Vyama vya Upinzani vyafungua kesi kwenye Mahakama ya Afrika Mashariki kupinga Sheria kandamizi ya vyama vya siasa kutumika

Wasalaam, nauliza tu ili nipate elimu japo kidogo: je ni sahihi na uzalendo kwa vyama vya upinzani tanzania bara kufungua shitaka la kikatiba ktka mahakama kuu kanda ya dar es salaam kupinga sheria mpya ya vyama vya siasa 2018 ikiwa hili LA CAG bado halijapoa ni kaa la moto.

Ingekua vema wangevuta subira kusubiri suluhu ya huu mgogoro wa kikatiba kati mh spika na CAG. Maana inazusha taharuki, kesi za kikatiba zitakua nyingi tutachelewa maendeleo na Tanzania ya viwanda. Ova
 
Tupo kwenye tatizo la Sheria kandamizi,zinapitishwa kwa mabavu na kutumika dhidi ya wapinzani.
Hii dhana Ni mbovu mno,kwamba chama tawala ndiyo Watanzania.Mambo sensitive kama haya huamsha hasira za watawaliwa.
Mkuu hizi sheria sio kwaajiri ya wapinzani nikwaajili ya Watanzania wote sema ccm ni vilaza wanaliwa live


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bora huko kwenye mahakama ya Afrika mashariki wangalau majaji wanajua wajibu wao. Hata serekali wasipotekeleza hukumu ya mahakama lakini nia ovu ya hiyo sheria itawekwa wazi, na dunia itafahamika kabisa kwamba serekali ya Tanzania haifuati sheria na mahakama za ndani zimeingiliwa na wanasiasa wa ccm. Kuanzia sasa kuonyesha kwamba hatuna imani na mahakama za ndani ni vyema kesi zote kufunguliwa kwenye mahakama zisizotii watawala bali zinazotoa haki.
 
Mambo mengine bhana. ..
Sasa hata wakishinda nani ata enforce hiyo ruling?
Maana Africa kila mtu anajitawala anayotaka

Uko sawa, lakini hata serikali isipotekelexa hiyo hukumu bado nia ovu ya hiyo sheria itawekwa wazi, na serikali ya Tanzania itafahamika kwamba haifuati sheria. Mbinyo mingi ya kimataifa itaiweka Tanzania pabaya. Dunia ikianza kuiweka Tanzania pabaya hali itazidi kuwa ngumu. Mfano mrahisi ni sasa kwa wafadhili kuzuia misaada yao unaona mambo yanavyoyumba. Hali hii itakuwa mbaya zaidi.
 
I am ignorant of the Good Word in the Clean Book....

Uncle looks down upon Us ,he says we are mere dialema..we dont know the way of our Government
He says ,we.are real ignorant of the good word in the clean Book..and we dont have that uzalendo....


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Swadakta
 
Unajua hii sheria ya vyama vya siasa ya Tanzania hata Makaburu hawakuwahi kuitumia
Erythro, naomba niulize, kwa sababu sina kumbukumbu na hili.
Hivi kesi kama hiyo iliyofunguliwa kwenye mahakama ya Afrika Mashariki iliwahi kufikishwa kwenye mahakama yetu hapa?

Ninachokumbuka ni wakati ilipofunguliwa kesi kabla bunge halijapitisha sheria hiyo; ilikuwa bado ni mswada. Je, baada ya kuwa sheria na kusainiwa, mahakama zetu bado zilikataa kuipokea kesi hiyo, na kulazimu kwenda Mahakama ya Afrika Mashariki?
 

Mkuu inawezekana hitler ame re incarnate. Ndio maana mambo ya ki dictator tumeanza kuyaona tz. Mkuu na hasa ukichukulia kuwa Tanganyika iliwahi kuwa chini ya dola la wajerumani, si ajabu roho ya babu hitler kuweza kujipenyeza miongoni mwa watawala wetu. Nadhani hata Botha na Ian Smith wanatushangaa kwa jisnsi serekali yetu ilivyowashupalia wakati wa utawala wao wa mabavu. Lakini kwa sasa serekali yetu inafanya udhalimu kuliko walio ufanya wao.
 
Lundo la watu wema wamependekeza kesi hii ifunguliwe huko wakiwemo majaji wa Tanzania wanaoelewa sana mambo ya awamu ya 5
 
Asante sana mkuu
 
Safi sana.........

Naona mwisho wa udikteta umekaribia!

Kwa kuwa hizo mahakama za nje, Jiwe hawezi "kuziagiza" watoe hukumu anayotaka yeye
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…