Vyeti feki vyazua kizaazaa

Vyeti feki vyazua kizaazaa

Mungu hawezi kushusha dikteta mwenye kudharau taratibu na sheria mbali mbali za nchi ambaye pia ni muongo fisadi na mnyanyasaji. Acha kujibaraguza.


Dua la kuku haliwezi kumpata mwewe ndugu yangu. mimi ninapenda style ya Magufuli nadhani ni fundisho kwa wajinga kama kina Marando na wenzake waliochezea shilingi chooni mwaka 1995 kwa kukimbilia Ikulu. Magu tufundishe adabu.
 
Awape pension zao.
Sheria inasema ukipata mali kwa njia ya halifu unanyang'anywa mali. uza unga halafu ukikamatwa uone moto wake wanachukua mpaka nyumba ulizojenga. Hili ni kosa la jinai lakini watu tunachukulia utani utani sababu ya watu kama hawa wanasiasa uchwara kujifanya kuwaunga mkono wahalifu.
 
Sheria inasema ukipata mali kwa njia ya halifu unanyang'anywa mali. uza unga halafu ukikamatwa uone moto wake wanachukua mpaka nyumba ulizojenga. Hili ni kosa la jinai lakini watu tunachukulia utani utani sababu ya watu kama hawa wanasiasa uchwara kujifanya kuwaunga mkono wahalifu.
Kufoji Bashite ni sahihi lakini wengine hapana?
 
SERIKALI YASHUSHA PRESHA VYETI FEKI


*Yawataka walioonewa wakate rufaa, yatafakari mafao

*Ajira za dharura mbioni kutangazwa kuziba nafasi

vyeti-feki-300x200.jpg


Na MAREGESI PAUL-DODOMA

SERIKALI, imesema watumishi wa umma walioorodheshwa kwenye orodha ya watumishi wa umma wenye vyeti feki, wakati hawakutakiwa kuwekwa, wakate rufaa.

Kauli hiyo, ilitolewa jana mjini hapa na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dk. Laurean Ndumbaro, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

“Kama mtakumbuka, uhakiki wa vyeti feki kwa watumishi wa umma, ulihusisha vyeti vya kidato cha nne, kidato cha sita, ualimu na taaluma zingine.

“Baada ya uhakiki huo, iliagizwa watumishi 9,932 waliokuwa na vyeti feki, waondolewe katika ajira, watumishi 1,538 wenye vyeti vyenye utata kwa maana kwamba vinatumiwa na watu zaidi ya mmoja, wathibitishe vyeti vyao kabla ya Mei 15 mwaka huu na mishahara yao isimamishwe hadi uhakiki utakapokamilika.

“Wale watumishi 11,596 waliogundulika kuwa na vyeti pungufu, wanatakiwa kuwasilisha vyeti vyao vikaguliwe kabla ya Mei 15, mwaka huu, vinginevyo watachukuliwa hatua.

“Lakini, wale wanaodai kwamba wamewekwa kwenye orodha ya wenye vyeti feki wakati hawakutakiwa kuwa huko, tunawaomba waandike barua za kukata rufaa kwa Katibu Mkuu Utumishi kupitia kwa waajiri wao.

“Waajiri hao, watatakiwa kuwasilisha vyeti hivyo Baraza la Mitihani la Taifa kwa ajili ya uhakiki zaidi kabla ya Mei 15, mwaka huu.

“Pamoja na hayo, ieleweke kwamba, baadhi ya watumishi wakati wanaajiriwa, waliwasilisha vyeti vya matokeo mengine ya sekondari na wakati wa uhakiki, walionyesha vyeti vingine.

“Lakini, naomba ieleweke kwamba, hakuna mtumishi wa umma mwenye cheti halali atakayeondolewa katika utumishi wa umma.

“Kuhusu suala la mafao ya watumishi hao, hilo tunaliangalia namna ya kulifanya kwa sababu kuna sheria zinazolisimamia,” alisema Dk. Ndumbaro.

