Mabibi na mabwana vyama kufukuza watu tangu lini imekuwa habari kubwa hadi vyama mahasimu kushadadia kwa mbinde namna hii?
Kila chama kina taratibu zake ambazo wanachama wanalazimika kuzifuata au kushawishi vinginevyo kwa hoja. Kwa kuzikiuka zinamuweka awaye yote kunako mlango wa kutokea kwa hiari au kwa Shuruti.
Hakuna mageni kwenye haya. Si kwa CCM, CUF, CHADEMA, ODM, JUBILEE, nk. Leo mimi kesho wewe. Unataka kubakia kwenye chama, zipo taratibu za kufuata ambapo kila mwanachama anao uhuru wa kuamua kusuka au kunyoa.
Kachero mbobezi baada ya mahojiano na kamati ile alisikika akisema, walikuwa na mazungumzo mazuri, wakashauriana vizuri mambo ya kitaifa na kimataifa, akamalizia kwa kwenda kupata chakula kizuri kwenye hoteli isiyojulikana.
Pamoja na yote alionyeshwa mlango wa kutokea naye bila hiana akautumia. Bahati mbaya zaidi kwake hata lile goli lake la dak ya 89 nalo likawa si riziki.
Kwamba Bi Halima na wenziwe kwa hili la kwenda kuapishwa bila ya ridhaa ya chama chao huo ni usaliti. Kwa huo, wameonyeshwa mlango wa kutokea.
Kwani wao walitegemea pongezi? Ya kwamba pana chama na vyombo vyake wanakomaa kwamba wasifukuzwe? Kwani CCM wao ni nani kwenye hili? Wamekuwa na uchungu na mtoto kuliko mama yake? Si kuwa labda hawa ni mafataki tu?
Kwani trespassing maana yake nini? Mbona Membe walipomfukuza hakuna chama kilichoingilia au kuhoji? Mmekuwa mashabiki, walinzi na facilitators wa wasaliti wetu? Wachawi watakuwa nani basi kama siyo nyie?
Kwao hawa waliokuwa wanachama CHADEMA, kwa kuweka maslahi ya taifa hili mbele, sana sana saidieni kuonyesha wahusika kamili wa ghushi hii. Hiyo ni jinai na ni mbaya sana kwa mustakabala wa taifa letu.
Mengine yote, hapa tulipo ni historia na kujilisha upepo tu. Kwa hekima kubwa mlango wa kurejea kwenu haujafungwa na kufuli. Bado mnaweza kuutumia mkitaka.
Kuvunjika kwa koleo si mwisho wa uhunzi.
Aluta continua!