Vyakula gani huwezi kula hata iweje?

karv

JF-Expert Member
Dec 26, 2019
1,799
3,221
Nawasalimu kwa jina la jamuhuri mtaitikia wenyewe huko

Kila mtu kuna baadhi ya vyakula hawezi kuvila kwa sababu kama za magonjwa au kutokuvipenda.

Mimi binafsi siwezi kula vyakula vifuatavyo yani heri nishinde njaa. Sili sababu sivipendi tu.

~Viazi vitamu vya kuchemsha sili vya
Kukaanga nakula.

~Maharage yakiungwa na mafuta sili iwe kwa ugali hata kwa wali ila yakiwekwa nazi au mrenda wa majani nakula.

~Wali au ugali ukipoa sili

~kabichi hapana, kachumbali hapana

~Nyama ya ng'ombe, mbuzi, kondoo, nguruwe, sungura, Bata na nyama za pori zote sili

~Chai iwekwe mchai chai na tangawizi tofauti na hapo sinywi.

~Maandazi, mikate, skonsi Sili

Sili kwa sababu sivipendi sio sababu vinaniletea matatizo hapana

Hebu na wewe tuambie ni vyakula gani huwezi kula hata vipikweje
DSC02523.jpg
 
Ebu ngoja niendelee kusoma comments, maana namuona kijana wangu anascrow up kuendelea kusoma huu uzi...🙂
Ok naona ameanza kutype..😊
 
Kuweni serious hamli nyama!, mwengine boga na kabeji wakati kabeji ni kitunguu kikubwa!

Niwaeleze ukweli kitu Kama hukili kwasababu isiyo ya kiafya jua tu hujakutana na fundi wa kupika hicho kitu!. Hivi kabeji ipikwe na karanga ya kutosha kitu roast moja amaizing unaachaje??
Kitu cha magimbi kipikwe rojo kichanyanywe na nazi iliyoshiba unaanzaje kusema huli!!?? 😀

Chakula ni ufundi ndugu zanguni,mkikutana na makungwi mbona mtakula.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom