Vurugu zatokea Mahakamani Arusha kwenye kesi ya viongozi na wanachama wa CHADEMA

Tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
43,683
2,000
Mambo ya Halima James Mdee yamevuruga sana!

Halafu kuna wapuuzi walikuwa wanasema cdm waende mahakamani wakafungue mashtaka kama wameibiwa kura, kisha mahakama ndio hizo zinaagizwa na wahuni wachache wa serekali jinsi ya kuendesha kesi.
 
REALNEGRONEVABROKE

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
3,465
2,000
Una uhakika aliyoandika huyo mleta mada. Mimi siamini Mahakama haiwezi toa hukumi mbili kwa wakati mmoja.
Siyo uhakika tu bali kuna jamaa zangu wanasimamia hizo kesi kwa upande wa utetezi.
Ni kipofu tu wa 'akili' hatoona kinachoendelea katika mahakama zetu specific kesi za kisiasa.
 
Ghosryder

JF-Expert Member
Jul 6, 2014
10,195
2,000
Katika hali ya kushangaza Dunia, mahakama ya hakimu mkazi Arusha,imesema haina mamlaka ya kutoa dhamana kwa Washtakiwa 20 ambao ni wanachama na viongozi wa CHADEMA wanaokabiliwa na Kesi no 72,75 na 76 zote za UHUJUMU UCHUMI zinazokabili wanachama 20 wa Arusha Mjini na Arumeru Magharibi

Hakimu Mfawidhi Bibi Mahumbugwa alikuwa anawasiliana na wakili wa serikali kabla ya kusoma hukumu hii ambayo imefanya ndugu wa washtakiwa kubaki midomo wazi, kabla ya hukumu ya leo Hakimu huyu huyu na mahakama hii ilitoa uamuzi Novemba 9 kuwa ina mamlaka ya kutoa dhamana kwa kuwa shtaka lenyewe halina zaidi ya 10mil.Ni mara ya kwanza kwa hakimu wa mahakama kutoa hukumu mbili tofauti kwenye shauri moja

Kisheria baada ya hukumu ya kwanza upande wa Jamhuri ulipaswa kukata rufaa kupinga uamuzi wa mahakama lakini badala yake hakimu amewekewa shinikizo na Serikali kufuta hukumu ya awali

Baada ya ndugu kusikia hivo walizingira mahakama wakitaka haki itendeke kwa ndugu zao ambao ndio watafuta mkate wa kila siku wa familia,baadhi ya washtakiwa wana watoto wachanga!

Mawakili wa upande wa Wafuasi wameeleza kuwa wataenda mahakama kuu kuomba dhamana kwa ajili ya wateja wao! Jopo hili linaongozwa na Wakili maarufu Jijini Arusha Sheck Mfinanga,pamoja na wakili Jebra Kambole na Winnie

Ndugu wa washtakiwa walionekana mahakamani hapa wakiwa na jaziba kali kiasi cha kutishia usalama wa mahakama,na wamesema siku ya shauri watakuja kwa wingi kuonyesha mshikamano,aidha wametaka Mahakama itende haki kwa kuwa ndugu zao wamebambikiziwa kesi za kisiasa

My take
Mahakama inapaswa kutoa haki mapema maana haki iliyocheleweshwa ni haki iliyonyimwa.
Huyu hakimu aache ubabaishaji atende haki maana kuna siku uvumilivu utawashinda watu
Umeandika kishabiki sana hata hueleweki!! wafuasi wa Lissu akili zenu mnazijua wenyewe
 
Jozi 1

JF-Expert Member
Aug 16, 2015
6,559
2,000
Ni kweli Mahalama ya Hakimu Mkazi haina mamlaka ya kutoa dhamana kwenyr uhujumu uchumi
Katika hali ya kushangaza Dunia, mahakama ya hakimu mkazi Arusha,imesema haina mamlaka ya kutoa dhamana kwa Washtakiwa 20 ambao ni wanachama na viongozi wa CHADEMA wanaokabiliwa na Kesi no 72,75 na 76 zote za UHUJUMU UCHUMI zinazokabili wanachama 20 wa Arusha Mjini na Arumeru Magharibi

Hakimu Mfawidhi Bibi Mahumbugwa alikuwa anawasiliana na wakili wa serikali kabla ya kusoma hukumu hii ambayo imefanya ndugu wa washtakiwa kubaki midomo wazi, kabla ya hukumu ya leo Hakimu huyu huyu na mahakama hii ilitoa uamuzi Novemba 9 kuwa ina mamlaka ya kutoa dhamana kwa kuwa shtaka lenyewe halina zaidi ya 10mil.Ni mara ya kwanza kwa hakimu wa mahakama kutoa hukumu mbili tofauti kwenye shauri moja

Kisheria baada ya hukumu ya kwanza upande wa Jamhuri ulipaswa kukata rufaa kupinga uamuzi wa mahakama lakini badala yake hakimu amewekewa shinikizo na Serikali kufuta hukumu ya awali

Baada ya ndugu kusikia hivo walizingira mahakama wakitaka haki itendeke kwa ndugu zao ambao ndio watafuta mkate wa kila siku wa familia,baadhi ya washtakiwa wana watoto wachanga!

Mawakili wa upande wa Wafuasi wameeleza kuwa wataenda mahakama kuu kuomba dhamana kwa ajili ya wateja wao! Jopo hili linaongozwa na Wakili maarufu Jijini Arusha Sheck Mfinanga,pamoja na wakili Jebra Kambole na Winnie

Ndugu wa washtakiwa walionekana mahakamani hapa wakiwa na jaziba kali kiasi cha kutishia usalama wa mahakama,na wamesema siku ya shauri watakuja kwa wingi kuonyesha mshikamano,aidha wametaka Mahakama itende haki kwa kuwa ndugu zao wamebambikiziwa kesi za kisiasa

My take
Mahakama inapaswa kutoa haki mapema maana haki iliyocheleweshwa ni haki iliyonyimwa.
Huyu hakimu aache ubabaishaji atende haki maana kuna siku uvumilivu utawashinda watu
 
1954

JF-Expert Member
Nov 14, 2006
9,639
2,000
Kwani Rais haoni kuwa watu wake maskini wanateseka kwa yeye kuwepo madarakani madaraka amepata sasa kwanini asiwaachie watu wasio na makosa hao?
Kwani hiyo mahakama imesharamka kuwa watu haa hawana makosa?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom