Vyama vya Siasa vyaombwa kuwasilisha Mapendekezo ya Utungwaji wa Sheria ya Uchaguzi

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,377
8,121
Vyama vya Siasa nchini vimeombwa kuwasilisha maoni au mapendekezo yanayohusu mchakato wa utungaji Sheria mpya za uchaguzi na marekebisho ya Sheria zinazosimamiwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa

Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa kwa Makatibu Wakuu wa Vyama vya Siasa vyote vyenye usajili wa kudumu,kila Chama cha Siasa kimeombwa kuwasilisha maoni au mapendekezo yake kwenye Ofisi hiyo kwa maandiashi ili kufanikisha zoezi hilo

Taarifa hiyo iliyosainiwa na Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa Sisty Nyahoza kwa niaba ya Msajili wa Vyama hivyo Jaji Francis Mutungi imebainisha kuwa hatua hiyo inakuja kufuatia mapendekezo yaliyowasilishwa na Kikosi Kazi kilichoratibu maoni ya wadau yanayohusu Demokrasia ya Vyama vingi vya Siasa nchini na wadau wengine wa Demokrasia ya Vyama vingi vya Siasa

Sheria zinazoangaziwa kwenye suala hilo ni pamoja na Sheria mpya ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Sheria mpya ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani, Marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa, Sura 258 pamoja na Marekebisho ya Sheria ya gharama za Uchaguzi, Sura 278, ambapo Vyama vya Siasa vimepewa hadi Julai 20.2023 kukamilisha zoezi hilo.
 
Tumewasubiria cdm wapeleke mapendekezo Yao.
 
Back
Top Bottom