Vyama vya Upinzani Kushindwa Katika Chaguzi Ndogo, Viongozi lazima Wawajibishwe

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,172
23,974
Ukweli husemwa:

Tanzania imeingia miaka ishirini (20) toka mageuzi makubwa ya kisiasa yalipoanziswa. Tumeshuhudia kufanyika chaguzi kuu tatu zikiambatana na chaguzi ndogo nyingi mbalimbali, na katika chaguzi zote, CCM imekuwa ikishinda kwa kura nyingi.

Nchi nyingi za kidemokrasia duniani, pamoja na kwamba chaguzi ndogo huwa siyo kipimo mahsusi cha hali ya kisiasa, lakini ni kipindi ambacho mara nyingi vyama vilivyoko madarakani huwa vinakuwa vimepunguza umaarufu kwa muda katika jamii kutokana na matatizo ya utendaji serikalini au mchakato katika utekelezaji wa ilani zake za uchaguzi. Kutokana na hili, mara nyingi huwa vinashindwa kwenye chaguzi ndogo. Hapa nchini imekuwa ni tofauti kwa sababu hata katika chaguzi ndogo, CCM imekuwa ikifanya vizuri pamoja na kuonekana machoni mwa jamii kuwa kimechoka au kuzeeka katika kusimamia maslahi ya wananchi wake.

Wiki hii tutashuhudia chaguzi ndogo zingine ambazo Wananchi wengi na wadadisi wa mambo ya kisiasa wanatumaini matokeo yatakuwa ni tofauti na miaka ya nyuma. Vyombo vingi vya habari na wananchi wengi wanatabiri vyama vya upinzani kushinda kwa kiwango cha juu katika kata nyingi nchini. Kama nilivyobainisha hapo juu, hakuna sababu kwa nini visishinde kwa kiwango hicho cha juu ikizingatiwa kuwa viongozi wengi na wanachama wa CCM hawakujihusisha ipasavyo katika kampeni nyingi kutokana na kuwepo kwa chaguzi za viongozi wao ndani ya chama. Kampeni za udiwani hazikupewa kipaumbele ndani ya CCM mwaka huu.

Kwa wapenda demokrasia ya kweli, haikubaliki hata kidogo kwa vyama vya upinzani kuendelea kufanya vibaya hata kwenye chaguzi ndogo wakati historia inabainisha kuwa ni lazima vifanye vizuri. Ninafikiri ni vizuri kwa viongozi wa vyama vyetu vya upinzani kutafakari na kuchukua maamuzi ya kuwajibika kwa kujiuzuru au kuwajibishwa ili kuwapisha wanachama wengine kuviongoza vyama kama matokeo katika chaguzi hizi ndogo yataendelea kuipa CCM ushindi zaidi.

Viongozi wetu wa kisiasa lazima waondoe hii dhana ya kuwa chama ni Baba na Mama yao na pia ni sehemu ya kuvuna tu mapato badala ya kuvuna wananchi na kukijenga chama kwa ufanisi. Hatuwezi kuendelea kujivuna kama tuna demokrasia nchini wakati vyama vya kisiasa haviendeshwi kwa demokrasia ya uwajibikaji na vingine vikizidi kudidimia huku viongozi wake wakijitajirisha na malipo kutoka kodi ya wananchi.

Nawasilisha...

UPDATES

Matokeo ya chaguzi ndogo zilizofanyika tarehe 28/10/2012

Viti vilivyokuwa wazi ni katika kata 29

Chama cha Mapinduzi (CCM) kimeshinda kata 23 ni sawa na 79.3%

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeshinda kata 5 ni sawa na 17.2%

Tanzania Labour Party kimeshinda kata 1 ni sawa na 3.4%

angalizo:

Kwa sasa ni kipindi cha viongozi wa kisiasa wa vyama vya upinzani kutafakari na kupisha nguvu mpya ili ilisukume gurudumu la mabadiliko ya kisiasa kwa nguvu na mbinu mpya, kutokufanya hivyo ni kutowatendea haki wananchi wanaowaongoza.

Mtoa mada Unaumwa au umetumwa!! Hakuna jingine kati ya hayo.
 
Wagonjwa wa akili si lazima wawe Mirembe tu..... Source: mimi mwenyewe babu Asprin a.k.a ODM.
 
Ukweli husemwa:

It's true, wagonjwa wa akili siyo lazima wawe hospitali kwa vile hata wewe au mimi tunaweza tukawa wagonjwa lakini tuko mitaani nyuma ya keyboard ya komputa.
Ukweli unasimama palepale. Viongozi wetu wa vyama vya upinzania katika miaka 20 bado hawajaviweka vyama katika hali mbadala ya kupambana na CCM ambayo pamoja na kuchoka kuongoza nchi bado wananchi wanakosa chama mbadala na viongozi makini wa kuwapatia nchi.

Wagonjwa wa akili si lazima wawe Mirembe tu..... Source: mimi mwenyewe babu Asprin a.k.a ODM.
 
Ukweli husemwa:

Tumekuwa na chaguzi kuu tatu na chaguzi ndogo nyingi tu ambazo pamoja na CCM kuchoka kuongoza lakini bado wananchi wanaipa kura. Kosa siyo wananchi kuipa CCM kura, Kosa ni viongozi wa vyama vya upinzani kushindwa kufanya kazi yao vizuri ili wananchi wawaamini na kuwapa uongozi wa nchi.

vyama gani vimeshindwa???? kwenye chaguzi zipi?????
 
Ukweli husemwa:

Tumekuwa na chaguzi kuu tatu na chaguzi ndogo nyingi tu ambazo pamoja na CCM kuchoka kuongoza lakini bado wananchi wanaipa kura. Kosa siyo wananchi kuipa CCM kura, Kosa ni viongozi wa vyama vya upinzani kushindwa kufanya kazi yao vizuri ili wananchi wawaamini na kuwapa uongozi wa nchi.

Baada ya maelezo yako yoote hayo ambayo sikuwa nayahitaji, sasa unaweza kujibu swali langu tafadhali?

Niliuliza hivi:

Vyama gani vimeshindwa ??????? Kwenye chaguzi zipi?????
 
Mtoa mada Unaumwa au umetumwa!! Hakuna jingine kati ya hayo.

mawazo ya mtu lazima yaheshimiwe ili kuleta usawa! Eti unaumwa au umetumwa! Maneno ya kijinga kama haya hayajengi kamwe bali kupandikiza chuki mioyoni mwa watu,sasa wewe mwenye mawazo bora tuambie ya kwako.Toa mambo yanayovutia watu na siyo upuuzi wa ku attack watu kwa sababu za kijinga.MUONE DR SLAA AKUELEKEZE WE FARAFATA
 
Ukweli husemwa:

Mkuu, Mbona nilikujibu.

Chaguzi kuu tatu, CCM bado iko madarakani.

Kama na chaguzi hizi ndogo CCM itashinda kwa kura nyingi basi viongozi wa Vyama vya upinzani lazima wawajibike.

Baada ya maelezo yako yoote hayo ambayo sikuwa nayahitaji, sasa unaweza kujibu swali langu tafadhali?

Niliuliza hivi:

Vyama gani vimeshindwa ??????? Kwenye chaguzi zipi?????
 
Ukweli husemwa:

Tumekuwa na chaguzi kuu tatu na chaguzi ndogo nyingi tu ambazo pamoja na CCM kuchoka kuongoza lakini bado wananchi wanaipa kura. Kosa siyo wananchi kuipa CCM kura, Kosa ni viongozi wa vyama vya upinzani kushindwa kufanya kazi yao vizuri ili wananchi wawaamini na kuwapa uongozi wa nchi.
Inatakiwa ufuatilie kwa ukaribu CCM imeshinda vipi, wewe ulitaka na vyama vya upinzani vinunue shahada za wapiga kura, kuna baadhi ya majina ya vijana hayajaonekana kwenye daftari la kura ulitaka viongozi wafanyeje ili hao vijana wapige kura.
Halafu ni chama kipi kimeshindwa katika chaguzi hizi CDM wamerudisha kata zao na kuipokonya CCM zingine, hivi huoni kama huo ni ushindi tosha?
 
