Vurugu za Zanzibar na Dar - Predicted Govt failure | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vurugu za Zanzibar na Dar - Predicted Govt failure

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by FairPlayer, Oct 18, 2012.

 1. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #1
  Oct 18, 2012
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Wakuu,

  Siku nyingi sijawahi kuanzisha topic humu.

  Nimekua nikifuatilia kwa makini vurugu za hivi karibuni, nikajaribu kuzifikiria kwa mapana na marefu.

  Ninachoweza kusema ni kuwa Serikali yetu imefeli kwenye USALAMA na AJIRA. Nitaelezea kidogo hapo chini.

  Kuna kiongozi aliwahi kusema ukosefu wa ajira kwa vijana ni a TIME BOMB. Watu tukabeza...

  Naelezea, Timing ya Mtoto alietenda kosa Mbagala na vurugu ni vitu viwili vya kufikiriwa.

  Vijana hawana ajira, anasikia kuna kufanya vurugu sehemu akiangalia hana BUKU mfukoni anafanyaje?, anaenda kubahatisha huko kwenye vurugu angalau anaweza kupata hata Buku (shs elfu moja).

  Kumbe basi vurugu, maandamano mengi ni "AJIRA" kwa hawa vijana! mie nafikiria hivyo. Haiingii akilini mtu yupo BIZE na shughuli zake halafu umuondoe eti akaandamane tena akavunje amani?, labda uwe na akili ndogo kama yangu ndo utasema uende.

  UAMSHO Zanzibar. Hainiingii akilini kwakweli kua serikali imeshindwa kudhibiti hili GENGE. Ukiangalia kwa makini utagundia kuwa hiki kikundi hakikuanza leo. Kilikuwepo kabla. Ni nini basi kinachochea haya mambo?. Kwa hakika ni PESA. Uhamsho wanapata RUZUKU. Hili msiniambie UWT (TISS) hawajui, hawa jamaa wanafadhiliwa kufanya haya wanayofanya. Nani anawafadhili? mbona simpo, hata gari analotumia kiongozi wao kasema kasaidiwa atumie..... Of coz tunahitaji CIA kuja kugundua wafadhili wao.

  Vurugu zote zinazotumia UDINI ni Hatari kama vurugu zote zitumiazo UKABILA. Lazima tuzipinge kwa nguvu zote.

  Siamini kua mifano tulionayo tumeisahau... siamini kua kuna TISS au intelijensia ya Polisi haioni haya.

  Ila Serikali ikiweka mambo sawa na maisha bora kwa kila mtanzania ambayo tuliwahidi hawa watu mwaka 2005 basi hizi vurugu zitatokomea. Na wafadhili wa hizi vurugu wakitembelewa na TRA mara kwa mara watatulia. Hela wanaiba serikalini (kutolipa kodi) kisha wanazipeleka kuishambulia same govt.

  AU KUNA WANAOFAIDIKA NA HIZI VURUGU SERIKALINI??

  Mrisho Mpoto: Chocheeni kuni mbichi moto ukolee.....

  Ni hayo tu

  Fairplayer
   
 2. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #2
  Oct 18, 2012
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145

  Siamini kuwa hatuoni kabisa kuwa taarifa kama hii INATUHARIBIA UTALII. Maana wageni wengi wanafuatilia vitu kama hivi.
  Siamini kuwa serikali haioni hili. Siamini, Siamini, Siamini.

  Swali la msingi ni JE KWA FAIDA YA NANI SERIKALI INAFANYA HAYA?
   
 3. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #3
  Oct 18, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  kamanda umenene vema sasa, tatizo ni ukosefu wa ajira, na Goverment failure, issue ya Mbagala kwangu mie ni huyo mwalimu wa madrasa kwa kuganga njaa tu kaanzisha kama ajira... kakaa anapotosha watoto wetu badala ya kufundisha misingi ya dini...

  Mkuu, ukosefu wa ajira ni zaidi ya Bomu, kwa kuwa serikali ni dhaifu inapuuzia puuzia tu...
   
 4. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #4
  Oct 18, 2012
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Kaka ukiacha la ajira kuna hata VIONGOZI serikalini wanaopenda haya yaendelee. Hasa ya UHAMSHO. Kwani Muungano ukivunjika si vyeo vinaongezeka? au sio? Pesa

  Serikali inabidi ifidie haya makanisa si ndio? Pesa

  Utalii ukipungua si itabidi tutangaze na tuwe na semina kadhaa na makongamano nje ya nchi au sio? Pesa

  It is all about Money!
   
 5. I

  IKISU Member

  #5
  Oct 18, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 64
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 15
  Kwakweli mi siko mbali na mtoa mada apa ishu ni ajira,na elimu pia ndugu zetu awana, lakini ata kama tungekua na viwanda vya kutosha watu wasinge kosa ajira kabisa ata kama mtu ajasoma pia kazi zingekuepo za kuwa fiti, mtu kwanzia asubui anakaa kijiweni unategemea nini ata wakimwambia unaandamana bila pesa ana kubali kwasababu anapata kitu cha kumuweka bize aijalishi ni atari. BOMU LIMEANZA KUFUKUTA ASANTE NDUGU LOSAWA KWA KUTABILI.
   
 6. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #6
  Oct 18, 2012
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Naam. Nabii hakubaliki kwao.

  Hili tuliliona na tumelisema.
   
 7. Takalani Sesame

  Takalani Sesame JF-Expert Member

  #7
  Oct 18, 2012
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 588
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Serikali dhaifu inachukulia poa hizi vurugu kwa sasa lakini impact yake ni kubwa sana. Haiwezekani kila siku ni watu wale wale na kwa sababu almost zile zile na hatua stahiki za kumaliza tatizo hazichukuliwi. Kifupi serikali ipo ipo tu kwenye hili. Inafunika kombe tu. CCM na serikali yake kwa sasa ni janga la kitaifa.
   
 8. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #8
  Oct 18, 2012
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Wanachochea kuni mbichi zilizotiwa maji Moto ukolee ugali uivee..

  Yaani huyu Mrisho Mpoto ana akili sana kaimba wakati muafaka kabisa.
   
 9. n

  nyantella JF-Expert Member

  #9
  Oct 18, 2012
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 890
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45

  Tatizo ni hilo tuu? hivi serikali ni nini? sisi wananchi hatuna role yoyote? mimi naona watanzania tunapenda kuiga mno! Mwalimu aliwahi kutoa mfano wa mtu mwenye almasi anavyoweza kudanganywa na tapeli mwenye kipande cha chupa wakabadilishana kiulaini!! sisi watanzania tulikuwa na almasi yetu iitwayo "Amani", wamekuja wapuuzi wametwambia ni feki, tumekubali sasa imetoweka, tuanaaanza kutafuta sababu oh, ajira, ooooh serikali dhaifu, oooooh blah, blahhhh, tutazitoa sana but, the beautiful peaceful TZ we had is no longer!! issue ya Zanzibar tayari ipo Aljazeera, ngoja tuone hiyo kesho Dar!

  kwamba tatizo ni kazi si sababu pekee maana hakuna nchi duniani iliyofanikiwa kutoa kazi kwa kila mtu ata USA si wote waliosoma wana kazi! I am out!
   
 10. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #10
  Oct 18, 2012
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Nasikia kanisa lingine limechomwa YOMBO leo!!

  Kweli hatuna Polisi au hata usalama wa Taifa?

  Kwani amani ikitoweka si ni failure ya usalama wa taifa?

  Am sure kuna anaye faidika na hizi vurugu. Naombeni mnikosoe .
   
 11. M

  Makyomwango JF-Expert Member

  #11
  Oct 18, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 323
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ndugu yangu fairplayer UWT (TISS) wako kwa ajili ya CHADEMA, uLIMBOKA. pIA Intelligency ya polisi iko kwa ajili ya CHADEMA. Angalia walivyotaabika kumkamata mtu hatali katika jamii ya watanzani, angalia ambavyo wanaifumbia macho radio hatari kwa mustakabali wa watanzania, zaidi sana anagalia ambavyo kikundi kidogo na chenye wafuasi wachache cha uamsho kinavyopeleka vidole machoni kwa mwema, othman na wengine! kuna TISS hapo? kuna intelligence ya police hapo!
   
 12. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #12
  Oct 19, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Mkuu unaishi nchi gani? namashaka sana na wewe, Ukosefu wa AJIRA Tanzania unacompare na USA ana nchi zingine? pole sana,

  mfano ujeruman...kuna Job Creation Department, ipo chini ya serikali kazi yao ni kutengeneza ajira kwa watu wake, Je serikali hii dhaifu imatengeneza ajira?

