“Vyama vya Upinzania (UKAWA): Mumejikita kupiga chenga huku mukifungwa magoli”

Ccm wanaringia vyombo vya dola hiyo ndio silaha yao kubwa!
 
Mara nyingi sipendi kuandika makala zinazogusa wanasiasa na vyama vya siasa kwani miitikio yake huwa ni ya miheuko na ushabiki zaidi kuliko mantiki ya kile kilichoongelewa. Mbaya zaidi mijadala ya kisiasa inalazimisha kutaja majina/watu ili kujenga hoja (imezoeleka hivyo) jambo ambalo halina afya kabisa kwenye dhana ya kujadili hoja. Hata hvyo ngoja leo niandike kudogo labda kuna mtu mmoja anaweza kusaidika na ninaelekeza hoja yangu kwenye eneo moja tu: namna siasa za UKAWA zilivyoshindwa kupata pa kusimamia katika kushindana na serikali ya CCM chini Rais JPM.

Mjadala wa mabadiliko ya sheria zihusianazo na mali asili ulioko bungeni na matukio mengine kadhaa ya siku za karibuni, vimenikumbusha pambano la ngumi za uzito wa juu la round 12 nililolitazama wiki chache zilizopita. Pambano hili lililofanyika katika ukumbi wa Wembley pale London na kwa bahati mbaya nimeshindwa kukumbuka majina ya mabondia hussika. Ila jambo moja linanifanya nikumbuke pambano lile pambano mara nyingi. Bondia mmoja alikua mrefu mwenye umbo kubwa na mwenye asili kama ya Ukraine na wa pili alikua mweusi, ana umbo la kumtosha lakini hakua mrefu kama wa kwanza.

Muda wote wa pambano kuanzia round ya kwanza yule mrefu alikua anajitamba tu kwa maneno mengi na kuonesha kwamba ngumu alizokua anapigwa sio chochote na hazimtingishi. Alikua akichapwa ngumi anajitingisha mabega kuonesha ubabe wake huki akisindikiza na lugha za kebehi na uso uliojaa dharau. Wakati anafanya hayo yote, yule jamaa mwingine muda wote alijitahidi kurusha ngumu na kumsikumizia mwenzake kwa kila ujuzi aliokua nao. Alitumia muda wake wote kwa umakini kutafuta ushindi ama kwa points au kw knockout. Alifanikiwa kumtandika mbabe yule ngumu zilizomtoa hata damu mdomoni. Mwisho wa round ya mwisho huyu mweusi alishinda pambano kwa points wakati yule mrefu bado akijinasibu kwa uso wa dharau kama mbabe.

Pambano hili lilinikumbusha sana umuhim wa kutambua aina ya mashindano/vita inayokukabili kwa wakati fulani na ni yepi mambo ya muhim ya kuzingatia kwa wakati huo. Ni muhim kutambua ni kitu gani chenye tija unatakiwa kufanya kwa wakati maalum na hasa katika mashindano. Jina, uwezo, na umaarufu wako au shuhuda za utendaji wako wa huko nyuma zinaweza zisiwe na msaada kwa kila kitu na mahali. Mabondia hawa walikua ulingoni na jambo kubwa lililokua linatafutwa ulingoni ni ushindi. Ni wakati wa kuonesha maarifa, ujuzi na uwezo wa kumkabili mwenzako ili kujipatia ushindi kwa njia yoyote ile iliyo ndani ya kanuni za mchezo. Ule haukua muda wa matambo, kujivuna, kuongea wala kuonesha kwamba wewe huumizwi na ngumu za mwenzako. Ulikua ujinga mkubwa kujitamba kwamba ni mbabe huku unavuja damu mdomoni.

