Nchi hii hata watu wote wawe na Degree moja, haiwezi kuendelea

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,339
51,883
Kwema Wakubwa!

Kwa tathmini zangu ninazoziamini kuliko kitu chochote kile. Nachelea kusema, nchi hii hata watu wote yaani wote milioni 60 tuwe na Degree moja moja na zaidi kamwe haiwezi kuendelea.

Kwa bahati nzuri Mimi ninayo hiyo degree hivyo ninachokiongea nakielewa vizuri Sana. Kama ningekuwa madarasa yangu ni madogo basi huenda ningeongea Jambo nisilo na Uelewa nalo.

Pengine naweza sema tena, nchi hii hata wote tungekuwa na PhD bado nchi hii isingeendelea.

Unajua Kwa sababu gani?

Sitaki kulijibu hili.
Lakini angalia wenye hizo degree mpaka maprofesa utaelewa nazungumzia Jambo gani.

Elimu tuipatayo ni Ile iliyopitwa na wakati,
Uliona wapi kitu kilichopitwa na wakati kikaendeleza nchi.

Elimu inayoua udadisi sio elimu,
Elimu inayofundisha ubinafsi sio elimu,
Elimu Inayomfanya mtu akariri badala ya kuelewa sio elimu,nilipokuwa nasoma degree nilikaririshwa mavitu ya watu wazamani mno ambayo Kwa akili ndogo tuu ningeweza kuayaeleza.

Embu assume ati uambiwe utoe maana ya istilahi "Lugha" au ueleze maana ya "mawingu" au ueleze Maana ya neno "udongo"
Mambo hayo ati mpaka umnukuu sijui Nani huko ambaye naye alitoa maana ya maneno hayo Kwa mtazamo wake.

Elimu za kidunia zinachekesha Sana. Yaani ukishindwa kuikariri maana hizo umefeli wakati huenda ukitoa maana yako ya kichwani ni Sawa kabisa na Ile Ile walioitoa HAO wahenga.

Elimu ya kunukuu watu waliopewa jina la utaalamu 🤣🤣🤣, elimu hii ndio inawafanya Vijana wasijiamini mpaka wapate mawazo ya watu wengine.

Unakuta liprofesa limepewa wizara serikalini, linatakiwa litoe maamuzi kuhusu Jambo Fulani ambalo kimsingi ni lawakawaida Sana. Yaani hata mtu ambaye shule hajaenda anaweza akalitathmini na kulitolea maamuzi. Lakini Kwa vile haiamini akili yake, utashangaa mpaka lifungue watu waitwao Wataalamu WA zamani huko, au aangalie nchi za Wazungu wamefanyaje.

Lini mtaweza kuzitumia akili zenu wenyewe enyi wasomi?"

Wasomi hawajiamini Kwa sababu wamefundishwa kutojiamini,

Kwa elimu hii tupewayo ukiwa na wasomi wengi basi jua fika kabisa taifa Lina idadi kubwa ya watu wasiojiamini, kwani shuleni ndivyo walivyofunzwa hivyo.

Kwa sasa hivi ni rahisi kumnyima haki msomi tena wa degree kuliko kumnyima mtu asiyesoma, mtu asiyesoma anatumia common sense yaani akili ya kuzaliwa tuu kujitetea na mazingira yake. Lakini wasomi wengi hawana hata hiyo common sense.

Msomi anasema Hana mtaji wa kuanzisha biashara lakini asiyesoma halalamiki hivyo,
Usoni imekaa mdomoni kuliko akilini huenda ndivyo walivyofunzwa.

Hata humu JF ati ili mtu aonekane Yuko na akili/ uwezo wake wakufikiri upo njema, utashangaa ati mtu akijifaraguza na kingereza ATI huo ndio usomi,🤣🤣🤣. Nacheka Kama MAZURI.

Msomi badala aumize kichwa kujua atatatua vipi changamoto ya Ajira iliyomo katika jamii yake yeye anakalia kulia Lia ati hakuna ajira. Pumbavu.

Degree nyingi zime-expire miaka mingi iliyopita.
Hazina tofauti na ngano au visasili vya Fasihi.
Labda iwe Kwa burudani tuu Kama Sanaa.

Elimu ambayo inamfundisha mtu Kumheshimu boss wake hata katika mambo ya Uhalifu uliona wapi elimu ya hivyo ikaendeleza nchi?

Elimu ambayo wasomi wanawategemea Wanasiasa 🤣🤣🤣 uliona wapi ikaendeleza nchi ndugu yangu?

Siku moja nikafanya utafiti huko kwenye vilinge Kwa waganga na waganguzi WA kienyeji, nikapata connection nyingi tuu nikikusudia kuchunguza mambo kadhaa.

Nikashangaa mpaka wenye degree wakienda Kwa waganga WA kienyeji🤣🤣🤣

Hivi degree hizi za kuamini waganga WA kienyeji ndio ziendeleze nchi hii, labda Kwenye ndoto.
Mtu na degree zake uketishwe Kwa waganga ati kujipatia Utajiri, sijui kupata kazi🤣🤣🤣 sijui kumfanya boss akuogope yaani vituko vitupu. Degree hiyo ndio iendeleze nchi hii. Thubutu!

Degree zilizofundishwa miujiza na maendeleo ya dezo, yaani maendeleo yanakuja kirahisi rahisi.
Nchi iendeleze na degree za wanaokimbizana kwenye maji ya upako Kwa hawa wajiitao manabii 🤣🤣🤣🤣.
Uende wakupe visakale vya wahenga wakiyahudi alafu ujifanye nawe utakuwa hivyo hivyo🤣🤣🤣.

Jamani tuache kudanganyana, hii nchi haitaendelea Kwa elimu hizi na Mchunguzi hata ipite miaka Buku.

Siku moja nilicheka kweli nimeona mtu aliyetengeneza Ndege ya kiwango cha chini Kabisa, walau yeye alitengeneza, nilipofuatilia elimu yake kumbe hata hajafika Kidato cha nne. Sasa wenye degree zao kuhojiwa wakaanza kunukuu sijui vifaa gani vya kitaalamu Kama walivyofundishwa huko vyuoni 😃😃😃.
Wewe na degree yako uprofesa wako umeshindwa kuunda hata baiskeli ya mabati ati unamkosoa mtu aliyeunda unda Ndege Kwa kuchanga vifaa mbalimbali sijui vya baiskeli, pikipiki au Gari.
Unamkosoa wakati wewe ukipewa walau Kama huyo wa aliyekimbia shule.

Nchi haitaendelezwa na wenye degree, wenye degree Hali zao nazijua, kwani Mimi ni mmoja wao.
Nje ya Ajira wengi wao ni Kama Masai bila some au rungu.

Aaargrrrrrrrhii!! Nilikuwa nataka kusema nini kwani?

Niishie hapa nasubiri povu la wenye degree.


Robert Heriel
TAIKON WA FASIHI
Kwa sasa Dar es salaam
 
Hata wote wawe maprofesa haitasaidia.

Elimu ambayo inakufundisha kuwa na elimu ni kuwa na akili kuliko watu wote ni ujinga kuliko
ujinga wowote ule kwa sababu inakupa confidence ya kufanya ujinga bila kuhoji wala kuwa na mashaka juu ya
ujinga ujinga huo kisa makaratasi yaliandika hivo au utashi wako ukisadiwa na kitu unachokiita elimu kimekutuma kufanya hivo.

Mara mia tujue kujua kusoma na kuandika tu kuliko kupata degree zitakazo tupa confidence ya kufanya ujinga wowote
kwa kisingizio tumeelimika.

Jinsi unavokuwa na elimu kubwa au cheo kikubwa ndio jinsi unavokuwa na confidence ya kufanya ujinga mkubwa
eti tukijifariji elimu/cheo kita justify huo ujinga kuwa ni welevu
 
Hata wote wawe maprofesa haitasaidia.
Elimu ambayo inakufundisha kuwa na elimu ni kuwa na akili kuliko watu wote ni ujinga kuliko
ujinga wowote ule kwa sababu unakupa confidence ya kufanya ujinga bila kuhoji wala kuwa na mashaka juu ya
ujinga ujinga huo kisa makaratasi yaliandika hivo au utashi wako ukisadiwa na kitu unachkiita elimu kimekutuma kufanya hivo.
Mara mia tujue kujua kusoma na kuandika tu kuliko kupata degree zitakazo tupa confidence ya kufanya ujinga wowote
kwa kisingizio tumeelimika.


Ati Kwa vile alisema Fulani hivi basi nasi tuseme hivyo pfuuu
 
Upumbavu mtupu unaiponda degree wakati walionayo hawafiki hata 10% ya jamii ya tz (mil. 60) alafu unawalaumu

Hao 90% wasio na degree wameleta maendeleo gani?
Unawapa sifa wasio na degree na ndo wengi tz tuoneshe mchango wao kwenye maendeleo.
 
Iliyotufikisha hapa ni serekali ya ccm , mambo ya kukaa kusubiria wanasiasa wakuamulie maisha yako sio kabisa , kwani siasa zenyewe ni uchwara mtupu
 
Iliyotufikisha hapa ni serekali ya ccm , mambo ya kukaa kusubiria wanasiasa wakuamulie maisha yako sio kabisa , kwani siasa zenyewe ni uchwara mtupu
Hawa wanasiasa wengi wana degree ama hapana

Kama jibu ni hapana kwa nini lawama zinaenda kwa wenye degree
 
Upumbavu mtupu unaiponda degree wakati walionayo hawafiki hata 10% ya jamii ya tz (mil. 60) alafu unawalaumu

Hao 90% wasio na degree wameleta maendeleo gani?
Unawapa sifa wasio na degree na ndo wengi tz tuoneshe mchango wao kwenye maendeleo.
Umemjibu vyema kabisa.
 
Niishie hapa nasubiri povu la wenye degree.
Umezunguka zunguka mno na hiki 'kimada' chako aisee, hadi unaboa! Nimesoma hiyo aya ya kwanza, nikashindwa kuendelea mbele; kwa sababu sioni mantiki ya hoja yako.
Ukitaka kueleza habari yako ya namna hii ielekeze kwenye uhusika wa CCM na kuharibu taratibu zote za kiutawala ambazo zingeweza kuleta maendeleo Tanzania.

Kama unaona elimu (ikiwa ni pamoja na hizo digrii unazozielezea hapa) kuwa hazisaidii wanaozipata kugeuza hali zao za kimaisha na kwa nchi kwa ujumla, itakulazimu urudi kule kule kwenye CCM na uhusika wake kwenye hilo.

Usiparamie tu kunijibu, naomba ukae chini utafakari vizuri haya niliyoandika hapa, na kama huridhiki, basi njoo tujadili kiungwana.

Mkuu'ROBERT HERIEL', umenielewa?
 
Upumbavu mtupu unaiponda degree wakati walionayo hawafiki hata 10% ya jamii ya tz (mil. 60) alafu unawalaumu

Hao 90% wasio na degree wameleta maendeleo gani?
Unawapa sifa wasio na degree na ndo wengi tz tuoneshe mchango wao kwenye maendeleo.
Hao 10% wameifanyia nini tz?
Hao 90% ndio wamewasomesha hao wenye degree wakitegemea watapata matokeo chanya.
Hao 10% ndio wapo kila kona kuanzia ngazi za maamzi mpaka kwenye mashirika ya umma ambayo kila siku ya tangaza hasara.
Tupe matokeo ya elimu yao imelisaidia nini taifa
 
Back
Top Bottom