Ajira za dharura

Pamoja na hali hiyo, Dk. Ndumbaro aliwataka wakuu wa idara ambazo huduma zake zimeathiriwa na zoezi la vyeti feki baada ya watumishi kuacha kazi kwa kuwataka kuandika barua kwake ili zitangazwe nafasi za ajira za dharura kwa lengo la kuziba mapengo hayo.

Akizungumzia wizara ambazo taarifa za uhakiki wake hazikutolewa hivi karibuni, alisema zitatolewa Mei 10 mwaka huu baada ya uhakiki wake kukamilika.

Katika hatua nyingine, Dk. Ndumbaro alisema Serikali itaajiri watumishi 1,500 kuanzia sasa hadi mwisho wa Bunge la Bajeti linaloendelea mjini hapa.

Kwa mujibu wa Dk. Ndumbaro, ajira hizo zimetolewa ili kukabiliana na uhaba wa watumishi wa umma ulioko katika sekta mbalimbali serikalini.


“Katika hili, waajiri watatakiwa kuhakiki vyeti vya waombaji wote kabla hawajaajiriwa ili kuepuka uwepo wa watumishi wengine wenye vyeti feki,” aliagiza.

Wakati Dk. Ndumbaro akisema hayo, awali Mbunge wa Viti Maalum, Rhoda Kunchele (Chadema), aliliambia Bunge, kwamba watumishi wanne wa umma wamelazwa mkoani Katavi, baada ya majina yao kuonekana katika orodha ya watumishi wenye vyeti feki.

Kutokana na hali hiyo, alitaka Serikali iliangalia suala hilo kwa kina kwa kuwa baadhi ya watumishi waliowekwa katika orodha hiyo, wanadaiwa kuwa na elimu ya sekondari wakati hawajawahi kusoma.

Ripoti ya uhakiki wa watumishi wa umma nchini ilikabidhiwa wiki iliyopita na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki kwa Rais Dk. John Magufuli.

Ripoti hiyo inaonyesha kuwa watumishi 9,732 wamebainika kuwa na vyeti feki.

Rais Magufuli aliagiza watumishi hao wakatwe mshahara wa mwezi uliopita na pia wafukuzwe kazi na watakaoendelea kubaki kazini hadi Mei 15 wakamatwe na kuchukuliwa hatua za kisheria ikiwamo kufungwa jela miaka saba.
 
Yan sasa nafikiria kwa namna yoyote ingetokea msako mpaka private sector daa Tanzania tunaweza fikiri watu wamesoma kumbe hakuna kitu waliosoma na walio kwenye positions kwa haki ni wachache mnooo
Utagundua wasomi wako mtaani.. watu ambao hawakustahili kuwa kazini ndio wako kazin
 
WATUMISHI 6 JELA KWA VYETI FEKI



*DAS naye atajwa katika orodha ya walioghushi

*Zahanati mbili zafungwa kwa kukosa wahudumu

kairuki-300x225.jpg


Maregesi Paul-Dodoma na ALLY BADI- KILWA



UAMUZI wa Serikali wa kuwafukuza kazi watumishi wanaodaiwa kughushi vyeti, umezidi kuchukua sura mpya, baada ya watumishi sita wa Halmashauri ya Kilwa mkoani Lindi kufungwa jela mwaka mmoja kila mmoja kwa kosa la kughushi vyeti vya kidato cha nne na kujipatia ajira.

Taarifa nyingine zinasema Katibu Tawala wa Wilaya ya Tandahimba (DAS), Mohamed Azizi naye ameguswa na sakata la vyeti feki baada ya kutajwa katika orodha ya watumishi wenye vyeti feki akiwa namba 5356.

Chanzo cha uhakika kutoka ofisi ya DAS kimelidokeza MTANZANIA kuwa, tayari kiongozi huyo ameshaondoka Mtwara kuelekea Dar es Salaam kupeleka malalamiko yake katika mamlaka za juu kwamba jina lake limeingizwa kimakosa katika orodha hiyo.

Taarifa nyingine kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Lindi Vijijini zinasema zahanati mbili zimefungwa baada ya watumishi wote waliokuwapo kukumbwa na sakata la vyeti feki.

MADEREVA

Madereva hao, walihukumiwa jana na Mahakama ya Wilaya ya Kilwa, baada ya kupatikana na hatia ya makosa matatu ya kufoji vyeti vya kidato cha nne.

Hukumu hiyo, imetolewa na Hakimu wa Mahakama hiyo, Gabriel Ngaeje baada ya kuridhishwa na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka.

Madereva waliohukumiwa ni Juma Sungura, Issa Juma Abdurahamani, Abdull Chubi, Dactuce, Ahamadi Selemani na Abdallah Kilolopera.

Kabla ya kutolewa hukumu hiyo, Hakimu Ngaeje aliwauliza washtakiwa kama wana sababu zitakazoishawishi mahakama isiwape adhabu kali.

Kila mmoja kwa wakati wake, aliomba mahakama iwaonee huruma, kwani wana familia zinazowategemea, hivyo iwapo watapewa adhabu kali kuna hatari ya kukosa matunzo yao.

Naye mwanasheria wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Emmanuel Camilius aliiomba mahakama kutoa adhabu kali ili iwe fundisho kwa watuhumiwa na watu wengine wenye tabia ya aina hiyo ndani ya Mkoa wa Lindi na Taifa kwa ujumla.

“Tabia ya aina hii si ya kuifumbia macho, kazi wanazozifanya zinahusu usalama wa watu, kugushi vyeti kwa ajili ya kujipatia ajira ni hatari,”alisema Camulius.

Hakimu Ngaeje, akitoa hukumu katika kesi hiyo namba 07/2014, alisema amesikiliza maombi ya pande zote mbili, hivyo akawahukumu kila mmoja kifungo cha nje cha miezi (12) kwa kila kosa na kufanya idadi ya miezi (196).

“Kwa vile adhabu inakwenda pamoja, mtatumikia kifungo cha nje miezi 12,”alisema.

Awali ilidaiwa mahakamani hapo na mwanasheria Camilius, kuwa watumishi hao wakijua wanachokifanya ni makosa, walifoji vyeti vya kidato cha nne na kujipatia ajira kinyume na sheria ya nchi.

DODOMA

Naye Mbunge wa Mchinga, Hamidu Bobali (CUF), alisema zahanati mbili katika Halmashauri ya Wilaya ya Lindi Vijijini mkoani Lindi, zimefungwa baada ya watumishi wake kutajwa katika orodha ya watumishi wa umma wenye vyeti feki.

Bobali alitoa taarifa hiyo bungeni mjini Dodoma jana, alipokuwa akichangia bajeti ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, kwa mwaka wa fedha 2017/18.

“Mheshimiwa mwenyekiti, hili suala la vyeti feki limeleta shida katika Halmashauri ya Wilaya ya Lindi Vijijini kwa sababu kuna zahanati mbili zimefungwa, baada ya watumishi wake wote kubainika wana vyeti feki.

“Kwa hiyo, namwomba mheshimiwa waziri, achukue hatua haraka,” alisema Bobali wakati alipokuwa akihitimisha mchango wake.

Pamoja na kusema hayo bungeni, Bobali aliiambia MTANZANIA nje ya Bunge, kwamba zahanati zilizofungwa ziko katika Jimbo la Mtama katika Halmashauri ya Wilaya ya Lindi Vijijini.

“Zahanati zilizofungwa ni za Mkanga 2 na Sudi ambazo zote ziko pembezoni kabisa ya mji, kiasi kwamba kitendo cha kuzifunga, kitaathiri mno wananchi.

“Kwa hiyo, ndiyo maana nilimwomba mheshimiwa waziri afanye kila analoweza kuhakikisha zinafunguliwa haraka ili kunusuru maisha ya wananchi,”alisema Bobali.

Kwa mujibu wa Bobali, zahanati hizo zilikuwa na watumishi watatu watatu kila moja.

Taarifa zaidi kutoka Lindi, zinasema watumishi 236 wa Serikali wamegundulika kutumia vyeti feki.

Katika sakata hilo, halmashauri za wilaya za Nachingwea na Kilwa zinaongoza kwa kuwa na idadi kubwa.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi alizitaja wilaya na idaidi ya watumishi kwenye mabano, kuwa ni Nachingwea (72), Kilwa (53), Ruangwa (45),Lindi Vijijini (25), Ofisi ya Katibu Tawala (RAS) (23), Manispaa (11) na Liwale (7).

Alisema katika idadi hiyo, idara za afya na elimu zinaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya watumishi wa vyeti feki.

Hivi karibuni, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angela Kairuki, alimkabidhi Rais Dk. John Magufuli, orodha ya watumishi wa umma wenye vyeti feki.

Hata hivyo, Kairuki alisema katika uhakiki wao, hawakuhusisha wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, wabunge na wanasiasa wengine.

Baada ya uhakiki huo, iliagizwa watumishi 9,932 waliokuwa na vyeti feki, waondolewe katika ajira, watumishi 1,538 wenye vyeti vyenye utata kwa maana kwamba vinatumiwa na watu zaidi ya mmoja, wathibitishe vyeti vyao kabla ya Mei 15 mwaka huu na mishahara yao isimamishwe hadi uhakiki utakapokamilika.

Watumishi wengine 11,596 waliogundulika kuwa na vyeti pungufu, waliagizwa kuwasilisha vyeti vyao vikaguliwe kabla ya Mei 15 mwaka huu, vinginevyo watachukuliwa hatua.

Wakati huo huo, juzi Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dk. Laurean Ndumbaro, aliwataka watumishi wa umma walioorodheshwa kwenye orodha ya watumishi wa umma wenye vyeti feki wakati hawakutakiwa kuwekwa, wakate rufaa.

Dk. Ndumbaro alitoa kauli hiyo wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma.

Pamoja na hayo, Dk. Ndumbaro aliwataka watumishi waliowekwa kwenye orodha hiyo, waandike barua za kukata rufaa kwa Katibu Mkuu Utumishi kupitia kwa waajili wao.

Kwa mujibu wa Dk. Ndumbaro, waajiri hao watatakiwa kuwasilisha vyeti hivyo Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) kwa ajili ya uhakiki zaidi kabla ya Mei 15 mwaka huu.

Pamoja na hayo, alisema hakuna watumishi wa umma wenye vyeti halali watakaoondolewa katika utumishi wa umma na kwamba wakuu wa idara ambazo huduma zake zimeathiriwa na zoezi la vyeti feki baada ya watumishi kuacha kazi, wanatakiwa kuandika barua kwake ili zitangazwe nafasi za ajira za dharura kwa lengo la kuziba mapengo hayo.

Akizungumzia wizara ambazo taarifa za uhakiki wake wa vyeti feki hazikutolewa hivi karibuni, alisema zitatolewa Mei 10 mwaka huu baada ya uhakiki wake kukamilika.

BUTIAMA

Habari zinasema Wilaya ya Butiama, imekumbwa na fagio hilo, baada ya watumishi 40 kutoka sekta mbalimbali kusimamishwa.

Akizungumza na MTANZANIA, jana Mganga Mkuu wa Wilaya ya Butiama, Dk. Getera Nyangi alisema hospitali yake imepoteza watumishi watano.

“Ni kweli wafanyakazi watano wameondolewa kwa suala hili la vyeti..unajua katika kada hii hata akitoa mfanyakazi mmoja ni pengo kubwa,tunajipanga kuona tutazibaje nafasi hizi, naamini mamlaka husika zitatupatia maelekezo,”alisema Dk. Nyangi
 
3.JPG

Kairuki.jpg


angellah-charaz.blogspot.com_.jpg


Angela Kairuki.....Waziri aliyesimamia Zoezi Zito la Vyeti feki....Hatari sana (In Kipozeo Voice)
 
