Vyama vya upinzani na mgomo wa TUCTA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vyama vya upinzani na mgomo wa TUCTA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Dingswayo, May 5, 2010.

 1. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #1
  May 5, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Ningependa kujua kuwa vyama vya upinzani vina mawazo gani kuhusu suala zima la madai ya TUCTA na kufuatilia vitisho vya serikali kuzuia wafanyakazi kugoma.
   
 2. Technician

  Technician JF-Expert Member

  #2
  May 5, 2010
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 843
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  :target:
   
 3. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #3
  May 5, 2010
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Nadhani unge-rekebisha sentensi yako na kuwa hivi...."Dr. Slaa ana maoni gani?" maana so far sioni chama cha upinzani kilichosimama imara zaidi ya Mh. Dr. Slaa as an individual.
   
 4. s

  shujaa Member

  #4
  May 5, 2010
  Joined: Jul 10, 2009
  Messages: 60
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Inasikitisha sana kuona vyama vyetu vya upinzani vinavyoshindwa kuonyesha mshikamano katika suala SENSITIVE kama hili, Mpaka sasa walitakiwa watoe kauli ya pamoya kulaana kauli za HOVYO HOVYO za "MWAJIRI MKUU" badala ya kuongea mmoja mmoja kama alivyofanya Proph Lipunba, na watoe msimamo wao kama wanaunga mkkono TUCTE au la
   
 5. Henry Kilewo

  Henry Kilewo Verified User

  #5
  May 6, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 889
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  CDM/Wazee/2010/02

  Kamanda wa Polisi
  Kanda Maalum
  Dar es salaam

  Ndugu

  YAH: TAARIFA YA WAZEE KUFANYA MAANDAMANO KUUNGA MKONO MADAI YAWAFANYAKAZI, KUPINGA MANENO YA RAIS KIKWETE/IKULU NA KULAANI MATENDO YAWALIOITWA WAZEE WA DAR ES SALAAM

  Kichwa cha habari hapo juu cha husika.Kwa niaba ya Baraza la Wazee wa CHADEMA nawasilisha kwako barua ya taarifaya Wazee wa Dar es salaam kufanya maandamano ya amani yenye lengo la kuunga mkono madai ya wafanyakazi, kupinga maneno ya Rais Kikwete/Ikulu na kulaani matendo ya walioitwa wazee wa Dar es salaam.

  Tumefikia uamuzi huu kwa kuzingatia kauli mbiu ya Baraza la Wazee wa CHADEMA kwamba “Wazeeni Hazina ya Hekima na Busara”. Maandamano hayo tumepanga kuyafanya sikuya ijumaa tarehe 7 Mei 2010 na tunakusudia yaanze saa 2 kamili asubuhikatika kituo cha mabasi ya Mwenge kupitia Barabara ya Sam Nujoma mpakakituo cha mabasi cha Ubungo. Maandamano hayo yataongozwa na viongozi wawazee wa CHADEMA kutoka wilaya mbalimbali za mkoa wa kichama wa KinondoniKanda Maalum ya Dar es salaam.

  Tumeamua kuchagua barabara hiyo kwa kuwainapitia katika wilaya za kichama za Kawe, Kinondoni na Ubungo ndani yaHalmashauri ya Kinondoni katika Mkoa wa Dar es salaam. Mwenyekiti wa Mkoawa kichama wa Kinondoni Kanda Maalum Dar es salaam, John Mnyika ambaye piani mwakilishi wa wenyeviti wa CHADEMA katika kanda husika amekubalikupokea maandamano hayo akiambatana na wenyeviti wenzake wa mikoa yakichama ya Ilala na Temeke.

  Izingatiwe kuwa pamoja na kuwa Baraza la Wazee wa CHADEMA Mkoa waKinondoni Kanda ya Dar es salaam hatukuridhishwa na hotuba ya Rais Kikwetealiyoitoa tarehe 3 Mei 2010 tuliheshimu taarifa ya TUCTA ya tarehe 4 Mei2010 ya kusitisha mgomo kwa muda kusubiria hatma ya majadiliano tarehe 8Mei 2010.

  Kwa busara na subira za uzee tulitarajia kwamba Rais Kikwete amawasaidizi wake wangerekebisha kauli zao na kurejea katika ustaarabu wakukubaliana na madai ya msingi ya wafanyakazi na kukiri kuteleza katikamatamshi ya tarehe 3 Mei 2010.

  Hata hivyo, kauli za wasaidizi wa Rais Kikwete walizozitoa tarehe 4 na 5 Mei za kuendeleza suala hili kwakuwabeza wafanyakazi ambao wameamua kurejea kwenye meza ya majadilianozimetufanya tujitokeze wazi kuunga mkono madai ya wafanyakazi na kulaanikauli hizo ili ieleweke wazi kwamba wafanyakazi wanapoingia kwenyemajadiliano tarehe 8 Mei hoja zao zinaungwa mkono na wananchi wa kadambalimbali.

  Wazee tumeshangazwa kauli za Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais ,Menejimenti ya Utumishi wa Umma, George Yambesi za kukanusha kwambawasaidizi wa Rais ikiwemo wa ikulu walimpa taarifa potofu Rais Kikwetezilizopelekea Rais kuwapotosha watanzania katika hotuba yake ya tarehe 3Mei 2010. Pamoja na taarifa ya TUCTA ya kuwa Rais Kikwete hakutoa taarifaza kweli alipoeleza kwamba wameafikiana kuhusu viwango vya kima cha chinicha mishahara katika sekta ya umma wakati ‘wamekubaliana kutokubaliana’kama tamko la Baraza lilivyoeleza; taarifa nyingine ya TUCTAiliyoambatana na ushahidi wa barua kuhusu Rais Kikwete kuupotosha ummakuhusu mwaliko wa mkutano, katika maandamano yetu tunakusudia kutoamaelezo na vielelezo zaidi katika maeneo mengine ambayo Rais Kikwete naikulu hawasemi kweli.

  Mathalani; Rais Kikwete alidai serikali ikitoamishahara kwa kiwango cha shilingi 315,000 kwa watumishi wa umma zaidi ya300,000 shilingi 6,852 bilioni (takribani trilioni saba); alitoa takwimuhii isiyokuwa ya kweli kwa lengo la kuwachonganisha wafanyakazi nawananchi wengine kuwa kama serikali ikiongeza mishahara fedha zotezitaishia kulipa mishahara na hivyo kukosekana fedha kwa ajili ya hudumanyingine za msingi.

  Hata hivyo Rais Kikwete hakusema kweli kwa kuwa kwakiwango cha malipo hayo hayo ya 315,000 jumla ya kiwango cha matumizikatika mishahara hakiwezi kwa watumishi hao wa kima cha chini pamoja nawatumishi wengine hakiwezi kufikia Bilioni 3000 (Trilioni tatu). Hivyo,tunakusudia katika maandamano hayo kuweka hadharani masuala mengine yaziada ambayo Rais Kikwete na ikulu hawasemi ukweli. Katika maandamano hayotunakusudia kutoa maelezo na vielelezo vya sababu za kuunga mkono madai yamsingi matatu ya wafanyakazi kwa kuzingatia kuwa madai hayo yametolewa kwamiaka mingi toka serikali ya Rais Kikwete iingie madarakani mwaka 2005 nayakajadiliwa kwa kina mwaka 2007 lakini mpaka sasa serikali imekuwaikikwepa kuyatekeleza.

  Kuhusu dai la wafanyakazi kutaka nyongeza ya kima cha chini cha mshaharakwa wafanyakazi wa sekta ya umma kufikia ikiwezekana 315,000 Baraza laWazee wa CHADEMA Mkoa wa Kinondoni tunaunga mkono suala hili tukiaminikwamba ni haki ya msingi kwa kuzingatia hali halisi ya gharama za maishana tunaamini serikali inaouwezo wa kulitekeleza.

  Tunakusudia kueleza katika maandamano hayo kueleza kwa maelezo na vielelezo namna ambavyo kwarasilimali ambazo nchi yetu inazo ikiwemo kodi dai hili linawezakutekelezwa kupitia sera mbadala kama ambavyo kambi ya upinzani ilianzakueleza toka hotuba mbadala ya bajeti ya mwaka wa fedha 2007/08.

