Vyandarua vinapunguza nguvu za kiume?

Mallaba

JF-Expert Member
Jan 30, 2008
2,554
47
BAADHI ya kinamama katika Kijiji cha Sazira Kata ya Sazira wilayani hapa wameacha kutumia vyandarua vyenye dawa ya kuulia mbu kwa kuwa zinawapunguzia waume zao nguvu za kiume.

Wakichangia maoni yao kwa timu ya kuhamasisha matumizi ya vyandarua kutoka asasi binafsi ya Bunda Youth and Women Development iliyotembelea kijijini hapo jana,wanawake hao walisema katika kipindi ambacho wamekuwa wakitumia vyandarua hivyo waume zao wamekuwa wachovu wakati wa tendo la ndoa.

Walisema hali imekuwa tofauti baada ya kuacha kutumia vyandarua hivyo siku chache na kufafanua kuwa pengine udhaifu huo, ulisababishwa na kemikali zilizomo kwenye vyandarua hivyo.

“Tumeachana na vyandarua hivyo kwani tulipokuwa tukivitumia tulikuwa hatuwasikii waume zetu vitandani, lakini sasa mambo yako safi,”alisema mwanamke mmoja ambaye jina lake linahifadhiwa .

Pamoja na mratibu wa kupambana na ugonjwa wa malaria kutoka katika asasi hiyo Protas Materego kuwahakikishia kinamama hao kuwa vyandarua hivyo havina madhara yoyote na kuwasihi wavitumie ili kujikinga na ugonjwa huo, walisisitiza kwamba hawatavitumia kwani wakiendelea kuvitumia watakosa raha ya ndoa zao.

Naye Maimu Mganga Mkuu wa wilaya hiyo, Sucha Samuel alipoulizwa na mwandishi kuhusu madai ya kinamama hao alisema hali ya kupungua kwa nguvu za kiume kwa wanaume haitokani na matumizi ya vyandarua bali ni matatizo ya kisaikolojia na kuitaka jamii kutoendekeza mapokeo yasiyo ya maana badala yake wawasikilize wataalam.
Mwannchi.
 
Mambo hayo...

Offside Trick wanakwambia kwa nini unashangaa ukiambiwa na kwa nini unakataa kinacholiwa.
 
Hii kali, sasa kwa wanaoishi huko jijini dsm ambapo vyandarua ni daily wanaume si watakuwa hawana kabisa hizo nguvu zao? Mmh
 
yaani we acha tu maana hata mimi nimefikiria sana bila ya kupata majibu sitahiki
Hii kali, sasa kwa wanaoishi huko jijini dsm ambapo vyandarua ni daily wanaume si watakuwa hawana kabisa hizo nguvu zao? Mmh
 
Enyi kundi dogo lenye fikra pevu mnijulishe mimi juu ya habari zilizozagaa huku mtaani kuwa vyandarua vyenye dawa zinamaliza nguvu za kiume.je kuna ukweli wowote? na kama hakuna nini kisa za uzushi huu?.mwenye upeo wa jambo hili lete ukweli
 
Back
Top Bottom