Kumbe tulikuwa wa hovyo kiasi hiki? Ndo maana wengine tunaamini JPM ameshushwa na Mungu kuja kutuweka sawa. TULIKOKUWA TNAPELEKWA NCHI HII SIKO!!!
Ni hatari sana mkuu. Ukitaka maisha kubali kuumia kwanza, kuna waliojifanya ndo wazee wa short cut sasa kumbe hawakujua wanaruka mkojo na kukanyaga mavi
 
Unasema wasomi wako mitaani na wasiosoma wako makazini kakini hiyo ni hoja yako ya kutaka ww ndo upate ajira lakini kauli mbiu ya rais wetu ni kufanya kazi hao unaowatumbua ss hivi lazima wapewe sifa kwani kuna kipindi enzi ya rais awamu ta kwanza aliamua kuajiri walimu wa darasa la saba (7) marufu UPE miaka ya sabini nawalifanya kazi kubwa ambao ss ni mawaziri wetu wa sasa na waliopita walinufaika na walimu hao hivyo msiwadharau hatakidogo, kwa tanzania hii katika ukanda wetu wa afrika mashariki kielimu kidogo tupo nyuma ya wenzetu hili swala la wasomi kusotea ajira wenzetu lipo mda mrefu mfano ktk miaka 80 kuja 90 wenzetu mtu aliyemaliza form iv walikuwa hawana nafasi za ajira labda majeshini wakati huo kwetu form iv alikuwa analinga anachagua kazi ña hali kama hiyo kwa wahitimu wetu wa vyuo vikuu, ni bora uongozi awamu hii wangefanya hekima tú waliofanya kazi mda mrefu na wamekuwa wazoefu wangeachwa kwani tayari walishatumia nguvu nyingi katika maisha yao ila wanaopata ajira kwa sasa udhibiti infanyike yasijejirudia tena!
 
Duh! ila nimeamini akina Lowasa, Sumaye, Kingunge, Kikwete .... waliiharibu sana nchi hii! Asante Mungu kutuletea Dr John Pombe Magufuli. Ana kazi kubwa hadi 2025 tutakuwa pazuri sana!!!!!
2020
harudi mkuu!
 
Kumbe tulikuwa wa hovyo kiasi hiki? Ndo maana wengine tunaamini JPM ameshushwa na Mungu kuja kutuweka sawa. TULIKOKUWA TNAPELEKWA NCHI HII SIKO!!!
Mkapa alishushwa na nani?
 
Aliyefukuza wenye vyeti feki ni Necta si Mh Magufuli. Necta ndio walioona vyeti hivyo vimegushiwa kwa kubadilisha matokeo. Wakujilaumu ni waliobadili matokeo kienyeji badala ya kurudia masomo.
Inauma sana lakini wamekosea na si waamiiifu na ni watu wanaojijali wao tu hawakotayari kuona wenzao wanapata ndio maana wamethubutu kubadili alama zao.
Waende ajira binafsi ili mradi taaluma zao hazijakataliwa na vyuo walivyopita.
 
Sakata la vyeti ni kizungumkuti, kwa watu wenye uwezo wa kufanya kazi wangepunguzwa sifa zao,mfano wenginewalitakiwa warudishwe kwenye sifa ya astashahda badala ya stashahada.
Nakumbuka mwaka fulani nilikuwa Songea,na kulikuwa na afisa mmoja wa polisi akiwa na wadhifa mkubwa kule CCP na zilipotoka nafasi za upolisi alisomba wafanyakazi wake wa ndani kama saba hivi,kuanzia walisha mifugo,wapishi,watunza bustani na mashmba wote wakaingia upolisi kwa kutumia vyeti vya kidato cha nne vya watu wengine!!!
Sasa hawa najua zoezi la uhakiki litawaacha salama maana vyeti vyao ni halali,ila kiuhalisia hata elimu kamili ya msingi hawana.!!!!
Mmoja aliyetoa cheti chake nasikia alilalamika baada ya kusikia jina lake linatumiwa na polisi huko Mpanda lakini alishindwa namna ya kufika huko maana yeye hana kazi.
 
Back
Top Bottom