Kama mwanafunzi wa uzuoni, nina amini katika mijadala na tofauti ya tafakuri maana hakuna mtu mwenye kujua kila kitu kwa kiwango kinachotegemewa. Kwa minajili hiyo ninaamini siasa za ushindani kwa maana ya kuwa na mitizamo tofauti kwenye mambo yahusuyo uongozi na maslahi ya taifa letu. Vyama vya upinzani Tanzania vimekua na hoja nzito kwa miaka mingi ikiwa ni pamoja na vita dhidi ya rushwa, ufisadi, mikataba mibovu, ulinzi wa maliasili zetu. Pamoja na madhaifu yao mengine lakini walijijengea heshima kwenye misimamo thabiti juu ya mambo yenye manufaa kwa taifa letu. Sina hakika kama kuna mtu aapinga katika hili.

Kwa namna ambayo haikutegemewa na wengi, CCM ileile iliyolaumiwa kwa kutokuja kelele za utendaji mbovu, sasa imetoa ungozi wa nchi ambao kwa sehemu kubwa unaonesha kufanyia kazi zile hoja ambazo zilisimamiwa na wapinzani. Kwa lugha ya wageni wangesema kinachofanyika na serikali ya CCM ni GAME CHANGE na kwenye lugha ya kitafiti tungesema kinachofanyika ni PARADIGM SHIFT ya dhana ya uongozi wa serikali chini ya CCM. Kwamba yanayofanywa yanafanywa kwa usahihi au makosa kiasi gani hilo ni jambo jingine, ila hoja yangu ni kwamba CCM inafanya na inagusa yale mambo ambayo haikutegemewa kabisa kugusa hasa kutokaa na historia ya serikali zake za nyuma.

Kwa maana nyingine, kama tukichukulia CCM chini ya Dr. JPM na upinzani (UKAWA to be specific) ni mambondia, sasa ni muda wa pambano juu ya ulingo ambapo lengo ni ushindi. Pambano hili la kisiasa linahitaji kuonesha ni nani kati yao ana hoja zenye mashiko kwa ustawi mpana wa taifa letu. Yoyote kati ya hawa wawili atakayefanya mambo yanayogusa maisha ya wananchi au kulenga kutatua changamoto zao ndio atakayeondoka na points na kuwa mshindi wa pambano. Hivyo kila mmoja anatakiwa kujikita katika kurusha makonde na kuonesha ujuzi wa kutandika mahali sahihi pa kumletea ushindi.

Kwa jinsi mambo yanavyoenenda nashawishika kwamba vyama vya upinzani vimeshindwa kujikita mahali sahihi katika pambano hili. Tangu Mh Rais JPM aliemshe dude kwenye mambo kadhaa haswa kama tatizo la wizi kwenye madini na sasa mjadala wa mabadiliko ya sheria, ninaona udhaifu mkubwa jinsi ambavyo vyama vya upinzani vinatekeleza wajibu wao. Kuhoji na kujenga hoja kwao, kwa sehemu kubwa kunatoka nje ya mada na hivyo kujikuta wanachanganyikiwa. Sina hakika iwapo wana msimamo wa pamoja kwenye mambo mengi ambayo baadhi yao wanahoji au kupinga. Wamejikita sana kuonesha historia yao, misuli yao, umahiri wao wa kujenga hoja na jinsi ambavyo walitetea mambo ya msingi kwa taifa huku wakiicha mada mezani. Nimefuatilia mijadala mingi bungeni na ninashawishika kwamba muda mwingi wa kushiriki pambano unatumika kupoteza muda wa mchezo. Kauli za kuonesha kwamba CCM ilikosea kwa miaka mingi, nani alikosea zaidi, nani amekua akitetea nini kwa miaka mingi, kutabiri hali mbaya zinazoweza kutukabili baadaye, kulaani, na mengine sidhani sana kama vinaongeza points kwenye hili pambano.

