Vyama visivyo na wabunge, Magufuli umevifuta?

CCM inashika mitaa zaidi ya sabini huko Arusha ...

CCM imefanya chaguzi zake za ndani bila maandamano.

Zitto badala ya kwenda kuhamasisha kigoma kila kukicha yuko facebook.

Mbowe anasubiri 2020 aende HAI kupeleka ambulance second hand ya kuwazugia wananchi.

Lissu yuko busy kumtukana Rais wakati jimboni kwake watoto wanakaa chini.

Mnyika anapeleka kesi yakuomba kuonekana live wakati Kibamba hamna maji.
Hayo yote uliyosema sii ndiyo aliahidi magu kwa nchi nzima? Mwache naye azunguke aeleze na wengine watazunguka.
Tumegundua anaye mpoteza huyu jamaa ni nyie ndani ya chama chenu mnaojikita katika kujipendekeza kwa kila asemalo kumsifia bila kukosoa makosa
 
"Kila mtu afanye mkutano wa siasa sehemu aliyochaguliwa" by JPM
Bwana mkubwa ana kauli tata kweli! Ina maana vile vyama ambavyo havina wabunge nchini ndio anavifuta? Kwa sheria gani? Au sehemu iliyochaguliwa ccm vyama vingine vitajijengaje bila mikutano ya kujitangaza?
Anachotaka kutuambia mahali kama Arusha mjini CCM wafunge kabisa ofisi zao maana hawakuchaguliwa na hawawezi kufanya mikutano kwa amri ya mkuu?
Nadhani ni wakati wa kuwajua kwa uwazi kabisa majina ya Washauri wa Siasa na Uchumi wa Rais maana yaweza kuwa wanampotosha ili aharibikiwe.
Yaweza kuwa anamshauri wa siasa mwana Ukawa hivyo anampoteza ili aharibikiwe na kudharauliwa kama sasa.
Mbowe kuandamana jimbo la hai usiku na mchana ili kudumisha democrasia ni kinyume cha katiba ??

Mbowe njoo Moshi ,tuandamane , maana ndio ulichotuahidi wakati wa uchaguzi kwamba ukishinda utatuletea maandamano.

Tunahitaji maandamano
 
Chama hakijengwi kwa maandamano
Asante kwa kuelewa ni kweli chama hakijengwi kwa maandamano bali kinajengwa kwa kufanya mikutano sehemu tofauti tofauti ili kueneza sera zao na kupata kuungwa mkono na kila kaya,kata,wilaya,mkoa na taifa kwa ujumla.

Kwa hesabu zenu ccm mmepotoka kwa hili.
 
CCM inashika mitaa zaidi ya sabini huko Arusha ...

CCM imefanya chaguzi zake za ndani bila maandamano.

Zitto badala ya kwenda kuhamasisha kigoma kila kukicha yuko facebook.

Mbowe anasubiri 2020 aende HAI kupeleka ambulance second hand ya kuwazugia wananchi.

Lissu yuko busy kumtukana Rais wakati jimboni kwake watoto wanakaa chini.

Mnyika anapeleka kesi yakuomba kuonekana live wakati Kibamba hamna maji.
Kweli Wejingalao... akiruhusu mtarudi kuja hapa kusifia.. hv nyie watu wa lumumba kwa ujumla wenu huwa mnafikiri kwa kutumia nn? [emoji15] [emoji780]
 
Wakati mwangine hawa watu kufikiri nje ya Box ni pagumu!!!!!!! Kuna Umuhimu wa mtu akitaka Kuwa Rais awe angalau amewah kupitia Coz za Political Science ili Kuwa na uelewa mpana wa mambo ya ki Taifa na Kimataifa!!!!!! Ivo tu yan
 
"Kila mtu afanye mkutano wa siasa sehemu aliyochaguliwa" by JPM
Bwana mkubwa ana kauli tata kweli! Ina maana vile vyama ambavyo havina wabunge nchini ndio anavifuta? Kwa sheria gani? Au sehemu iliyochaguliwa ccm vyama vingine vitajijengaje bila mikutano ya kujitangaza?
Anachotaka kutuambia mahali kama Arusha mjini CCM wafunge kabisa ofisi zao maana hawakuchaguliwa na hawawezi kufanya mikutano kwa amri ya mkuu?
Nadhani ni wakati wa kuwajua kwa uwazi kabisa majina ya Washauri wa Siasa na Uchumi wa Rais maana yaweza kuwa wanampotosha ili aharibikiwe.
Yaweza kuwa anamshauri wa siasa mwana Ukawa hivyo anampoteza ili aharibikiwe na kudharauliwa kama sasa.

BAVICHA uelewe kuwa vyama havifutwi isipokuwa msifanye fujo na maandamano yenu sehemu ambako watu wametulia wanafanya kazi. Mbona Hai maandamano yenu huwa hayafanyiki?
 
Maandamo ni mojawapo ya mbinu ya mnyonge kupaza sauti kwa watala waliojaa kiburi na jeuri waliopoka haki,usawa na ustawi wa demkrasia. Kama kusingekuwa na zuio la mikutano ya kisiasa usingeona wala kusikia swala la maandamano.

Hayo mengine ni porojo na propaganda chafu tu.
 
Hayo yote uliyosema sii ndiyo aliahidi magu kwa nchi nzima? Mwache naye azunguke aeleze na wengine watazunguka.
Tumegundua anaye mpoteza huyu jamaa ni nyie ndani ya chama chenu mnaojikita katika kujipendekeza kwa kila asemalo kumsifia bila kukosoa makosa
Magufuli anatekeleza aliyoyaahidi nyie mnaenda kuandamana kudai bunge live...je mliahidi bunge live?
 
Hata kama anashauriwa rais ni nafasi kubwa anatakiwa,achanganye na zake...ajiongeze
Mkuu hii habari ya za kuambiwa changanya na zako.ina maana kubwa kuliko tunavyofikiri. Kama huna za kuchanganya unachanganya na nini? Unashauriwa jambo la kitaalamu ambao wewe huo utaalamu huna, unachanganya na wako upi? Ndio maana rais ni taasisi!
 
BAVICHA uelewe kuwa vyama havifutwi isipokuwa msifanye fujo na maandamano yenu sehemu ambako watu wametulia wanafanya kazi. Mbona Hai maandamano yenu huwa hayafanyiki?
Hivi hiyo dhana ya kuwa maandamano ni fujo imeanzia wapi? Mbona yapo maandamano ya aina nyingi na hayana fujo? Siku zote fujo zinatokea kutokana na Polisi kuingilia kati bila sababu yeyote
 
CCM inashika mitaa zaidi ya sabini huko Arusha ...

CCM imefanya chaguzi zake za ndani bila maandamano.

Zitto badala ya kwenda kuhamasisha kigoma kila kukicha yuko facebook.

Mbowe anasubiri 2020 aende HAI kupeleka ambulance second hand ya kuwazugia wananchi.

Lissu yuko busy kumtukana Rais wakati jimboni kwake watoto wanakaa chini.

Mnyika anapeleka kesi yakuomba kuonekana live wakati Kibamba hamna maji.
Huna hoja madhaifu unayoyaona ktk majimbo yanayoongozwa na wabunge wa UKAWA yametokana na serikali za mitaa na kuu za Ccm,

Wabunge wetu wasiposemea wananchi unataka nani aseme ??!! Tumia hicho kichwa vizuri
 
Back
Top Bottom