Vurugu zatokea Mahakamani Arusha kwenye kesi ya viongozi na wanachama wa CHADEMA

Mwan mpambanaji

JF-Expert Member
Apr 3, 2008
482
131
Katika hali ya kushangaza Dunia, mahakama ya hakimu mkazi Arusha,imesema haina mamlaka ya kutoa dhamana kwa Washtakiwa 20 ambao ni wanachama na viongozi wa CHADEMA wanaokabiliwa na Kesi no 72,75 na 76 zote za Uhujumu Uchumi zinazokabili wanachama 20 wa Arusha Mjini na Arumeru Magharibi

Hakimu Mfawidhi Bi.Mahumbugwa alikuwa anawasiliana na wakili wa serikali kabla ya kusoma hukumu hii ambayo imefanya ndugu wa washtakiwa kubaki midomo wazi, kabla ya hukumu ya leo Hakimu huyu huyu na mahakama hii ilitoa uamuzi Novemba 9 kuwa ina mamlaka ya kutoa dhamana kwa kuwa shtaka lenyewe halina zaidi ya 10mil.Ni mara ya kwanza kwa hakimu wa mahakama kutoa hukumu mbili tofauti kwenye shauri moja

Kisheria baada ya hukumu ya kwanza upande wa Jamhuri ulipaswa kukata rufaa kupinga uamuzi wa mahakama lakini badala yake hakimu amewekewa shinikizo na Serikali kufuta hukumu ya awali

Baada ya ndugu kusikia hivo walizingira mahakama wakitaka haki itendeke kwa ndugu zao ambao ndio watafuta mkate wa kila siku wa familia,baadhi ya washtakiwa wana watoto wachanga!

Mawakili wa upande wa Wafuasi wameeleza kuwa wataenda mahakama kuu kuomba dhamana kwa ajili ya wateja wao! Jopo hili linaongozwa na Wakili maarufu Jijini Arusha Sheck Mfinanga,pamoja na wakili Jebra Kambole na Winnie

Ndugu wa washtakiwa walionekana mahakamani hapa wakiwa na jaziba kali kiasi cha kutishia usalama wa mahakama,na wamesema siku ya shauri watakuja kwa wingi kuonyesha mshikamano,aidha wametaka Mahakama itende haki kwa kuwa ndugu zao wamebambikiziwa kesi za kisiasa

My take,
Mahakama inapaswa kutoa haki mapema maana haki iliyocheleweshwa ni haki iliyonyimwa.
Huyu hakimu aache ubabaishaji atende haki maana kuna siku uvumilivu utawashinda watu
 
Shughuli ya mitano tena inaendelea!
0659010.jpg
 
Mbona kichwa cha habari na habari yenyewe haviendani? Nilitegemea kusoma aina ya vurugu zilizotokea hapo mahakamani. Bahati mbaya nimesoma utopolo tuuu!!
 
Mbona kichwa cha habari na habari yenyewe haviendani? Nilitegemea kusoma aina ya vurugu zilizotokea hapo mahakamani. Bahati mbaya nimesoma utopolo tuuu!!
'Kisheria baada ya hukumu ya kwanza upande wa Jamhuri ulipaswa kukata rufaa kupinga uamuzi wa mahakama lakini badala yake hakimu amewekewa shinikizo na Serikali kufuta hukumu ya awali.'

Hivi hapo huoni kama hao watafsiri sheria waneleta/ wanaleta vurugu zisizo na msingi kwa matakwa ya malaika wako.

Hivyo vichwa vyenu vimebeba nini ndani?
 
'Kisheria baada ya hukumu ya kwanza upande wa Jamhuri ulipaswa kukata rufaa kupinga uamuzi wa mahakama lakini badala yake hakimu amewekewa shinikizo na Serikali kufuta hukumu ya awali.'

Hivi hapo huoni kama hao watafsiri sheria waneleta/ wanaleta vurugu zisizo na msingi kwa matakwa ya malaika wako.

Hivyo vichwa vyenu vimebeba nini ndani.?
Una uhakika aliyoandika huyo mleta mada. Mimi siamini Mahakama haiwezi toa hukumi mbili kwa wakati mmoja.
 
Back
Top Bottom