Ukweli husemwa:

Mkuu, Mbona nilikujibu.

Chaguzi kuu tatu, CCM bado iko madarakani.

MsemajiUkweli

Ukweli ambao hujausema ni huu.
Kuwa CCM bado iko madarakani baada ya chaguzi(chafuzi) kuu tatu kwa sababu hata wenyewe wanasema kuwa wanashinda kwa ushindi wa kishindo na sio kwa kura.

Kishindo hapa unaweza kukitafsiri:
-Kubebwa na Katiba ambayo hakuna ambaye hajui kuwa katiba iliyopo ni kwa ajili ya kuibeba/kuibakisha madarakani CCM.

-Vyombo vya dola, polisi, usalama wa taifa, mahakama hazitekelezi majukumu yake kama vyombo vya taifa badala yake vinafanya kazi kama matawi ya CCM. Lengo ni kuibeba/kuibakisha CCM madarakani.

Lakini nakubaliana na wewe kuwa viongozi wa vyama vya upinzani wanapaswa kuwajibika.
Bado baada ya chaguzi(Chafuzi) kuu tatu hawajaona umuhimu wa kupigania kuwepo kwa tume ya uchaguzi uliyo huru.

Bado hawahakikishi vyombo vya dola vinafanya kazi kama vyombo vya nchi na sio kama vyombo vya chama.

Bado wanashiriki kwenye chaguzi (chafuzi) hizo.

Lakini wa kuwajibika hasa ni CCM na viongozi wa CCM(hata serikali wanasema ni serikali za CCM). Uvumilivu wa watanzania utafikia kikomo na hapo "amani ,mshikamano na utulivu" ambao CCM na serikali zake zinauchezea kama mwanaserere na wakisema kama asemavyo Pinda."Liwalo na Liwe" hatutazungumzia tena "kisiwa cha amani".

Mifano ya nchi jirani kama haitoshi kuwa fundisho kwetu; madhara yake, makovu yake huhitaji miaka kadha, miongo kadhaa kufutika. Katika CCM kama bado wamebaki walio weledi na wenye upeo wa kuona mbali walione hili na watuepushe kufika huko.
 
Sina budi pia kukubaliana nawe kwa hayo uliyoyasema. Ni kweli Vyombo vya dola, tume ya taifa ya uchaguzi na katiba ya nchi ziko kusaidia chama kilichoko madarakani badala ya kusimamia misingi na ukuaji wa demokrasia. Lakini kwa viongozi wa upinzani wa vyama vya siasa hii isiwe ndiyo sababu kuu kila kukicha wanayoitoa kwa wananchi pale wanaposhindwa katika chaguzi mbalimbali. Kama ndiyo hivyo, na kama ulivyoainisha, kwa nini basi wanaenda kwenye chaguzi wakati wanajua ni chaguzi chafu.

Hii sababu ya chaguzi chafu isiwe ndiyo kigezo cha viongozi wa vyama vya upinzani kuharalisha kuendelea kuongoza vyama, bali iwe ni changamoto ambayo wananchi wanategemea kama viongozi watakabiliana nayo.

CHADEMA kinaonekana angalau kupiga hatua kidogo mbele. Hata hivyo kwa wapenda demokrasia hii haitoshi. Kilitakiwa kwa sasa kiwe tayari ni chama hasa mbadala kutokana na udhaifu wa hali ya juu ulivyo ndani ya CCM na Serikali yake. Kuna vyama vya siasa toka vianzishwe miaka zaidi ya kumi na tano bado vina viongozi walewale miaka nenda, miaka rudi pamoja na kuzidi kudidimia kisiasa. Lazima viongozi wake wajue kuwa swala la kuwajibika sio la serikali na chama kilichoko madarakani peke yake, bali hata wao kwenye vyama vya upinzani kwa sababu tunawalipa pesa tukitegemea kututendea haki ya kidemokrasia.
 
Ukweli husemwa:

Tanzania imeingia miaka ishirini (20) toka mageuzi makubwa ya kisiasa yalipoanziswa. Tumeshuhudia kufanyika chaguzi kuu tatu zikiambatana na chaguzi ndogo nyingi mbalimbali, na katika chaguzi zote, CCM imekuwa ikishinda kwa kura nyingi.

