Vyama kufukuza watu, mbona Kachero alifukuzwa?

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
14,906
2,000
Mabibi na mabwana vyama kufukuza watu tangu lini imekuwa habari kubwa hadi vyama mahasimu kushadadia kwa mbinde namna hii?

Kila chama kina taratibu zake ambazo wanachama wanalazimika kuzifuata au kushawishi vinginevyo kwa hoja. Kwa kuzikiuka zinamuweka awaye yote kunako mlango wa kutokea kwa hiari au kwa Shuruti.

Hakuna mageni kwenye haya. Si kwa CCM, CUF, CHADEMA, ODM, JUBILEE, nk. Leo mimi kesho wewe. Unataka kubakia kwenye chama, zipo taratibu za kufuata ambapo kila mwanachama anao uhuru wa kuamua kusuka au kunyoa.

Kachero mbobezi baada ya mahojiano na kamati ile alisikika akisema, walikuwa na mazungumzo mazuri, wakashauriana vizuri mambo ya kitaifa na kimataifa, akamalizia kwa kwenda kupata chakula kizuri kwenye hoteli isiyojulikana.

Pamoja na yote alionyeshwa mlango wa kutokea naye bila hiana akautumia. Bahati mbaya zaidi kwake hata lile goli lake la dak ya 89 nalo likawa si riziki.

Kwamba Bi Halima na wenziwe kwa hili la kwenda kuapishwa bila ya ridhaa ya chama chao huo ni usaliti. Kwa huo, wameonyeshwa mlango wa kutokea.

Kwani wao walitegemea pongezi? Ya kwamba pana chama na vyombo vyake wanakomaa kwamba wasifukuzwe? Kwani CCM wao ni nani kwenye hili? Wamekuwa na uchungu na mtoto kuliko mama yake? Si kuwa labda hawa ni mafataki tu?

Kwani trespassing maana yake nini? Mbona Membe walipomfukuza hakuna chama kilichoingilia au kuhoji? Mmekuwa mashabiki, walinzi na facilitators wa wasaliti wetu? Wachawi watakuwa nani basi kama siyo nyie?

Kwao hawa waliokuwa wanachama CHADEMA, kwa kuweka maslahi ya taifa hili mbele, sana sana saidieni kuonyesha wahusika kamili wa ghushi hii. Hiyo ni jinai na ni mbaya sana kwa mustakabala wa taifa letu.

Mengine yote, hapa tulipo ni historia na kujilisha upepo tu. Kwa hekima kubwa mlango wa kurejea kwenu haujafungwa na kufuli. Bado mnaweza kuutumia mkitaka.

Kuvunjika kwa koleo si mwisho wa uhunzi.

Aluta continua!
 
Tigershark

JF-Expert Member
Oct 9, 2018
7,095
2,000
Lipumba alifukuza wabunge 8 wa viti maalumu,Ndugai alikuwa India akipata matibabu!Lakini haraka haraka siku hiyo hiyo aliandika barua kwa NEC kuwaeleza kuwa nafasi 8 ziko wazi na ndio ukawa mwisho wa wale viti maalumu!Walipinga mahakamani bila mafanikio!
Ndugai mbona hakuwatetea hao viti maalumu 8?Au kwakuwa walikuwa na maslahi na Lipumba ndio maana akawatosa hao viti maalumu?
Akina Halima Mdee wamekosa sifa za kuwa wabunge baada ya kufutwa uanachama!
 
adolay

JF-Expert Member
Dec 8, 2011
12,064
2,000
CCM ilimfukuza BERNARD KAMILIUS MEMBE

1. Bila kufuata utaratibu/katiba ya ccm

2. Bila kufuata matakwa ya katiba ya nchi

Ila tu asigombee urais

1. Msajili wa vyama kimyaa

2. Mwanasheria mkuu wa serikali kimyaa

3. Vyombo vya dola kimyaaa

Cha ajabu ikiwa Chadema baasi kila mwenye videvu atainua gongo lake ilimradi kuwajeruhi cdm..... japo cdm siku zote wanazingatia sheria kanuni na taratibu.

Tanzania tunawatu wajinga sana
 
UmkhontoweSizwe

JF-Expert Member
Dec 19, 2008
5,403
2,000
Naona makamanda mmesahau tu, ccm walipompuga kachero mbobea sisi makamanda tuliwakoromea sana, tukimpamba, kumpigia upatu, na kumpaka mafuta kwa mgongo wa chupa, in every way we could. Tukamvimbisha kichwa na kumwaminisha kuwa atashinda urais kwa kishindo!
Kwa hiyo hakuna cha ajabu kwa yanayoendelea sasa hivi
 
The imp

JF-Expert Member
Jul 6, 2012
13,523
2,000
CCM ilimfukuza BERNARD KAMILIUS MEMBE

1. Bila kufuata utaratibu/katiba ya ccm

2. Bila kufuata matakwa ya katiba ya nchi

Ila tu asigombee urais

1. Msajili wa vyama kimyaa

2. Mwanasheria mkuu wa serikali kimyaa

3. Vyombo vya dola kimyaaa

Cha ajabu ikiwa Chadema baasi kila mwenye videvu atainua gongo lake ilimradi kuwajeruhi cdm..... japo cdm siku zote wanazingatia sheria kanuni na taratibu.

Tanzania tunawatu wajinga sana
Inawezekana chadema watapeleka inaogopwa sana
 
brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
14,906
2,000
Naona makamanda mmesahau tu, ccm walipompuga kachero mbobea sisi makamanda tuliwakoromea sana, tukimpamba, kumpigia upatu, na kumpaka mafuta kwa mgongo wa chupa, in every way we could. Tukamvimbisha kichwa na kumwaminisha kuwa atashinda urais kwa kishindo!
Kwa hiyo hakuna cha ajabu kwa yanayoendelea sasa hivi

Labda kama una maana tofauti ya kukoroma.

CHADEMA imetakiwa kutowafukuza wasaliti, ikionywa kuwa watawalinda kwa nguvu zote. Alichosema supika, mwana sheria mkuu nk kila mwenye masikio kasikia.

Jombi, jiridhishe una maana sahihi ya neno kukoroma na uhalali wake.
 
MIGNON

JF-Expert Member
Nov 23, 2009
3,881
2,000
Lipumba alifukuza wabunge 8 wa viti maalumu,Ndugai alikuwa India akipata matibabu!Lakini haraka haraka siku hiyo hiyo aliandika barua kwa NEC kuwaeleza kuwa nafasi 8 ziko wazi na ndio ukawa mwisho wa wale viti maalumu!Walipinga mahakamani bila mafanikio!
Ndugai mbona hakuwatetea hao viti maalumu 8?Au kwakuwa walikuwa na maslahi na Lipumba ndio maana akawatosa hao viti maalumu?
Akina Halima Mdee wamekosa sifa za kuwa wabunge baada ya kufutwa uanachama!
Katika yote kumbuka "Mungu na Technolojia".Ruge aituachia usia huu.Hivi Ndugai akikumbusha haya atasemaje?
 
dmketo

JF-Expert Member
Aug 10, 2015
552
1,000
Tunaharibu sana nchi kwa kuendekeza hii tabia ya watu kusaliti vyama vyao kuonekana mashujaa. Kama mtu anaweza kusaliti chama chake na kufanya jambo kwa minajiri ya kujipatia manufaa binafsi mtu huyu atashindwa kuisaliti nchi yake kwa maslahi yake binafsi?

Tunapandikiza utamaduni wa hovyo sana ambao hutakuja kutugharimu huko mbele
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom