Kwakweli ukiwa unafukia vyakula wewe unajiona sawa ila ni hatari sana ndugu zangu.
Tunaendekeza kula hovyo, dr janabi yuko sahihi.
Mleta mada asante kutukumbusha nisisitize tena tunywe maji ya kutosha, na tuache kula vyakula vigumu usiku.
Nimebadirika sana kiasi kwamba nikitembea kwa watu najikuta vyakula walivyo vipika siwezi kuvila.
Kwanza situmii , sukari, soda, juice za kununua, sili vyakula vyote vya kuunga nachemsha tu.
Mafuta kidogo nakutana nayo kwenye wali, nchicha na mayai pale ninapo yakaanga.( mchana tu)
Ratiba yangu inaanza saa 11:30 za asubuhi nakunywa ile chupa mkubwa ya maji yote. Yaani usiku wakati naenda kulala naenda nayo chumbani. (Sichemshi maji nanunua katon)
Hiyo chupa yote naipiga ingawa dr wangu wa ngozi aliniambia niwe nakunywa lita moja muda huo kabla ya mswaki..
Maji hayo hayatakiwi kuwa ya baridi yawe tu yakawaida usiyaweke kwenye friji. Nikimaliza kuyanywa huwa najisikia vibaya kwahiyo naendelea kulala kama lisaa nakaa sawa.
12:30 naamka nafanya shughuri
zangu kujianda kwenda kazini muda huo naanda breakfast ambayo sio chai nachemsha mhogo au gimbi nitakula na kipande kimoja cha labda kuku mchemsho au nakausha kweny Airflier nakula bila chai.
Saa 4: 00 nusu lita ya maji.
Chakula cha mchana tuseme saa 8 au 9 mchana hapa ndo changamojo aisee mazingira yetu ya kazi huwezi kukwepa wali, so nitakula wali kidogo na mlenda au na mboga za majani tu. Baada ya kula dk 40 zikipita nakunywa tena nusu lita ya maji.
Kuanzia saa 11 jion hadi saa 2 usiku huo muda nakuwa bado ofisin nakuwa nakunywa maji kidogo kidogo hadi saa 2 kamili usiku naenda home.
Nikifika home nafanya mazoezi kidogo kama nusu saa naoga nakula matunda tu, yaani tango mbili au papai moja au tikiti au nikisikia tumbo linalalamika kutoshiba nakula ka kipande ka kuku au ka samaki nalala. Mpaka kesho saa 11 na nusu.
Ratiba hii ni nzuri sana ukinywa maji asubuhi mapema lazima kila asubuhi uende choo.
Magonjwa kama UTI sikumbuki mwisho nimepata lini.
Ngozi yangu imekaa vizuri mno nina ule weusi chocolate flani niliyo kuwa naitamani (ni pamoja na kutumia lotion original za SH AMON'S.
Wakuu maji ni uhai.
Nb. Ukijisikia kuumwa usikimbilie kumeza dawa kwanza kunywa hata chupa moja ya maji kubwa baada ya nusu saa utaanza kukojoa. Baada ya kisaa ukiendelea kujisikia vibaya nenda kapime
Mwili ukikosa maji lazima ukupe taarifa utajisikia vibaya au utaumwa kichwa.
Nb mbinguni hakuna hotel hakikisha unakula vizuri. Usijinyime eti unawekeza kula kwa mpangilio.