Vyakula vya siku hizi havina harufu kabisa

samsun

JF-Expert Member
Feb 9, 2014
7,386
5,954
Wakuu najua mko poa,
Yaani vyakula vya siku hizi havina harufu kabisa. Miaka ya nyuma kipikwe kitu cha wali hadi mtaa wa 7 utakisikia tu, lakini sasa hivi hata kipikwe hapo hutosikia harufu yake na hata mdomoni hauna ladha kivile.

Wajameni kulikoni harufu na ladha ya vyakula haipo siku hizi ????
 
Mia kabisa mleta uzi.
Kwa sasa vyakula vingi havina harufu wala ladha mdomoni.
Mimi kipindi nakua nilikuwa mpenzi sana wa viazi mbatata vya kuchemsha na nilichokuwa napenda ni ile ladha yake pamoja na unga unga fulani hivi(sio amaizingi!)...Kwa sasa nimeacha huo mlo,viazi havina ladha na havina ule unga unga baada ya kuchemshwa.Kwa sasa ukichemsha kiazi kinakuwa kama kimelowekwa,kikwetu tunaita "vichelema".
 
Mikate ya siku hizi hayaoti ukungu(mold) pamoja na kuhifadhiwa muda mrefu. Je nini madhara ya preservatives zinazotimika kwa afya zetu?
 
Mia kabisa mleta uzi.
Kwa sasa vyakula vingi havina harufu wala ladha mdomoni.
Mimi kipindi nakua nilikuwa mpenzi sana wa viazi mbatata vya kuchemsha na nilichokuwa napenda ni ile ladha yake pamoja na unga unga fulani hivi(sio amaizingi!)...Kwa sasa nimeacha huo mlo,viazi havina ladha na havina ule unga unga baada ya kuchemshwa.Kwa sasa ukichemsha kiazi kinakuwa kama kimelowekwa,kikwetu tunaita "vichelema".
Ni kweli mkuu.
 
Ni kweli, niliagiza kuku wa kienyeji kikaletewa kuku mkuuuubwa kakomaa hana ladha kabsaa, nikashtuka huyu si kuku wa kienyeji. Nikaambiwa ndio kuna kuku feki kienyeji siku hizi.
 
. Vinawekwa wekwa madawa mno
. Vinahifadhiwa kwenye friji, mabarafu ladha inaisha tofauti na zile njia za asili asili nyama inabanikwa au inakaushwa kwa chumvi

Afu pia kupikia kwenye gas napo kunapunguza utamu wa chakula, kitu cha kuni bana yani wali uliopikwa kwa kuni hata uwe mbaya lazma una ladha nzuri, sahivi Mara vi gas, mara vi rice cooker,sijui pressure cooker
 
Back
Top Bottom