  Mfano kama Rais Kikwete angeamua toka Orodha ya Mafisadi (List of Shame)iliyosomwa Septemba 15, 2007 kuchukua hatua za haraka kufikisha katika vyombo vya dola watuhumiwa wote wakuu wa ufisadi na hatimaye hukumuzingekamilika haraka zikihusisha kufilisiwa kwa mali za mafisadi; kiwangocha fedha ambacho kingeweza kupatikana ni zaidi ya trilioni moja fedhaambazo ni sawa na malipo ya mishahara ya mwaka mzima kwa kiwango chanyongeza ya 315,000 kwa zaidi ya 100,000 wa umma Tanzania.

  Kiwango cha nyongeza ya mishahara kingeweza kuleta motisha katika kazi na kuongezatija na pato la taifa hatimaye kujenga msingi wa kuweza kulipa mishaharawakati mwingine. Aidha ikumbukwe kwamba katika bajeti mbadala 2007/08Kambi ya Upinzani ilieleza vyanzo vingine mbalimbali vya kodi kwenyemisitu, uvuvi, madini nk ambavyo vilifanya bajeti hiyo kuwa ya shilingitrilioni 8.

  Hata hivyo, Wabunge wa CCM walitumia vibaya wingi wao nakuzikataa hoja za bajeti mbadala na kupitisha bajeti ambayo ilikwepaongezeko hilo la mishahara badala yake ikaongeza gharama za maisha kwakupandisha kodi ya mafuta na bidhaa nyingine zinazowagusa wafanyakazi nawananchi wa kipato cha chini.

  Aidha kima cha chini cha wafanyakazi katikasekta ya umma kingeweza kuongezwa na kulipwa kila mwaka kwa kutumia fedhazinazopatikana kwa kuondoa matumizi ya anasa ya serikali na pia kupunguzapengo kubwa la mishahara katika utumishi wa umma ambalo linazua matabaka.

  Si jambo lenye tija katika utumishi wa umma kuwa Rais, mawaziri wake na watumishi wengine wenye kulipwa mishahara kati ya milioni 5 mpaka 20 kwa mwezi huku mfanyakazi mwingine akilipwa laki moja ambayo ni chini hataposho ya kikao cha siku moja cha watumishi hao wenye kulipwa mishahara mikubwa.

  Hivyo, kupitia maandamano hayo tutatoa maelezo na vielelezo zaidina kulaani kauli ya Rais Kikwete ya kutamka kwa kiburi kwamba hatawafanyakazi wakigoma kwa miaka nane kima cha chini hakitaongezeka kufikia 315,000 na kuitaka ikulu itangaze hadharani kiwango cha mishahara namarupurupu ya Rais na viongozi wengine waandamizi wa serikali yake.

  Wazee tumepanga kuandamana kuunga mkono dai la kuboresha mafao na pensheni tukijua wazi kwamba suala hilo linahitaji kuainisha sheria za mifukopamoja na kuwa na mamlaka ya kudhibiti masuala ambayo yote yalikuwa jukumula bunge ambalo lina wabunge wengi toka CCM na serikali ambayo inaongozwana CCM lakini wameshindwa kuyatekeleza kwa kipindi chote hivyo RaisKikwete hakupaswa kuwalaumu wafanyakazi kwa udhaifu wa uongozi wake.

  Tunaunga mkono dai hili tukiamini kwamba hata kabla ya kuainisha sheria nakuweka mamlaka ya udhibiti bado mazingira yangeweza kuboreshawa kanuni nataratibu zinazopitishwa na mamlaka za kiserikali na wateule wake.

  Barazala Wazee wa CHADEMA tunatambua kwamba kati ya mambo ambayo yanawaathiri wafanyakazi wengi wakiwemo wazee ni mafao na pensheni hususani baada yakustaafu, hivyo, tunaandamana kulaani matendo ya wazee walioitwa wa Dar essalaam ambao wameshindwa hata kutambua hali za wazee wenzao na watanzaniawengine.

  Wazee tumepanga kuundamana kuunga mkono dai la wafanyakazi la kupunguziwakodi ya kipato (PAYE) kutoka kiwango cha asilimia 15 kuwa tarakimu moja(single digit) yaani si zaidi ya asilimia 9 kwa kuwa tunataka kutoamaelezo na vielelezo jinsi ambavyo kupitia sera mbadala na uongozi boraserikali inaweza kupanua wigo wa kodi na kupunguza misamaha ya kodi ilikuondoa mzigo mkubwa kwa wafanyakazi.

  Tarehe 19 Aprili 2010 Mkaguzi na Mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali (CAG) aliueleza umma kuwa serikaliimepoteza Sh 752.4 bilioni katika makusanyo yake ya kodi kutokana na kutoamisamaha mbalimbali ya kodi kwa watu binafsi, taasisi na wawekezajiwakubwa wa sekta ya madini katika kipindi kifupi. (Hii ni sawa na kodi yamwaka ya wafanyakazi zaidi ya milioni tano wa kima cha chini).

  Hii inadhihirisha wazi kwamba serikali inaweza kupunguza kodi kwa wafanyakazina ikafidia mapato kutoka vyanzo vingine kwa kuwa sehemu kubwa ya misamahaya kodi inatumika vibaya kama ambavyo Baraza la Wazee wa CHADEMA tumesoma matangazo kwenye magazeti ya tarehe 5 Mei 2010 kuhusu malalamiko ya Mamlaka ya Mapato (TRA) namna misamaha ya kodi inavyotumiwa vibaya katikasekta ya utalii.

  Wazee tumepanga kuandamana kulaani matendo ya walioitwa wazee wa Dar essalaam kushangilia na kuchochea wakati Rais Kikwete akizungumza manenoyasiyokuwa na ukweli wala ustaarabu ikiwemo kuwaita viongozi wafanyakazi“wazandiki, waongo, wanafiki na wafitini" na kutoa vitisho.

  Tunaandamana kulaani tukio zima ili umma wa watanzania ufahamu kuwa wazee wale hawakuwa wawakilishi rasmi wa wazee wa Dar es salaam jiji ambalo wakazi wake ni pamoja na wazee wenye kuheshimika katika jamii.

  Kutokana na mavazi yao inaonyesha kwamba wazee kwa sehemu kubwa walikuwa ni wanachama wa CCM ambao walikuwa wakishangilia hotuba ya mwenyekiti wa chama chao na kufanyatukio zima liwe kama mchezo wa kuigiza badala ya hotuba ya Rais kwa taifa.

  Kupitia maandamano hayo tutatoa tamko la kumtaka mkuu wa Mkoa wa Dar essalaam aeleze kwa umma sababu za kugeuza tukio la kiserikali kuwa kamamkutano wa chama. Ikumbukwe kwamba Mkoa wa Dar es salaam una wazee tokataasisi mbalimbali mathalani Baraza la Wazee wa CHADEMA pekee lina uongozikwenye ngazi mbambali katika mikoa, wilaya, majimbo na hata matawi lakini halikualikwa katika mkutano huo. Kama wangealikwa wazee ambao wenginewanauzoefu wa uongozi katika serikali ikiwemo masuala ya kisheria na fedhakama Mzee Bob Makani; wangechukua fursa hiyo kumpa Rais ushauri wa hekima na busara badala ya kufanya ushabiki wa kichama usiokuwa na maslahi kwawatanzania walio wengi.

  Tunapanga kuandaamana kutoa maelezo na vielelezo kwamba wazee wale hawakuwakilisha kundi la wazee wenye kutegemea vijana wao wafanyakazi na wazee wenye kukerwa na mfumo wa mafao ya wastaafumathalani wastaafu wa iliyokuwa jumuia ya Afrika Mashariki(EAC) ama wazee wasiokuwa na uwezo ambao wanalazimika kununua madawa katika hospitali hukustahili yao ikiwa ni kupata matibabu bure.

  Kutokana na hali hiyo,tunakusudia kuwaalika wazee mbalimbali bila kujali itikadi na wananchiwote walioguswa na kadhia hii tufanye maandamano ya amani yenye lengo la kuunga mkono madai ya wafanyakazi na kulaani maneno ya Rais Kikwete/Ikulu na matendo ya walioitwa wazee wa Dar es salaam.

  Baraza la Wazee wa CHADEMA tunatumaini jeshi la polisi litapokea taarifa hii na kutupa ulinziunastahili kufanikisha tukio hili muhimu kwa demokrasia na maendeleo yanchi yetu.

  Mzee Erasto Sindila-0715220638/0755220638

  Mwenyekiti wa Mkoa wa Kinondoni Kanda Maalum DSM

  Nakala:
  • Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni
  • Katibu CHADEMA Mkoa wa Kinondoni
  • Wenyeviti CHADEMA Wilaya za Ubungo, Kawe na Kinondoni
  • Vyombo Vya Habari
   
 6. TzPride

  TzPride JF-Expert Member

  #6
  May 6, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 2,422
  Likes Received: 393
  Trophy Points: 180
  mmmh! hawa wazee kama ni rahisi kutmika hivi, basi nami nitatafuta wangu kadhaa, watakuwa wakiandamana au nawahutubia mtu/watu fulani wakiniudhi.
   
 7. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #7
  May 6, 2010
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Hii ilitakiwa kufanywa na VIONGOZI WA CHADEMA wa TAIFA. Nategemea siku hiyo watakuwepo. Mungu ibariki Tanzania.

  TUCTA lazima mfike hapo muwashukuru hawa wazee kwa kuwa na nyinyi. Msiseme zaidi.
   
 8. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #8
  May 6, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  okey Asanteni wazee wa CHADEMA , naona mmeamua kuonyesha ukweli kuwa wale hawakua wazee wa DSM, wale walikua mamluki wa CCM, waliookotwa mitaani, na inadaiwa walipewa Tsh 10,000 baada ya kazi ngumu yakushangilia.
   
 9. Lyangalo

  Lyangalo JF-Expert Member

  #9
  May 6, 2010
  Joined: Sep 10, 2009
  Messages: 681
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Kwa ninavyoielewa Tanzania sizani kama wataruhusiwa. Polisi watazuia kwa maelezo kwamba watahatarisha amani. Si mnajua wakuu wote wa polisi ni CCM!
   
 10. Eliphaz the Temanite

  Eliphaz the Temanite JF-Expert Member

  #10
  May 6, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,836
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Wazee wakiamka ujue kuna kitu haiendi sawa! Natumai vijana pia tutakuwa msitari wa mbele kuwaunga mkono wazee! Pia TUCTA naomba muendeleze hili vuguvugu maana we are not yet done!
   
 11. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #11
  May 6, 2010
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Sometimes we needs to use logic... the moment you politicize employee rights... you have actually nullfying all processes...

  CHADEMA Mulikuwepo siku zote hizo haki za wafanyakazi zimeanza leo?
   
 12. saitama_kein

  saitama_kein JF-Expert Member

  #12
  May 6, 2010
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 982
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Tunakwenda wapi jamani na hii CCM???
   
 13. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #13
  May 6, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  I have never heard such nonsense! Labour movement is part and parcel of politics. In our country our uhuru struggle was associated with labour movement (TFL etc). They played an important part. So was in South Africa- COSATU.
   
 14. M

  Mutu JF-Expert Member

  #14
  May 6, 2010
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hakuna kuchelewa ktk kufanya mambo mazuri, swala ni wanachosimamia wao wazee wa chadema ni sahihi au sio.
  By the way in respond kwa hotuba ya lrais kuhusu mgomo,je hiyo hotuba ilikuwepo miaka yote?
   
 15. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #15
  May 6, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Huyo Kasheshe huongozwa na ideology za itikadi wala si uelewa wa mambo alitaka hao wazee waandamane kupinga hotuba kabla ya hotuba yenyewe.
   
 16. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #16
  May 7, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Pumbaaaaaaaaaaaaaa
   
 17. D

  Dr Willibrod Slaa Verified User

  #17
  May 7, 2010
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 675
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 60
  Kasheshe,
  Dr. Slaa ni Katibu Mkuu wa Chadema. Si vema kusema kuwa Dr. Slaa alishupalia kama individual. Kila alichofanya Dr. Slaa amefanya kwa kuwa amepewa fursa na Chadema.Hivyo si rahisi kumtenganisha Dr. Slaa na Chadema isipokuwa kama unafanya hivyo kwa makusudi. Isitoshe, Sidhani kama umesikia kauli ya kupinga kutoka Chadema kuhusu yale aliyosema Dr. Slaa. Ni leo mmesikia kuwa Wazee wa Dar-Es-Salaam wamenyimwa kibali cha kuandamana kwa amani ili kuwaunga mkono Wafanyi kazi. Nadhani hoja ipo wazi kabisa kuwa Chadema imeweka msimamo na msimamo wa Chadema uko wazi kabisa katika swala la Wafanyi kazi. Nilisema pia swala la Wafanyikazi na mishahara si swala la ushabiki na siasa ni swala la uhai wa sehemu kubwa ya Taifa letu, japo Rais amesema hahitaji kura zao. Sina hakika kama Rais amefanya hesabu kuna kura ngapi nyuma ya Wafanyi kazi, na kwa kuwa yeye ametamka hivyo hadharani asitulaumu tukianza kuchambua hotuba yake hiyo kisiasa pia.
   
 18. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #18
  May 7, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  asante kwa kulitolea swala hilo Ufafanuzi,
  Kuhusu kunyimwa Kibali kwa Wazee wa CHADEMA, nnchi hii bado inawatendaji wanaojiona nao ni sehemu ya CCM, KISIASA.
  uTAONA wAZEE WALE WA TABORA WATARUHUSIWA KUMUUNGA MKONO KIKWETE, ila mageuzi yoyote huchukua muda msikate tamaa, waeleze wazee waombe tena Kibali,.
   
 19. D

  Dr Willibrod Slaa Verified User

  #19
  May 7, 2010
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 675
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 60
  Kasheshe,
  Naomba kama ulivyo makini ku posti hapa, chukua muda kidogo kupitia Hansard yaani Kumbukumbu rasmi ya Bunge. Kuna mahali muhimu zaidi pa kusemea? Soma Hotuba/mchango (kwa lugha ya Bunge) ya Dr. Slaa kwa Hotuba ya Waziri wa Utumishi 2006, 2007 kuhusu matabaka yanayojengeka katika Taifa letu kutokana na Gap kubwa kuhusu mishahara na mafao ya Watumishi wetu. Nimesema awali, Dr Slaa ni Katibu Mkuu wa Chadema, Bungeni amepelekwa na Chadema kwa Tiket ya Chadema. Ukiwa analysist mzuri nadhani utaelewa Tafsiri ya hali hiyo vizuri. Hivyo si sahihi kusema Chadema walikuwa wapi. Kama vile wewe mwenyewe hukutusikiliza hadi hali imekuwa mbaya na JK naye na Serikali yake hawakutusikiliza hivyo hivyo. Matokeo yake sasa ndio yanaonekana. Hatuna uwoga kuyatamka tunayotamka kwa sababu kazi yetu ya msingi ni kutetea haki za Wananchi wa Tanzania bila kujali itikadi yao, wala hali yao ya maisha wala vyeo vyao.
   
 20. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #20
  May 7, 2010
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,560
  Likes Received: 1,929
  Trophy Points: 280
  Mh Dr Slaa kumbuka kama ni siasa keshaziingiza lakini kwa makini,pale alipodai kuwa kuna watu nyuma ya Mgaya hata kama si kweli,amesha imply kuwa watu hao ni upinzani,na kwahiyo vitisho havikuwa kwa Mgaya tu,bali na wale anaodai "Wamemtuma"

  Mh Rais anajuwa mlishajipanga zamani,kwa mfano kauli yako ya kutaka mishahara na marupu rupu ya wabunge vipunguzwe ni kauli ambayo wafanyakazi hao wataipenda kwani inaonyesha kiongozi mwenye kujali maslahi ya wananchi,na si eti kuwaambia acheni kazi kama hamtaki,na huku kodi ya wananchi hao ndio inalimpa yeye na misafari yake kila kukicha!

  Lets wait and see ila ccm wanaogopa sana this time....Tunaomba Mungu nguvu kubwa isitumike ili kusiwe na umwagaji damu,hadi sasa wapinzani mmeonyesha upiganaji wabusara....Tusisahau wafanyakazi ndio nguzo kuu ya mbadiliko.
   
Loading...