Nchi nyingi za demokrasia duniani, pamoja na kwamba chaguzi ndogo huwa siyo kipimo mahsusi cha hali ya kisiasa katika chaguzi kuu nchini, lakini ni kipindi ambacho mara nyingi vyama vilivyoko madarakani huwa vinakuwa vimepunguza umaarufu kwa muda katika jamii kutokana na matatizo ya utendaji serikalini au mchakato katika utekelezaji wa ilani zake za uchaguzi. Hapa nchini imekuwa ni tofauti kwa sababu hata katika chaguzi ndogo, CCM ilikuwa ikafanya vizuri.

Wiki hii tutashuhudia chaguzi ndogo zingine ambazo Wananchi wengi na wadadisi wa mambo ya kisiasa wanatumaini matokeo yatakuwa ni tofauti na miaka ya nyuma. Vyombo vingi vya habari na wananchi wengi wanatabiri vyama vya upinzani kushinda kwa kiwango cha juu katika kata nyingi nchini. Kama nilivyobainisha hapo juu, hakuna sababu kwa nini visishinde kwa kiwango hicho cha juu ukichukulia kuwa viongozi na wanachama wa CCM hawakujihusisha ipasavyo katika kampeni nyingi kutokana na kuwepo kwa chaguzi za viongozi wao ndani ya chama. Kampeni za udiwani hazikupewa kipaumbele.

Kwa wapenda demokrasia ya kweli, haikubaliki hata kidogo kwa vyama vya upinzani kuendelea kufanya vibaya hata kwenye chaguzi ndogo wakati historia inabainisha kuwa ni lazima vifanye vizuri. Ninafikiri ni vizuri kwa viongozi wa vyama vyetu vya upinzani kutafakari na kuchukua maamuzi ya kuwajibika kwa kujiuzuru ili kuwapisha wanachama wengine kuviongoza vyama kama matokeo katika chaguzi hizi ndogo yataendelea kuipa CCM ushindi zaidi.

Viongozi wetu wa kisiasa lazima waondoe hii dhana ya kuwa chama ni Baba na Mama yao na pia ni sehemu ya kuvuna tu mapato badala ya kuvuna wananchi na kukijenga chama kwa ufanisi. Hatuwezi kuendelea kujivuna kama tuna demokrasia nchini wakati vyama vya kisiasa haviendeshwi kwa demokrasia ya uwajibikaji.

Nawasilisha...

Kwanini hao VIONGOZI wakishindwa WAWAJIBISHWE? Kwenye kila chamakinachokwenda kwenye UCHGUZI huwa inachagua PLATFORM zao; sasa ni kumaanish platform zilikuwa introduced hazikuneemesha CHAMA well kun njia zipasavyo kuondoa VIONGOZI; Sababu HOJA zinaweza zikawa nzuri kweli, ukaopewa Wewe Mwakilishi Ukashindwa kupanua HEKIMA zako kuonekana kama vile YOU OWN and SUCH STRATURGIES or we now leaders we dont understand act of POLITICS just tht arc to the act of siphonic the weath of mother nature.

Our leaders shines like flowers some with Education and some with no education but wealth to dream for...

So, Who will ever strict politicoi? Until U become part of them..."Revolution is not a dinner party, not an essay, nor a painting, nor a piece of embroidery; it cannot be advanced softly, gradually, carefully, considerately, respectfully, politely, plainly, and modestly." Just hold your heads Up with PRIDE

,
 
Ukweli husemwa:

No, I can't just hold my head up for something too little and the days still counting.

It's unbelievable pain to have almost 21 years of 'democratic politics' without responsible political leaders.

Kwa kukubali mwendo wa kuchechemea kisiasa ndiyo kukubali mwendo wa kuchechemea kimaendeleo wakati nchi zingine zinakimbia.