  Bado hujajuaudhaifu ndio umetuleta hapa? pole sana ndugu?

  Kwa serikali makini kama ya mwalimu na nchi zingine zote kitu cha kwanza ni kuhakikisha usalama wa nchi...imagine kinaibuka kikundi na kiaanza kuukosoa katiba waziwazi/ muungano... wakati watawala wetu wameapa kuilinda na kuutetea katiba, serikali inawacha wanapata umaarufu, wamapata wafuasi ndio inaanza kuchukua hatua...

  soma signature yangu utajua kwa nini tumefika hapa tulipo...
  Tafakari.
   
 13. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #13
  Oct 19, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Waingereza wana msemo, " AN IDLE MIND IS THE HOME OF THE DEVIL" Hawa vijana wengi wasio kuwa na ajira wanaona afadhali wafanye fujo pengine wakienda mahabusu wanaweza angalau kupata mlo mmoja kuliko huku waliko ambapo hawana hakika hata ya dona na maharage.

  Ndio maana huko mijini ambako vijana wengi hawana shuhuli mmaluma za kufanya ukilinganisha na vijijini , ajali ikitokea badala ya kusaidia wao kwanza ndio wanawaibia wahanga wa ajali; hii yote inaonesha desperation ya maisha ya vijana wetu. Hivyo basi akitokea mtu anaeweza kuwafadhili hawa vijana kukidhi njaa yao ni rahisi hawa vijana kutumika hata kwa mambo ya kigaidi.
   
 14. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #14
  Oct 19, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Waingereza wana msemo, " AN IDLE MIND IS THE HOME OF THE DEVIL" Hawa vijana wengi wasio kuwa na ajira wanaona afadhali wafanye fujo pengine wakienda mahabusu wanaweza angalau kupata mlo mmoja kuliko huku waliko ambapo hawana hakika hata ya dona na maharage!! Ndio maana huko mijini ambako vijana wengi hawana shuhuli maalum za kufanya ukilinganisha na vijijini , ajali ikitokea badala ya kusaidia wao kwanza ndio wanawaibia wahanga wa ajali; hii yote inaonesha desperation ya maisha ya vijana wetu. Hivyo basi akitokea mtu anaeweza kuwafadhili hawa vijana kukidhi njaa yao ni rahisi hawa vijana kutumika hata kwa mambo ya kigaidi!!
   
 15. PJ

  PJ JF-Expert Member

  #15
  Oct 19, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 297
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kuna mpango wa waislam wenye siasa kali kufanya vurugu baada ya sala ya alasasiri kwa mujibu wa inteligency information kushinikiza kuachiwa kwa akina ponda na wezake.

  Kama walifanikiwa wakati walipoandama na kuachiwa bila masharti kwa wale waliozuia sensa ni nini kitakachowazuia wasitimize azma yao leo?
   
 16. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #16
  Oct 19, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  DOnt pray foR this thing to happen broda, tena kemea katika Jina la Yesu...my name-mate PJ!
   
 17. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #17
  Oct 19, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,798
  Likes Received: 3,883
  Trophy Points: 280
  Wakristu kwa umoja wetu tumiminike makanisa tukazihami nyumba za mungu! ni fedheha , aibu na najisi kwetu kuruhusu nyumba za mungu na madhabahu zake zilizowekwa wakfu na mungu anakaa humo kuchomwa moto huku tukiwa tunaangalia! Tusichokoze mtu wala kuingilia maandamano lakini atakayesogelea nyumba za ibada na mali za makanisa kwa lengo la kuchoma na kupora tupambane nae bila kujali ni mkristu, muislam, myahudi, au mpagani!
   
 18. PJ

  PJ JF-Expert Member

  #18
  Oct 19, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 297
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hatuombei hayo.

  Tunawataka wanausalama kuchukua hatua stahiki
   
 19. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #19
  Oct 19, 2012
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Vurugu zimetokea.

  Tulipost hii kitu jana. Siamini mimi mwananchi ninayekaa Mabwepande naweza kujua kuliko TISS wenye zana na bajeti ya hela ya kutosha.

  Polisi wameshindwa wameingia wanajeshi.

  A TIME BOMB,........yupo wapi ambaye bado anapinga?
   
 20. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #20
  Oct 19, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  The higher the jobless rate the higher the crime & chaos rate
   
Loading...