MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,976
Ukweli husemwa:
Tanzania imeingia miaka ishirini (20) toka mageuzi makubwa ya kisiasa yalipoanziswa. Tumeshuhudia kufanyika chaguzi kuu tatu zikiambatana na chaguzi ndogo nyingi mbalimbali, na katika chaguzi zote, CCM imekuwa ikishinda kwa kura nyingi.
Nchi nyingi za kidemokrasia duniani, pamoja na kwamba chaguzi ndogo huwa siyo kipimo mahsusi cha hali ya kisiasa, lakini ni kipindi ambacho mara nyingi vyama vilivyoko madarakani huwa vinakuwa vimepunguza umaarufu kwa muda katika jamii kutokana na matatizo ya utendaji serikalini au mchakato katika utekelezaji wa ilani zake za uchaguzi. Kutokana na hili, mara nyingi huwa vinashindwa kwenye chaguzi ndogo. Hapa nchini imekuwa ni tofauti kwa sababu hata katika chaguzi ndogo, CCM imekuwa ikifanya vizuri pamoja na kuonekana machoni mwa jamii kuwa kimechoka au kuzeeka katika kusimamia maslahi ya wananchi wake.
Wiki hii tutashuhudia chaguzi ndogo zingine ambazo Wananchi wengi na wadadisi wa mambo ya kisiasa wanatumaini matokeo yatakuwa ni tofauti na miaka ya nyuma. Vyombo vingi vya habari na wananchi wengi wanatabiri vyama vya upinzani kushinda kwa kiwango cha juu katika kata nyingi nchini. Kama nilivyobainisha hapo juu, hakuna sababu kwa nini visishinde kwa kiwango hicho cha juu ikizingatiwa kuwa viongozi wengi na wanachama wa CCM hawakujihusisha ipasavyo katika kampeni nyingi kutokana na kuwepo kwa chaguzi za viongozi wao ndani ya chama. Kampeni za udiwani hazikupewa kipaumbele ndani ya CCM mwaka huu.
Kwa wapenda demokrasia ya kweli, haikubaliki hata kidogo kwa vyama vya upinzani kuendelea kufanya vibaya hata kwenye chaguzi ndogo wakati historia inabainisha kuwa ni lazima vifanye vizuri. Ninafikiri ni vizuri kwa viongozi wa vyama vyetu vya upinzani kutafakari na kuchukua maamuzi ya kuwajibika kwa kujiuzuru au kuwajibishwa ili kuwapisha wanachama wengine kuviongoza vyama kama matokeo katika chaguzi hizi ndogo yataendelea kuipa CCM ushindi zaidi.
Viongozi wetu wa kisiasa lazima waondoe hii dhana ya kuwa chama ni Baba na Mama yao na pia ni sehemu ya kuvuna tu mapato badala ya kuvuna wananchi na kukijenga chama kwa ufanisi. Hatuwezi kuendelea kujivuna kama tuna demokrasia nchini wakati vyama vya kisiasa haviendeshwi kwa demokrasia ya uwajibikaji na vingine vikizidi kudidimia huku viongozi wake wakijitajirisha na malipo kutoka kodi ya wananchi.
Nawasilisha...
UPDATES
Matokeo ya chaguzi ndogo zilizofanyika tarehe 28/10/2012
Viti vilivyokuwa wazi ni katika kata 29
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimeshinda kata 23 ni sawa na 79.3%
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeshinda kata 5 ni sawa na 17.2%
Tanzania Labour Party kimeshinda kata 1 ni sawa na 3.4%
angalizo:
Kwa sasa ni kipindi cha viongozi wa kisiasa wa vyama vya upinzani kutafakari na kupisha nguvu mpya ili ilisukume gurudumu la mabadiliko ya kisiasa kwa nguvu na mbinu mpya, kutokufanya hivyo ni kutowatendea haki wananchi wanaowaongoza.