.jpg
 
Nchi hii inatia hasira sana kwa kweli. Mtu anaitumikia nchi hadi anakaribia kustaafu anaambiwa ni mtumishi hewa. So sad.
Sio HEWA.
Amegushi CHETI
 
sasa hao madereva siwangeenda kusoma QT,
Kubweteka eddy
Wapo wengi sana walibweteka.Hao madereva walikua wakipata hela kuliko degree holders,mambo ya Per Diem,mambo ya over time.So usome ili iweje while UNA PESA
 
Unamquote sana Mwinyi wakati kama utaitendea haki akili yako utagundua katika kipindi cha uongozi wake ilikuwa ni afadhali ya gari bovu.
Ukiniuliza katika Marais wote walioongoza nchi hii ni nani aliyekuwa mbovu kuliko wote nitakujibu bila kupepesa macho kuwa ni MWINYI. Serikali yake iliongoza katika ukwepaji kodi, ndicho kipindi ambacho akina Guramali, Dewiji walikuwa wakiwaahidi wachezaji kuwa mkiifunga Yanga/Simba kila mchezaji akachukue gari ya kutembelea. Mkapa ndiye aliyeiokoa nchi hii kutumbukia shimoni. Alirejesha heshima ya serikali na wafanyakazi, watu tukaanza kuheshimiana kwa mafanikio yanayotokana na juhudi na sio madili (ingawa naye Mkapa mwishoni wapiga madili - Mramba, Yona - walimuingiza mjini)
JK he was weak - hili hata John Myika anajua, mzee wa matanuzi, safari kila kukicha, lakini he did far better than Mwinyi although again worse than Mkapa.
JPM is doing his best. Ni Rais ambaye dhamira yake haina shaka hata chembe. He is determined kuona nchi inarudi kwenye msitari. AMESHATENDA ambayo mengine leo yanatushangaza. Watu waliokuwa wakiishi kifekifeki, kimadilimadili wanapata shida kwelikweli.
Wasubiri tu! labda 2025 CHADEMA ikifanikiwa kumuweka LOWASA madili yao atawarudishia. Lakini kwa sasa HAPA KAZI TU! hakuna ufekifeki serikalini. IMETOSHA! JPM kaza kamba turudi kwenye mstari.
Hakuna ufeki feki serikalini kuanzia lini? Bashite ni shambaboy? Huwezi kusema kuna dhamira safi kama kuna double standard! Huwezi kusema hakuna ufeki feki serikalini wakati serikali imejaza wakurugenzi wa halmashauri na madas feki eti tu kwa kuwa ni makada wa chama chetu! Na aibu inayowasubiri ni kwamba wale watu mliodai mlikesha mkiwafanyia vetting nao ni feki! Mmegundua aibu inayokuja kuwapata mmeanza kusema hao sio watumishi wa umma. Hovyo kabisa!
 
Alishajibu Hilo Mwinyi Tatizo lako hufuatilii!

Azimio la Arusha kilikuwa ni Paper Tiger halikuwa linatekelezeka!

Azimio la Arusha halikufanikiwa hata kitu kimoja cha Kiuchumi zaid ya kupora Wahindi na Wazungu, Viwanda, Mashamba Viwanja na Majumba



Bila ya kufa kwa Azimio la Arusha Mfumo wa Vyama vingi ulikuwa hautekelezeki

Azimio la Arusha Msingi wake ulikuwa Siasa na Uchumi wa Ujamaa lakin Kwa Miaka yote hiyo ya Azimio 1967-1992 Tanzania haikuwahi kujitegemea hata kwa Sekunde Mbili lakin Wimbo wa kujitegemea tuliendelea kuimba!

Takwimu za World Bank zinasema Watanzania wameanza kuficha Fedha Uswizi 1974 jee Azimio la Arusha halikuwepo?

Operation Uhujumu Uchumi ilikuwa kusaka Wahujumu Uchumi 1983 jee hao Wahujumu Uchumi waliletwa na Azimio la Znz?

Hapo ulipo nikikuuliza chochote kuhus Azimio la znz hujui kitu zaid ya kukariri kuwa Azimio la Arusha lilifutwa!

Azimio la Znz ndio liliachana na Mfumo wa Kijamaa ambao hata hao tuliowaiga China wameachana nao

Azimio la znz ndio limeruhusu uwepo wa Mfumo wa Vyama vingi

Azimio la Arusha lilinyang'anya Watu Mali zao na ndio ukawa mwanzo wa Watanzania kujifaharisha kwa Umaskini kuwa ndio Kigezo cha uadilifu na uchapakazi na utajiri ni dhambi ya kuepukwa!
Aisee wewe mtu uko safi!! Hukuhama ccm kwa bahati mbaya! Unajielewa haswa!
 
Yan sasa nafikiria kwa namna yoyote ingetokea msako mpaka private sector daa Tanzania tunaweza fikiri watu wamesoma kumbe hakuna kitu waliosoma na walio kwenye positions kwa haki ni wachache mnooo
 
Miiko ya Azimio la Arusha ilikuwa Mizuri sana kuizungumza kwny Mijadala lakini ilikuwa hautekelezeki hata kidogo hasa kwny Modern World( Pitia features za utopian Socialism) utanielewa!


Baadhi ya Miiko ya Azimio la Arusha Leo hii ingeweza kwenda kuwa challenged Mahakamani kwa kuwa Ina element ya Ubaguzi wa kiuchumi kuwabagua Wafanyabiashara ntakupa Mfano!

Azimio la Arusha lilipiga Marufuku Kiongozi wa Chama na Serikal kufanya Biashara ya aina yeyote na likasisitiza kabisa hairuhusiwi Kiongozi kumiliki Nyumba ya kupangisha

Jee Kama Mtumishi wa Umma ni Marufuku kuwa Mwanasiasa na hapo hapo Mfanyabiashara pia ni Marufuku sasa Huyo Mwanasiasa angekuwa na shughuli ipi ya kuingiza Kipato zaid ya Siasa yenyewe ?

Lazima tujue kuwa Azimio la Arusha lilitengenezwa kwa ajili ya Mfumo wa Chama Kimoja na Ndio sababu lilifanya kazi ki Chama zaid kuliko ki Serikal Ndio sababu kina Mwinyi na kina Comrade Ibrahim Kaduma wakaona haiwezekani kuruhusu Mfumo wa Vyama vingi bila kuhuisha Azimio ( Harmonisation)



Isingewezkana kushinikiza Vyama vya Upinzani kuendeshwa kwa Mfumo wa Azimio la TANU hata Siku Moja


Tusisahau kuwa Nyerere alikuwa Binadamu na Mwanasiasa hivyo sio kila neno lake ni Sheria

Aliwahi kunukuliwa akisema (1995) kuwa kwake yeye anaona Azimio la Arusha halifai kurekebishwa hata Alama ya koma kwenye lile andiko wakati Alijua kabisa hata Katiba Yenyewe ya Jamhuri ilibidi ifanyiwe Marekebisho ili kukidhi uanzishwaji wa Vyama vingi iweje Azimio libaki vile vile

Vipi kuhusu mchango wa Azimio la Zanzbar kwenye UFISADI wa viongozi wetu. Je si kweli kwamba Azimio la Zanzbar lilitoa mwanya kwa viongozi walafi kuanza UFISADI? Je si kweli kwamba Azimio la Zanzbar lilipaswa kuja baada ya kuweka some sort of speed governors kwa viongozi ambao walikuwa na mamlaka makubwa na fursa za kutupora?
 
Vipi kuhusu mchango wa Azimio la Zanzbar kwenye UFISADI wa viongozi wetu. Je si kweli kwamba Azimio la Zanzbar lilitoa mwanya kwa viongozi walafi kuanza UFISADI? Je si kweli kwamba Azimio la Zanzbar lilipaswa kuja baada ya kuweka some sort of speed governors kwa viongozi ambao walikuwa na mamlaka makubwa na fursa za kutupora?

Ndugu yangu Wewe ni Great thinker tazama jambo kwa Jicho Hilo!

Azimio ni Sera sio Sheria!

Naona unachanganya Kati ya Nguvu ya Katiba na mambo ya Azimio!

Umewahi kujiuliza kwanini Nyerere hakuliingiza Azimio la Arusha la 1967 kwny Katiba ya 1977?

Mambo ya Azimio ni Mambo ya kichama baada ya Mfumo wa Vyama vingi Guideline yetu ni Katiba sio Tena Azimio.


Usitumie nguvu kubwa kutafuta udhaifu wa Azimio la znz jaribu kuwaza kwa Mazingira ya Sasa na Wewe una Mawazo Kama ya Nyerere kuwa Azimio la Arusha halikupaswa kubadilishwa hata koma?,

nimejaribu kukuelezea sababu za Msingi za kuletwa Azimio la znz nilitegema uzi challenge hizo sababu kwanza Kama ni valid or not !

Azimio la Arusha katika kudhibiti Ufisadi lilipiga Marufuku Kiongozi wa Umma kumiliki Nyumba zaid ya Moja, kupangisha Wapangaji na asiwe Mfanyabiashara, jee unataka hiyo Miiko irudishwe Leo kudhibiti Ufisadi ?
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Ajira ni ajira tu hata kama ni kwa miaka 2 au miezi 6, hawa hawa wanakuja kwenda polisi na JWTZ.
Lkn unajua kwamba kabla ya kwenda kwenye hivyo vyombo unavyovitaja huwa wanafanyiwa usaili upya wa vyeti na kupelekwa baraza la mitihani?
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Mbona hutaki uhakiki ufike huko au una ndugu nini kapungukiwa cheti?
Nakufahamisha kitu ambacho na hakika hukijui, sikukataa hivyo vyombo kuhakikiwa, ila unavyosema JKT, hao hawaja ajiriwa bado wapo kwenye mchakato wa kutafuta ajira kwenye vyombo vya ulinzi na usalama.sasa watawahakiki nini? Ikiwa payroll haiwatambui?
 
Ukimwambia mtu aliyekua anazunguka na jua bila nauli na degree yake ya kweli mkononi mpaka kwenda kuomba kazi ya bar hatakuelewa. Mimi siwaonei huruma kabisa walijisahau sana na watu kama hao walipokua na wadhifa waliwanyanyasa sana wasomi wa kweli.

Magufuli Moto chini nawaonea huruma wale tu ambao wameonewa kwa makosa ya wahakiki.
 
Nakufahamisha kitu ambacho na hakika hukijui, sikukataa hivyo vyombo kuhakikiwa, ila unavyosema JKT, hao hawaja ajiriwa bado wapo kwenye mchakato wa kutafuta ajira kwenye vyombo vya ulinzi na usalama.sasa watawahakiki nini? Ikiwa payroll haiwatambui?
Haya
 
Ukimwambia mtu aliyekua anazunguka na jua bila nauli na degree yake ya kweli mkononi mpaka kwenda kuomba kazi ya bar hatakuelewa. Mimi siwaonei huruma kabisa walijisahau sana na watu kama hao walipokua na wadhifa waliwanyanyasa sana wasomi wa kweli.

Magufuli Moto chini nawaonea huruma wale tu ambao wameonewa kwa makosa ya wahakiki.
Awape pension zao.
 
Back
Top Bottom