Vyama visivyo na wabunge, Magufuli umevifuta?

Kuna tatizo kubwa sana kwa malezi ya wana CCM. Sisi wengine ambao tulipata bahati ya kuwa huko wakati wa enzi ya chama kimoja na mwanzoni mwa mfumo wa vyama vingi tunajua jinsi mambo yanavyoendeshwa. Kuna wakati Mrema alikuwa ana Nguvu sana za kisiasa hapa nchini na akaungwa mkono na Askofu Zacharia Kakobe.

Kakobe aliamua kumsaidia kufanya mikutano. Alipofika kwenye wilaya fulani ili afanye mkutano, aliyekuwa Mkuu wa Wilaya wa eneo hilo alipewa maagizo mawili mahsusi. La kwanza azuie Kakobe asifanye mkutano wake, lakini la pili ahahakikishe jimbo alimo yeye alichukuliwi na Upinzani, wakati huo ikimaanishwa TLP.

Alichofanya Mkuu yule wa wilaya ni kutafuta kundi kubwa la vijana ili kufanya vurugu kwenye mkutano ule wa Kakobe kwa hakikisho kwamba hawatakamatwa na Polisi na hata wakikamatwa hawatafunguliwa Mashitaka. Kilichotokea ni kuvurugwa kwa mkutano wa Kakobe na wavurugaji mbele ya Polisi bila ya kufanywa chochote na Polisi waliokuwepo eneo la tukio.

Ndani ya CCM kuna hofu kubwa sana ya kutolewa madarakani kulikoni hofu yao ya kushindwa kuendeleza nchi. Chama cha siasa haimaniishi Serikali za mitaa, wabunge au Rais, bali ni zaidi ya hapo. Kwa mfano mwenyekiti wa taifa wa chama anazuiwaje kufanya mikutano nchi nzima?

Unaposema wakafanye mikutano kule walikochaguliwa si pamoja na Dar es salaam? Sasa kama wabunge wa CHADEMA/UKAWA wanataka kufanya mkutano wao Jangwani na kuwaalika viongozi wao wa kitaifa wanaruhusiwa? Yeye kule ambako hakupata kura nyingi zaidi ya zile za Lowassa hatakwenda kufanya mikutano?

Ina maana yeye hatakiwi kufanya mikutano mkoa wa Arusha, Mbeya mjini, Iringa Mjini na kwingineko ambako Tume ya uchaguzi ilisema ameshindwa? Kama wengine wanatakiwa kufanya mikutano kule tu walikochaguliwa basi na yeye ni marufuku kufanya mikutao kule ambako hakuchaguliwa!!
 
unaweza ukute hao watu wanamshauri vizuri tu ila makufuli kama mnavyo mfahamu ni mtu anaependa kukaidi na kufanya kinyume na alivyo elekezwa na katiba kwa ujumla.
 
"Kila mtu afanye mkutano wa siasa sehemu aliyochaguliwa" by JPM
Bwana mkubwa ana kauli tata kweli! Ina maana vile vyama ambavyo havina wabunge nchini ndio anavifuta? Kwa sheria gani? Au sehemu iliyochaguliwa ccm vyama vingine vitajijengaje bila mikutano ya kujitangaza?
Anachotaka kutuambia mahali kama Arusha mjini CCM wafunge kabisa ofisi zao maana hawakuchaguliwa na hawawezi kufanya mikutano kwa amri ya mkuu?
Nadhani ni wakati wa kuwajua kwa uwazi kabisa majina ya Washauri wa Siasa na Uchumi wa Rais maana yaweza kuwa wanampotosha ili aharibikiwe.
Yaweza kuwa anamshauri wa siasa mwana Ukawa hivyo anampoteza ili aharibikiwe na kudharauliwa kama sasa.
mkuu anatumia nguvu nyingi kupambana na upinzani anadhani ndo atapendwa na wananchi, ukweli nikuwa hatumpemdi na tunamdharau
 
CCM inashika mitaa zaidi ya sabini huko Arusha ...

CCM imefanya chaguzi zake za ndani bila maandamano.

Zitto badala ya kwenda kuhamasisha kigoma kila kukicha yuko facebook.

Mbowe anasubiri 2020 aende HAI kupeleka ambulance second hand ya kuwazugia wananchi.

Lissu yuko busy kumtukana Rais wakati jimboni kwake watoto wanakaa chini.

Mnyika anapeleka kesi yakuomba kuonekana live wakati Kibamba hamna maji.

JPM asipokuwa makini hata mambo mazuri anayotaka kufanya yatamletea balaa. Hakuna nchi inayoweza kuendelea kwa kubana demokrasia. Wengi tunaamini ana nia njema, lakini kutuchukulia watanzania wote kama watoto wachanga au punguani hakumjengei hekima bali ukali wa woga. Kwanini uwaogope wapinzani kiasi hiki? Ungejuaje umeshinda uchaguzi wa kweli na wa haki bila kuhesabu kura za ndiyo na za hapana? Futeni vyama vya upinzani, tangazeni wazi tu, kwamba uchaguzi ujao watakaohusika ni wa chama kimoja, chama chenu tu. Dunia inawashangaa, kupambana na watu wenu wenyewe wasio na silaha! Muwambie wazi wananchi waliojiunga na vyama vya upinzani kwamba wote ni wapumbavu. Kwasababu wameiamini Katiba ya nchi inayowaruhusu kufanya hivyo. Kisha hata hiyo Katiba yenyewe watangazieni wazi kwamba ni batili. Vinginevyo kwanini mnaoiogapa? Lakini sio ndiyo imewapa madaraka kwa amani bila rungu? Sasa rungu la nini? Epusheni shari na kiu ya kumwaga damu za ndugu zenu. Mtazikosa baraka za Mungu zilizowapa mamlaka.
 
"Kila mtu afanye mkutano wa siasa sehemu aliyochaguliwa" by JPM
Bwana mkubwa ana kauli tata kweli! Ina maana vile vyama ambavyo havina wabunge nchini ndio anavifuta? Kwa sheria gani? Au sehemu iliyochaguliwa ccm vyama vingine vitajijengaje bila mikutano ya kujitangaza?
Anachotaka kutuambia mahali kama Arusha mjini CCM wafunge kabisa ofisi zao maana hawakuchaguliwa na hawawezi kufanya mikutano kwa amri ya mkuu?
Nadhani ni wakati wa kuwajua kwa uwazi kabisa majina ya Washauri wa Siasa na Uchumi wa Rais maana yaweza kuwa wanampotosha ili aharibikiwe.
Yaweza kuwa anamshauri wa siasa mwana Ukawa hivyo anampoteza ili aharibikiwe na kudharauliwa kama sasa.
Pasco alituonya na kutuusia.....
 
Kwa hiyo sendeka atahutubia wapi.

Swali la msingi sana. Nadhani hata Kinana anajiuliza huyu mtu ni wa aina gani? Na kwa nini rafiki yake Kikwete hakumshtua kukataa huo ukatibu mkuu kama yeye JK alivyotangaza kuwa hataki kabisa kuombwa ushauri wowote kwenye chama au serikali?
 
Kumbe JK alitangaza hivyo? Ila ngosha atafeli vibaya sana kwenye utawala wake, ni kheri angekuwa dikteta wa kimya kimya
 
Karibu Nduli IDD Amin dadaa Tanzania Mali yako chochote unachotaka Fanya lakini roho zetu tuachie
 
Karibu Nduli IDD Amin dadaa Tanzania Mali yako chochote unachotaka Fanya lakini roho zetu tuachie
 
CCM inashika mitaa zaidi ya sabini huko Arusha ...

CCM imefanya chaguzi zake za ndani bila maandamano.

Zitto badala ya kwenda kuhamasisha kigoma kila kukicha yuko facebook.

Mbowe anasubiri 2020 aende HAI kupeleka ambulance second hand ya kuwazugia wananchi.

Lissu yuko busy kumtukana Rais wakati jimboni kwake watoto wanakaa chini.

Mnyika anapeleka kesi yakuomba kuonekana live wakati Kibamba hamna maji.
sasa wewe maada inayojadiliwa unaingiza mambo ya kimagumashi uelewekeje.. Jambo la msingi ni position ya vyama ambavyo havina wabunge havina haki ya kujitangaza kuendana na kauli ya magu?? mmezoea mizaha sana na mtanyooshwa tu na Magu.. mmekaa kupata vya bure kwa kupost uharo badala ya kuwa cretical thinker.. Magu kasema asiyefanya kazi na asile na wewe hii sio kazi ni ungese.. maana huwezi acha hoja ya msing unaparamia watu wengine na hija za kiharo.. wenzako wanafanya kazi na wana akili kushinda mnaowadhani.. think tank lazima amshauri rais sio kukosoa wanaomshauri kwa wema.. Other wize you reflects your avatar. Mikutano ni haki ya wote provided hawavunji amani. na wasiruhusu polisi kuatend..
 
"Kila mtu afanye mkutano wa siasa sehemu aliyochaguliwa" by JPM
Bwana mkubwa ana kauli tata kweli! Ina maana vile vyama ambavyo havina wabunge nchini ndio anavifuta? Kwa sheria gani? Au sehemu iliyochaguliwa ccm vyama vingine vitajijengaje bila mikutano ya kujitangaza?
Anachotaka kutuambia mahali kama Arusha mjini CCM wafunge kabisa ofisi zao maana hawakuchaguliwa na hawawezi kufanya mikutano kwa amri ya mkuu?
Nadhani ni wakati wa kuwajua kwa uwazi kabisa majina ya Washauri wa Siasa na Uchumi wa Rais maana yaweza kuwa wanampotosha ili aharibikiwe.
Yaweza kuwa anamshauri wa siasa mwana Ukawa hivyo anampoteza ili aharibikiwe na kudharauliwa kama sasa.
Msiwasingizie washauri kazi yao ni kushauri tu maamuzi anayafanya muhusika so lawama zote ziende kwa mpokea ushauri a.k.a his holiness
 
Mshauri wake anaweza kuwa nape.
Naona ni Jaji Mutungi, maana ameacha kazi ya uleaji wa vyama na sasa amekuwa msaidizi wa Ccm.
Maana matamko kama haya ambayo yako kinyume na sheria ya vyama vingi angeshayatolea maelezo.
Sasa anamsaidia msemaji mmoja wa chama ambae hakupata cheti cha form six kukandamiza upinzani badala ya kuvilea.
 
CCM inashika mitaa zaidi ya sabini huko Arusha ...

CCM imefanya chaguzi zake za ndani bila maandamano.

Zitto badala ya kwenda kuhamasisha kigoma kila kukicha yuko facebook.

Mbowe anasubiri 2020 aende HAI kupeleka ambulance second hand ya kuwazugia wananchi.

Lissu yuko busy kumtukana Rais wakati jimboni kwake watoto wanakaa chini.

Mnyika anapeleka kesi yakuomba kuonekana live wakati Kibamba hamna maji.
JPM anazuia siasa wakati Hai, Kigoma mjini, Singida Mashariki na Kibamba ameshindwa kupeleka huduma ulizotaja
 
Naona ni Jaji Mutungi, maana ameacha kazi ya uleaji wa vyama na sasa amekuwa msaidizi wa Ccm.
Maana matamko kama haya ambayo yako kinyume na sheria ya vyama vingi angeshayatolea maelezo.
Sasa anamsaidia msemaji mmoja wa chama ambae hakupata cheti cha form six kukandamiza upinzani badala ya kuvilea.
Mkuu umelenga penyewe bila ya kupepesa macho. Yaani kwa maneno ya utu uzima ni kwamba umewavua nguo mchana kweupe.
 
Back
Top Bottom