Viongozi wa siasa tumewaweka na tunawalipa ili watutendee haki ya kisiasa. Kushindwa kufanya hivyo na kuja na sababu ambayo miaka nenda, miaka rudi ni hiyohiyo ya kusema tumeshindwa kwa sababu ya chaguzi chafu ni kutowatendea haki wananchi kwa sababu kila uchaguzi ukitokea wanashiriki, wakishindwa wanakuja na sababu na kusema uchaguzi ulikuwa mchafu. Miaka yote sababu ni hiyo hiyo. Why, they haven't done something about it.

It's time for politician to held their hand up and admit they have failed people and resign or kicked out as leader.

Kwanini hao VIONGOZI wakishindwa WAWAJIBISHWE? Kwenye kila chamakinachokwenda kwenye UCHGUZI huwa inachagua PLATFORM zao; sasa ni kumaanish platform zilikuwa introduced hazikuneemesha CHAMA well kun njia zipasavyo kuondoa VIONGOZI; Sababu HOJA zinaweza zikawa nzuri kweli, ukaopewa Wewe Mwakilishi Ukashindwa kupanua HEKIMA zako kuonekana kama vile YOU OWN and SUCH STRATURGIES or we now leaders we dont understand act of POLITICS just tht arc to the act of siphonic the weath of mother nature.

Our leaders shines like flowers some with Education and some with no education but wealth to dream for...

So, Who will ever strict politicoi? Until U become part of them..."Revolution is not a dinner party, not an essay, nor a painting, nor a piece of embroidery; it cannot be advanced softly, gradually, carefully, considerately, respectfully, politely, plainly, and modestly." Just hold your heads Up with PRIDE

,
 
Naona umeamiua kumcopy MMM ili na wewe utoke! Kushindwa au kushinda ni relative na inategemea contestant aliingiaje mashindanoni. Mwanafunzi wa form4 anaye re seat akipata credit zake tatu ni muujiza mkubwa sana kwake wakati huohuo mwanafunzi wa marian girls akipata B masomo yote anaugua na anaweza kuhitaji counselling ili astabilize.

Kwa chaguzi hizi ndogo na mazingira yalivyo magumu kwa upinzani ni wazi kwamba malengo kwa ya upinzani hasa CDM yamefikiwa na pengine Yamezidi kwa maana wameover perform. Chaguzi ndogo huwa ni vita ya wakurugenzi na upinzani tena ya kufa na kupona...kuna ambao wanapoteza kazi kwa ccm kushindwa au hamyajui haya? Viongozi wa vijiji na mitaa kwa zaidi ya asilimia 90 bado ni ccm mpaka 2014 tutakapobadilisha. Poleni mnaodhani ccm imeshinda kwa kuwa inastahili...kinachoniuma zaidi ni kuona kodi yangu inatumika kwenda kuwahonga pombe na chumvi ndugu zangu walionisomesha..siwalaumu wananchi ila nailaumu serikali dhalimu kwa udhalimu wanaoufanya.
 
katika suala la uwajibikaji kila chama kinapaswa kuwajibika , lakini zaidi yule aliyepoteza. Yupi wakupongezwa aliyepiga hatua mbele au aliyerudi nyuma. aliyerudi nyuma hata kwa nusu hatua ana mapungufu makubwa.

Tukilinganisha na mwaka 2010 je wapinzani wameongeza kura zozote au zimepungua ?

Tafakari ya kina na msingi bado Tanzania hatujawa na uwanja wa siasa ulio sawa kwa vyama vyote. Vyombo vya dola, tume ya uchaguzi, epa, kagoda, fadha za Uswisi nk. bado vimekumbatia chama tawala. Tadhimini makini na ya haki inabidi kuangalia mambo mengi sana na si vijimambo vichache.
 
Kwa mtazamo wangu ni kuwa upinzani hasa CDM wanahitaji pongezi nyingi sana maana ni ukweli kuwa CCM inatumia nguvu na ghiriba kubwa kuhakikisha kuwa wanashinda chaguzi hizi ndogo kwa kutisha wananchi ambao bado uelewa wao ni mdogo, kukataa kuboresha daftari la wapiga kura ambalo ndiyo kifo cha CCM.

Huu ni mwanzo mzuri subiri 2015 utaona nini kitatokea maana magamba wanazidi kutokota.
 