Kama ilivyokua kwa yule bondia mrefu, UKAWA wameshindwa kuelewa kwamba huu sio wakati wa majigambo. Huu sio wakati wa kuonesha waliwahi kufanya wala kusema nini wala hoja gani ilikuwa ya kwao na haikua ya nani. Huu sio wakati muafaka wa kuelezea kwa kina ni nani alihusika kutufikisha tulipo au nani alikua mkosaji mkubwa zaidi. Hoja iliyoko mezani kwa sasa ni kubadilisha mambo na mshindani wao ndipo alipoelekeza nguvu zake. Kajitokeza kiongozi ambaye anataka kubadili baadhi ya mambo ambayo waliyapigia kelele kwa muda mrefu na ni lazima nao wajipange kutafuta namna nafasi yao itaonekana. Focus ingetakiwa kujikita kwenye hoja serikali inazozitekeleza kwa kasi na kutafuta namna sahihi ya kushiriki kuwa sehemu ya mabadiliko badala ya kujikita kwenye udhaifu technicalities/logistics. Kwa kujikita kwenye technicalities wanazidi kujiweka pembeni na wanaonekana hawana mchango. Baadhi ya wabunge wao makini kabisa wanasimama bungeni na mwisho wa dakika za kuongea huoni walipogusa kwenye hoja inayojadiliwa. Mambo mengi wanayotumia muda mrefu kuyagusia kama malalamiko na madai labda yangefaa zaidi kwenye mikutano ya kisiasa kuliko bungeni.

Mimi ningewashauri UKAWA wabadili namna ya kukabiliana na siasa za zama hizi. Ile style ya miaka ya nyuma (hasa enzi za JK) haifanyi kazi kwenye mfumo wa sasa hivi kwani bondia JPM ana tofauti nyingi sana na bondia JMK kuanzia mitizamo, uchukuaji maamuzi, falsafa zinazowaongoza, umuhimu wanaouweka kwenye mambo, ujengaji mahusiano na mtu/watu, na hata kasumba zao kama binadamu. Watafute namna sahihi ya kufanya siasa za kuongeza tija kwenye yale yanayotekelezwa badala ya kubaki pembeni wakitarajia majuto baadaye. Kibaya zaidi, iwapo kuna makossa yatatokea yatatuathiri wote pamoja na wao. Wasitoe maoni, mapendekezo, ushauri na criticism kwa hasira/jazba au namna inayoonesha wako frustrated maana inatoa tafsiri tofauti kabiwa kwa yule wanayetaka awasikie. Nikiwasikiliza, ninaona hawapingani na mambo mengi CCM inayofanya chini ya Rais JPM ila wako frustrated na hali hilo inaondoa nguvu na mashiko ya hoja zao. Pili inawafanya kushindwa kutazama hata namna bora ya kuongelea mambo yanayotukabili kwa pamoja kama taifa (Mfano, mauaji yanayoendelea mkoa wa Pwani na mengine).

Nina hakika siwezi kujiweka kwenye viatu vyao ili nijue hisia gani wanazo, ila ninashwishika kwamba kuna njia mbadala ya kufanikisha wanachokitamani kwa manufaa ya nchi. Kama hawatazingatia hilo, basi wasije kushangaa mwisho wa pambano wakajikuta hawana ushindi / points huku bado wakijiona ni wenye nguvu na uwezo wa kushinda pambano (hoja za kisiasa). Rekodi za mapambano zinaelezea zaidi ni nani aliyekua mshindi wa magoli na sio ni nani alipiga chenga nyingi. Kwenye siasa, mwenye points atakua yule ambaye wananchi wengi wanaoana alisikiliza na kutekeleza kile walichokitamani au kinachogusa maisha yao na sio namna bora zaidi ya jinsi ya kukiteleza. Kwa kuwa mutaonekana hakuna ambacho mutakua mumefanikisha, wananchi hawatakua na cha kulinganisha kati ya kilichofanywa na kile munachosimamia kwamba kimefanywa kwa makosa.

Imeandikwa na Mwalimu MM
Mawasiliano: mmmwalimu@gmail.com
Mzee nakuahidi CCM hawawezi kuifanyia lolote la maana Tanzania zaidi ya usanii kama wewe unalo lamaana CCM wamefanya au Magufuli tutajiye sioni zaidi ya usanii tu
 
Like you said in your opening paragraph, in JF, political threads are not given the required indepth analysis leading to more informed discussions. Instead, they are judged by reading the first few lines and that is it. Consequently, you end up coming across irrelevant comments lacking in substance. I wonder where this weakness stems from but it is a high time our politicians sat down and strategized a fresh.
In any war, tactical retreat and re-strategization is a very important ingredient if you are interested in victory. Without taking their time to learn and make better use of current political environment, they will end up and find themselves in the same spot/page not knowing what actually afflicts them.
As has been seen in most of their discussions in the parliament, opposition politicians are living in their past, forgetting that the past is gone and tomorrow is more important than today. They have to cut down or all together stop their heckling and wailing like mad dogs on the loose.
 
1.jpg

Mara nyingi sipendi kuandika makala zinazogusa wanasiasa na vyama vya siasa kwani miitikio yake huwa ni ya miheuko na ushabiki zaidi kuliko mantiki ya kile kilichoongelewa. Mbaya zaidi mijadala ya kisiasa inalazimisha kutaja majina/watu ili kujenga hoja (imezoeleka hivyo katika nchi yetu) jambo ambalo halina afya kabisa kwenye dhana ya mijadala yenye tija. Hata hvyo ngoja leo niandike kidogo labda kuna mtu mmoja anaweza kusaidika na nitaelekeza hoja yangu kwenye eneo moja tu: namna ambavyo siasa za UKAWA zimeshindwa kupata pa kusimamia katika kushindana na serikali ya CCM chini Rais JPM.

Mjadala wa mabadiliko ya sheria zihusianazo na mali asili ulioko bungeni na matukio mengine kadhaa ya siku za karibuni, vimenikumbusha pambano la ngumi za uzito wa juu la round 12 nililolitazama wiki chache zilizopita. Pambano hili lililofanyika katika ukumbi wa Wembley pale London na kwa bahati mbaya nimeshindwa kukumbuka majina ya mabondia husika. Ila jambo moja linanifanya nikumbuke pambano lile mara nyingi. Bondia mmoja alikua mrefu, mwenye umbo kubwa na mwenye asili kama ya Ukraine na wa pili alikua mweusi, ana umbo la kumtosha lakini hakua mrefu kama wa kwanza.

Muda wote wa pambano kuanzia round ya kwanza yule mrefu alikua anajitamba tu kwa maneno mengi na kuonesha kwamba ngumi alizokua anapigwa sio chochote na hazimtingishi. Alikua akichapwa ngumi anajitingisha mabega kuonesha ni mbabe, huku akiongea lugha za kebehi na uso uliojaa dharau. Wakati anafanya hayo yote, yule jamaa mwingine muda wote alijitahidi kurusha ngumi kwa kila ujuzi aliokua nao. Alitumia muda wake wote kwa umakini kutafuta ushindi ambao angeupata ama kwa points au kwa knockout. Alifanikiwa kumtandika yule aliyejiona mbabe ngumi zilizopelekea hadi kumtoa damu mdomoni. Mwisho wa round ya 12 huyu mweusi alishinda pambano kwa points wakati yule mrefu bado akijinasibu kwa uso wa dharau kwamba ni mbabe.

Pambano hili lilinikumbusha sana umuhim wa kutambua aina ya mashindano/vita inayokukabili kwa wakati fulani na ni yepi mambo ya muhim ya kuzingatia kwa wakati huo. Ni muhim kutambua ni kitu gani chenye tija unatakiwa kufanya kwa wakati maalum na kwa usahihi. Jina, uwezo, na umaarufu wako au shuhuda za utendaji wako wa huko nyuma zinaweza zisiwe na msaada kwa kila kitu na kila mahali. Mabondia hawa walikua ulingoni na jambo kubwa lililokua linatafutwa ni ushindi. Ulikua wakati wa kuonesha maarifa, ujuzi na uwezo wa kumkabili mwenzako ili kujipatia ushindi kwa njia yoyote ile iliyo ndani ya kanuni za mchezo. Ule haukua muda wa matambo, kujivuna, kuongea wala kuonesha kwamba wewe huumizwi na ngumu za mwenzako. Ulikua ujinga mkubwa kwa bondia mrefu kujitamba kwamba ni mbabe huku unavuja damu mdomoni na mwenzake anachukua points.

Kama mwanafunzi wa uzuoni, ninaamini katika mijadala na tofauti za tafakuri maana hakuna mtu mwenye kujua kila kitu kwa kiwango kinachotegemewa. Kwa minajili hiyo ninaamini siasa za ushindani kwa maana ya kuwa na mitizamo tofauti kwenye mambo yahusuyo uongozi, utawala, vipaumbele na maslahi ya taifa letu. Vyama vya upinzani Tanzania vimekua na hoja nzito kwa miaka mingi ikiwa ni pamoja na vita dhidi ya rushwa, ufisadi, mikataba mibovu, ulinzi wa maliasili zetu, haki na mengine. Pamoja na madhaifu yao mengine lakini walijijengea heshima kwenye misimamo thabiti juu ya mambo yenye manufaa kwa taifa letu ambayo ilionekana kama vile CMM na serikali zake hawakujali. Sina hakika kama kuna mtu aapinga katika hili.

Hat ahivyo, kwa namna ambayo haikutegemewa na wengi, CCM ileile iliyolaumiwa kwa kutokujali kelele ndidi ya utendaji mbovu, sasa imetoa uongozi wa nchi ambao kwa sehemu kubwa unaonesha kufanyia kazi zile hoja ambazo zilisimamiwa na wapinzani. Kwa lugha ya wageni wangesema kinachofanyika na serikali ya CCM ni GAME CHANGE (kubadili mchezo) na kwenye lugha ya kitafiti tungesema kinachofanyika ni PARADIGM SHIFT (mtazamo mpya) ya dhana ya uongozi wa serikali chini ya CCM. Kwamba yanayofanywa yanafanyika kwa usahihi au makosa kiasi gani hilo ni jambo jingine, ila hoja yangu ni kwamba CCM inafanya na inagusa yale mambo ambayo haikutegemewa kabisa kugusa hasa kutokaa na historia ya serikali zake huko tulikotoka.

Kwa maana nyingine, kama tukichukulia CCM chini ya Dr. JPM na upinzani (UKAWA to be specific) ni mabondia, sasa ni muda wa pambano juu ya ulingo ambapo lengo ni ushindi wa kisiasa. Pambano hili la kisiasa linahitaji kuonesha ni nani kati yao ana hoja zenye mashiko kwa ustawi mpana wa taifa letu na hoja hizo kukubalika na wananchi walio wengi. Yoyote kati ya hawa wawili atakayefanya mambo yanayogusa maisha ya wananchi au kulenga kutatua changamoto zao ndio atakayeondoka na points na kuwa mshindi wa pambano. Hivyo kila mmoja anatakiwa kujikita katika kurusha makonde na kuonesha ujuzi wa kutandika mahali sahihi pa kumletea ushindi kulingana na kanuni za mchezo. Kigumu zaidi, mchezo huu wa siasa hauna kanuni zilizonyooka sana na kuna kuchezea rafu nyingi, hivyo utulivu, hekima, busara, na uwezo wa kubuni mbinu mpya kila wakati ni nyenzo za msingi sana.

Kwa jinsi mambo yanavyoenenda nashawishika kwamba UKAWA wameshindwa kujikita mahali sahihi katika harakati zao za kisiasa. Tangu Mh Rais JPM aliemshe dude kwenye mambo kadhaa haswa kama tatizo la wizi kwenye madini na sasa mjadala wa mabadiliko ya sheria, ninaona udhaifu mkubwa jinsi ambavyo wanatekeleza wajibu wao wa siasa za ushindani. Kuhoji na kujenga hoja kwao, kwa sehemu kubwa kunatoka nje ya mada zilizo mezani na hivyo kujikuta wanaonesha aina fulani ya kuchanganyikiwa. Sina hakika iwapo wana msimamo wa pamoja kwenye mambo mengi ambayo baadhi yao wanahoji au kupinga kwani hawaoneshi kuwa na rhythm yenye mwelekeo mmoja na wengine haijulikani wanasimamia nini kwa sasa kwani wameamua kukaa kimya. Kwa wanaongea, wamejikita sana kuonesha historia ya hoja zao, misuli yao ya kupambana kisiasa, umahiri wao wa kujenga hoja, na jinsi ambavyo walitetea mambo ya msingi kwa taifa. Wanayafanya haya kama mbadala wa mada iliyoko mezani hivyo kutoeleweka. Nimefuatilia mijadala mingi bungeni na nimesikitika kuona muda mwingi wa kushiriki pambano unatumika vibaya na hautumiki kaongeza points za mchezo. Kauli za kuonesha kwamba CCM ilikosea kwa miaka mingi, nani alikosea zaidi, nani amekua akitetea nini kwa miaka mingi, kutabiri hali mbaya zinazoweza kutukabili baadaye, kulaani uongozi wa serikali na CCM kaka kundi, na mengine ya aian hiyo, sioni kama vinawaongezea points kwenye hili pambano.

Kama ilivyokua kwa yule bondia mrefu, UKAWA wameshindwa kuelewa kwamba huu sio wakati wa majigambo. Huu sio wakati wa kuonesha waliwahi kufanya wala kusema nini huko nyuma wala hoja gani ilikuwa ya kwao na haikua ya nani. Huu sio wakati muafaka wa kuelezea kwa kina ni nani alihusika kutufikisha tulipo au nani alikua mkosaji mkubwa zaidi maana huenda wanajulikana. Huo sio wakati wa kuonesha (kwa maneno) nani mjinga zaidi, nani ana busara na hekima zaidi au nani kasoma kuliko wengine. Hoja iliyoko mezani kwa sasa ni kubadilisha mambo ya hovyo yaliyokuwepo na mshindani wao (CCM chini ya JPM) ndipo alipoelekeza nguvu zake zote. Kajitokeza kama kiongozi ambaye anataka kubadili mambo ambayo UKAWA (na baadhi ya wanaCCM) waliyapigia kelele kwa muda mrefu na ni lazima nao wajipange ili kutafuta namna ya mchango wao ktaonekana bado upo. Focus yao ingetakiwa kujikita kwenye hoja serikali inazozitekeleza kwa kasi na kutafuta namna sahihi ya kushiriki kuwa sehemu ya mabadiliko badala ya kujikita kwenye udhaifu technicalities/logistics unaoneshwa na serikali. Kwa kujikita kwenye technicalities pekee wanazidi kujiweka pembeni na wanaonekana hawana mchango/ relevance. Baadhi ya wabunge wao makini kabisa wanasimama bungeni na mwisho wa dakika za kuongea huoni walipogusa kwenye hoja inayojadiliwa. Mambo mengi wanayotumia muda mrefu kuyagusia kama malalamiko na madai labda yangefaa zaidi kutafutiwa mahali sahihi kama mikutano ya kisiasa lakini sio bungeni.

Mimi ningewashauri UKAWA wabadili namna ya kukabiliana na siasa za zama hizi. Ile style ya miaka ya nyuma (hasa enzi za JK) haifanyi kazi kwenye mfumo wa sasa hivi kwani bondia JPM ana tofauti nyingi sana na bondia JMK kuanzia mitizamo, uchukuaji maamuzi, falsafa zinazowaongoza, umuhimu wanaouweka kwenye mambo, ujengaji mahusiano na mtu/watu/nchi, na hata kasumba zao kama binadamu. UKAWA watafute namna sahihi ya kufanya siasa za kuongeza thamani/tija kwenye yale yanayotekelezwa na serikali au kusaulika badala ya kubaki pembeni wakitutabiria majuto/mabaya baadaye. Kibaya zaidi, iwapo kuna makosa yatatokea kwa kile wao wanachoona hakifanyiki sawa yatatuathiri wote pamoja na wao. Wasitoe maoni, mapendekezo, ushauri na criticism kwa hasira/jazba au namna inayoonesha wako frustrated maana inatoa tafsiri tofauti kabisa kwa yule wanayetaka awasikie. Wanaweza kuhisi/kuona wanapuuzwa serikali lakini shida ikawa ni naona wanavyojieleza na wanapoelekeza hoja zao. Nikiwasikiliza UKAWA, ninaona hawapingani na mambo mengi CCM inayofanya chini ya Rais JPM ila iko kama wako frustrated na hii inaondoa nguvu na mashiko ya hoja zao. Pili inawafanya kushindwa kutazama hata namna bora ya kuongelea mambo yanayotukabili kwa pamoja kama taifa (Mfano, mauaji yanayoendelea mkoa wa Pwani na mengine). Pamoja na kuonesha kutofurahishwa na mauaji yanayoendelea Pwani, wamefanya hivyo kama sehemu ya lawama na kuishutumu serikali badala ya kuonesha mshikamano na umoja wa kitaifa katika kulaani kinachoendelea. Hili ni kosa kubwa kisiasa.

Nina hakika siwezi kujiweka kwenye viatu vyao ili nijue hisia gani wanazo, ila ninashwishika kwamba kuna njia mbadala ya kufanikisha wanachokitamani kwa manufaa ya nchi na kuendelea kuonekana ni relevant kwenye siasa za ushindani. Kama hawatazingatia hilo, basi wasije kushangaa mwisho wa pambano wakajikuta hawana ushindi / points huku wao wakijiona ni wenye nguvu na uwezo wa kushinda pambano (hoja za kisiasa). Rekodi za mapambano zinaelezea zaidi ni nani aliyekua mshindi wa magoli na sio ni nani alipiga chenga nyingi. Kwenye siasa, mwenye points atakua yule ambaye wananchi wengi wanaoana alisikiliza na kutekeleza kile walichokitamani au kinachogusa maisha yao na sio namna bora zaidi ya jinsi ya kukiteleza. Kwa kuwa mwisho wa pambano mutaonekana hakuna ambacho mumefanikisha, wananchi hawatakua na cha kulinganisha kati ya kilichofanywa na serikali na kile munachosimamia kwamba kimefanywa kwa makosa.

Kama nia yenu ni kujenga Tiafa, basi badilisheni mkakati kwani njia munayoitumia kwa sasa inaweza kukosa mchango unaonekana. Ninashawishika kwamba hamujataka kutafuta njia sahihi ya kusikilizwa na Rais JPM bali munalazimisha njia ambazo kwake hazifanyi kazi. Mukikijua munachotaka kufanikisha mutatumia kila njia halali inayowezekana kukipata badala ya kulaumu kwamba kuna mtu (Rais JPM na CCM) anayekuweka ukuta.

Tatizo ni kushindwa kuelewa mambo kwa undani, kwa sisi wengi tunaoishi nje ya nchi tunaona wazi kuwa ccm imezidi kupata pigo na upinzani umezidi kuimarika. sasa kwa uelewa mdogo wa watu wachache wanahisi hizo kelele na vituko vinavyofanywa kwa mabavu ndio siasa la hasha mtakuja kushangaa jinsi ccm itakavyopoteza viti vingi
 
Back
Top Bottom