Vurugu za machinga: Tunahitaji sera mpya..

Timothy Peter Thomas

Senior Member
Joined
Jan 23, 2013
Posts
114
Reaction score
48
Migogoro baina ya aserikali na wachuuzi wa biashara ndogondogo imekuwa jambo lililozoeleka sasa. Wafanyabiashara hawa wameendelea kung'ang'ania kufanya biashara zao mijini ambapo kimsingi ndipo palipo na soko la bidhaa yao, huku Serikali, kupitia mamlaka za miji na jeshi la polisi wakiwatimua.. Ipo haja ya kuwa na suluhisho katika hili kwa kuja na sera endelevu itakayosimamia biashara hii. Maisha yamekuwa magumu jaman, anayefanya kazi kwa jitihada zake tusimzuie., tunataka wakaibe? Sera iwaelekeze kwenye kuanzisha vyama vyao vya wafanyabiashara ambavyo vitasimamia mazungumzo baina yao na serikali. Serikali iainishe maeneo yote muhimu ambayo machinga watafanyia biashara, na tena wawe na uhakika wa biashara. Tatu, serikali ikubaliane nao kuwa na muda/vipindi maalumu vya kufanya biashara.. Tuikumbuke mifano michache tu.. Mwanzoni mwa mwaka huu Serikali iliwaondoa wafanyabiashara wote maeneo ya Ubungo.. Leo nenda ubungo jioni ujionee jinsi wafanyabiashara walivyofurika..
HUWEZI KUZUIA NYUMBA ILIYOTOBOKA PAA KUVUJA KWA KUBANDIKA MAKARATASI..
 
Sheria za nchi lazima zifuatwe, wao kama wanafanya biashara maeneo yasiyo ruhusiwa wafanywe nini? . Hapo jibu ni wao kuondoshwa kwa nguvu tu, wamewekewa maeneo yao hawataki kwenda . Tumeona Dar wamejengewa machinga complex hawataki kwenda. Tuache siasa, tufuate sheria.
 
Sheria zimetungwa kwa ajili ya wananchi. Kama sheria haziwanufaishi wananchi wote zina manufaa gani? Sheria ya kuwatimua machinga mijini imemnufaisha nani?
 
Lipo suluhisho moja tu kwa tatizo la wafanyabiashara holela... Serikali ifungue maeneo mengi zaidi ya kilimo, iwezeshe uanzishwaji wa viwanda vidogo vya kusindika mazao ya kilimo, isaidia kupatikana na uimara wa masoko ya mazao ya kilimo na iimarishe miundombinu na huduma za jamii maeneo ya pembezoni... Tatizo la vijana kujirundika mijini litakauka kama umande...
 
Sheria za nchi lazima zifuatwe, wao kama wanafanya biashara maeneo yasiyo ruhusiwa wafanywe nini? . Hapo jibu ni wao kuondoshwa kwa nguvu tu, wamewekewa maeneo yao hawataki kwenda . Tumeona Dar wamejengewa machinga complex hawataki kwenda. Tuache siasa, tufuate sheria.

Wewe una akili kubwa sana, Ila angalia ile gharama ya pango iliyowekwa pale machinga complex inaweza kulipwa kwa mtaji walionao na biashara machinga?
 
Serikali ni wanyonyaji sana zile machinga complex hawana hela machinga kupangisha kutokana na mitaji yao kuwa midogo. Lakini pia yawezekana hata wakishushiwa bei wasiende kwa sababu wanakwepa kodi

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Migogoro baina ya aserikali na wachuuzi wa biashara ndogondogo imekuwa jambo lililozoeleka sasa. Wafanyabiashara hawa wameendelea kung'ang'ania kufanya biashara zao mijini ambapo kimsingi ndipo palipo na soko la bidhaa yao, huku Serikali, kupitia mamlaka za miji na jeshi la polisi wakiwatimua.. Ipo haja ya kuwa na suluhisho katika hili kwa kuja na sera endelevu itakayosimamia biashara hii. Maisha yamekuwa magumu jaman, anayefanya kazi kwa jitihada zake tusimzuie., tunataka wakaibe? Sera iwaelekeze kwenye kuanzisha vyama vyao vya wafanyabiashara ambavyo vitasimamia mazungumzo baina yao na serikali. Serikali iainishe maeneo yote muhimu ambayo machinga watafanyia biashara, na tena wawe na uhakika wa biashara. Tatu, serikali ikubaliane nao kuwa na muda/vipindi maalumu vya kufanya biashara.. Tuikumbuke mifano michache tu.. Mwanzoni mwa mwaka huu Serikali iliwaondoa wafanyabiashara wote maeneo ya Ubungo.. Leo nenda ubungo jioni ujionee jinsi wafanyabiashara walivyofurika..
HUWEZI KUZUIA NYUMBA ILIYOTOBOKA PAA KUVUJA KWA KUBANDIKA MAKARATASI..

CCM imebobea kwenye SIASA MPYA za NEOLIBERALISM... kwahiyo VITU na WATU wadogo wadogo hawafikiriwi kwenye Siasa hizo... Bye Bye Socialism... CCM ni officially CENTRAL WRIGHT PARTY kama hamjui

580px-EffectOfTariff.svg.png
 
Back
Top Bottom