Ukweli husemwa:

Tanzania imeingia miaka ishirini (20) toka mageuzi makubwa ya kisiasa yalipoanziswa. Tumeshuhudia kufanyika chaguzi kuu tatu zikiambatana na chaguzi ndogo nyingi mbalimbali, na katika chaguzi zote, CCM imekuwa ikishinda kwa kura nyingi.

Nchi nyingi za kidemokrasia duniani, pamoja na kwamba chaguzi ndogo huwa siyo kipimo mahsusi cha hali ya kisiasa, lakini ni kipindi ambacho mara nyingi vyama vilivyoko madarakani huwa vinakuwa vimepunguza umaarufu kwa muda katika jamii kutokana na matatizo ya utendaji serikalini au mchakato katika utekelezaji wa ilani zake za uchaguzi. Kutokana na hili, mara nyingi huwa vinashindwa kwenye chaguzi ndogo. Hapa nchini imekuwa ni tofauti kwa sababu hata katika chaguzi ndogo, CCM imekuwa ikifanya vizuri.

Wiki hii tutashuhudia chaguzi ndogo zingine ambazo Wananchi wengi na wadadisi wa mambo ya kisiasa wanatumaini matokeo yatakuwa ni tofauti na miaka ya nyuma. Vyombo vingi vya habari na wananchi wengi wanatabiri vyama vya upinzani kushinda kwa kiwango cha juu katika kata nyingi nchini. Kama nilivyobainisha hapo juu, hakuna sababu kwa nini visishinde kwa kiwango hicho cha juu ikizingatiwa kuwa viongozi wengi na wanachama wa CCM hawakujihusisha ipasavyo katika kampeni nyingi kutokana na kuwepo kwa chaguzi za viongozi wao ndani ya chama. Kampeni za udiwani hazikupewa kipaumbele ndani ya CCM mwaka huu.

Kwa wapenda demokrasia ya kweli, haikubaliki hata kidogo kwa vyama vya upinzani kuendelea kufanya vibaya hata kwenye chaguzi ndogo wakati historia inabainisha kuwa ni lazima vifanye vizuri. Ninafikiri ni vizuri kwa viongozi wa vyama vyetu vya upinzani kutafakari na kuchukua maamuzi ya kuwajibika kwa kujiuzuru au kuwajibishwa ili kuwapisha wanachama wengine kuviongoza vyama kama matokeo katika chaguzi hizi ndogo yataendelea kuipa CCM ushindi zaidi.

Viongozi wetu wa kisiasa lazima waondoe hii dhana ya kuwa chama ni Baba na Mama yao na pia ni sehemu ya kuvuna tu mapato badala ya kuvuna wananchi na kukijenga chama kwa ufanisi. Hatuwezi kuendelea kujivuna kama tuna demokrasia nchini wakati vyama vya kisiasa haviendeshwi kwa demokrasia ya uwajibikaji na vingine vikizidi kudidimia huku viongozi wake wakijitajirisha na malipo kutoka kodi ya wananchi.

Nawasilisha...

UPDATES

Matokeo ya chaguzi ndogo zilizofanyika tarehe 28/10/2012

Viti vilivyokuwa wazi ni katika kata 29

Chama cha Mapinduzi (CCM) kimeshinda kata 23 ni sawa na 79.3%

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeshinda kata 5 ni sawa na 17.2%

Tanzania Labour Party kimeshinda kata 1 ni sawa na 3.4%

angalizo:

Kwa sasa ni kipindi cha viongozi wa kisiasa wa vyama vya upinzani kutafakari na kupisha nguvu mpya ili ilisukume gurudumu la mabadiliko ya kisiasa kwa nguvu na mbinu mpya, kutokufanya hivyo ni kutowatendea haki wananchi wanaowaongoza.

Kabla ya hukumu yako unayoitaka, utujuze ni chama gani kimepoteza kata zake za awali. Ukifanya hivyo kesi yako itapata hukumu nzuri maana kata zilizokuwa wazi ni 29 ambazo zilikuwa zipo mikononi mwa chama kipi na sasa imekuwaje. Demokrasia siyo CCM ikigombea ishindwe kabisa au CUF ikigombea ndiyo ishinde kila chaguzi. Hatuendi hivyo mzee.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom