Uchaguzi 2020 Vurugu za Siasa ni za wendawazimu wasiopenda nchi yao na watu wake

TUMI EPAFRA

Member
Jul 12, 2020
59
56
Utakuwa upumbavu wa hali ya juu kufanya vurugu za kisiasa, kupigana na kupoteza maisha kwa ajili ya mtu mmoja au wachache wapate wadhifa wa kula na kuishi vizuri zaidi.

Upumbavu huu umefanyika nchi nyingi, lakini mfano mzuri ni Libya ambako wanajuta kumpindua Gaddafi. Yani wao wakae makwao waangalie kwenye TV jinsi wajinga wanavyo pigana kwa ajili yao, huo ni utumwa wa akili mbaya kuliko wa mzungu.

Wagombea wakisha chaguliwa hawajali wananchi tena, hasa wale wanao chaguliwa kwa mapinduzi au kura za vurugu au njia yeyote isiyo ya amani, kwa ujumla wanolazimisha kushinda.

Amani ya nchi yetu ipo hatiani, sababu ya kwanza ni kizazi kipya chenye hasira na maghabu na chuki za wenyewe kwa wenyewe, lakini sababu kuu ni siasa pasipo na demokrasia.

Vijana wa sasa sijui ni mitandaoni tu au hata mitaani, wanaghadhabu za maisha sana, na kwa yote yanayowashinda kimaisha wanailamu serikali.

Lakini maendeleo ya mtu mmoja mmoja ndiyo maendeleo ya nchi, tujifunze kwa wenzetu walioendelea na kwa nini wameendelea. Sababu kubwa ni wabunifu wa kujitengenezea ajira na wana ujuzi wa kuunda vitu mbalimbali kudumisha viwanda na biashara ambazo zinatengeneza ajira.

Hata nchi za magharibi zinahangaika na ajira, hazina za kutosha wote, pamoja na biashara zao zote kwa sababu wameua viwanda vyao kwa kuvihamishia mashariki ya kati na mbali

Hivyo kutatua tatizo la ajira lazima tuwe na viwanda vya kutosha kama Jitihada za awamu ya tano zinavyofanya, lakini pia lazima vijana wajiandae kwa elimu ya teknolojia na viwanda, ili waajiriwe na viwanda hivyo, hata pia kubuni bidhaa mbalimbali ili tukomeshe uagizaji wa kila kitu toka Ulaya na China, unaotugharimu kiasi kikubwa sana na kudumisha umasikini. Kwa kifupi siye ni soko la China na Ulaya, na wao ndiyo wanavyotaka tuwe kwa manufaa yao.
 
Back
Top Bottom